Kutokwa jasho jingi wakati wa kula chakula

babu kassamya

Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
15
Reaction score
10
Nima mwanangu ana umri wa miaka 15 akianza kula jasho linamtoka sana kama amemwagiwa maji hata kama kuna baridi kiasi gani na ana mwili mkubwa. Je wana JF huu ni ugonjwa au ni nini naombe msaada mnijuze.
 
Mchunguze akila kitu gani anatoka jasho watu wengi wakila chakula cha moto wanatoka jasho pamoja na maji mm nimuhanga wao nikila chakula cha moto kwa mbali lazime nitoke jasho haijalishi hata kama kuna Ac na issue nyengine ni maji nikinywa lazima jasho lianze kutiririka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kiongozi..kwa nyongeza, acheki kiwango cha insulini kwenye damu, huenda anaelekea kupatwa na balaa la kisukari
Kumbe ukiwa na kisukari unatokwa jasho eeh?Mimi nina kisukari huwa natokwa na jasho sana usiku.Sasa nimepata jibu.
 
Una kisukari cha kutumia dawa kabisa yani dozi, ama ni kile cha mbaaali. Unatumia dozi?
 
Nima mwanangu ana umri wa miaka 15 akianza kula jasho linamtoka sana kama amemwagiwa maji hata kama kuna baridi kiasi gani na ana mwili mkubwa. Je wana JF huu ni ugonjwa au ni nini naombe msaada mnijuze.
Kisukari saiv rika zote wanapata, vyakula na mtindo WA maisha vinachangia Sana.. Jitahidi kwenye vyakula apunguze huo ubonge ....
 
Nima mwanangu ana umri wa miaka 15 akianza kula jasho linamtoka sana kama amemwagiwa maji hata kama kuna baridi kiasi gani na ana mwili mkubwa. Je wana JF huu ni ugonjwa au ni nini naombe msaada mnijuze.
Habari,
Ni vyema kufika hospitali na kuwaona wataalamu wa afya ili kufanya majumuisho ya afya ya kijana wako.
Kwani kwa hapa kuna vitu inawezekana ukawa hujavieleza lakini ni mhimu kama:
1: kiasi cha uongezekaji wa uzito kulingana na muda
2: hamu yake ya kula
3: kiasi cha chakula anachokula kwa siku

Lakini pia kuna vitu atahitajika kuulizwa mwenyewe kama:
1: mwenendo wa mapigo ya moyo
2: upataji wake wa kiu
3: upataji wa haja ndogo
4: uwezo wake wa kuhimili joto au baridi
5: kutetemeka kwa vidole

Mwisho, ataweza kufanyiwa vipimo kulingana na majumuisho hapo juu na daktari atakapomfanyia ukaguzi/examination.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom