Kutongoza kwa maandiko

Kutongoza kwa maandiko

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,367
Jamaa: Hello mrembo, samahani, una
mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana
Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe
peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8
"Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa
maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe
unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana,
kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo
wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba
we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na
nchi zitapita; lakini maneno yangu
hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu?
Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi
wamefanya mema, Lakini wewe umewapita
wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi
kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi
wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako
hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata
sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali
mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na
mama yake naye ataambatana na mkewe,
nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua
maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati
kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku, upate
kuangalia kutenda sawasawa na maneno
yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo
utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana
Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya
kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule
anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda
nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu
zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo
yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki,
yo yote yaliyo safi, yo yote yenye
kupendeza, yo yote yenye sifa njema;
ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri
yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali.
Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"


C.C sakapal Heaven on earth Passion Lady Mzee Vinci Angel Nylon Mikataba feki Katavi Mamndenyi kiwatengu figganigga
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha.Juzi juzi tu nimetumia kitabu cha Mwanzo kutongoza,tena hizo swaga zinasaidia sana asee.Umenigusa kwa kweli.
 
Mtumishi umeamua kuja kihivyo,
Ongeza na haya hapa japo siku hizi ni pesa mbele,
wanasema haya maneno wanayajua toka wakiwa sunday schools
[TABLE="width: 657"]
[TR]
[TD="class: xl67, width: 82, bgcolor: transparent"]2 Timotheo[/TD]
[TD="class: xl65, width: 28, bgcolor: transparent"]3[/TD]
[TD="class: xl65, width: 28, bgcolor: transparent"]16[/TD]
[TD="class: xl66, width: 737, bgcolor: transparent"]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
ha ha ha....watumishi wa mungu hao, hapo kama binti ni mlokole hachomoi kabisa Excellent :tape:
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha....watumishi wa mungu hao, hapo kama binti ni mlokole hachomoi kabisa Excellent :tape:
style nyingine ya kutongoza kadem kama ni mlokole unaenda kilokole,unatongoza kutokana na jinsi alivyojiweka
 
Mtumishi umeamua kuja kihivyo,
Ongeza na haya hapa japo siku hizi ni pesa mbele,
wanasema haya maneno wanayajua toka wakiwa sunday schools
[TABLE="width: 657"]
[TR]
[TD="class: xl67, width: 82, bgcolor: transparent"]2 Timotheo[/TD]
[TD="class: xl65, width: 28, bgcolor: transparent"]3[/TD]
[TD="class: xl65, width: 28, bgcolor: transparent"]16[/TD]
[TD="class: xl66, width: 737, bgcolor: transparent"]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
kesho usisahau kuja kanisani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom