KERO Kutolipwa kwa wakati kwa wakandarasi

KERO Kutolipwa kwa wakati kwa wakandarasi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,198
Kumekuwa na kilio kwa Wakandarasi kutolipwa kwa wakati huku wakimaliza kazi zao na kukaguliwa na mamlaka na kuthibitisha kuwa kazi zao ziko sahihi na wanatakiwa walipwe.

Ikumbukwe kuwa Bunge letu lilipitisha sheria ya kila anayeweka mafuta kwenye gari lake sharti aichangie Tanroads/Tarura kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Fedha hizi zinaingia kwenye akaunti maalum ili wakandarasi wanapomaliza matengenezo inabidi walipwe kutoka kwenye akaunti hiyo.

Ninauliza swali. Je kama fedha hizi zina akunti maalum na kila kukicha wananchi wanatozwa fedha kila wanapoweka mafuta. Kwa nini kuwe na malalamiko ya wakandarasi?

Isije ikawa fedha hizi zinaelekezwa kwenye matumizi mengine nje ya kusudio iliyoanzisha sheria ya tozo hizi. Serikali itende haki kwa wakandarasi waliomaliza kazi zao kwa usahihi.
 
Back
Top Bottom