Valentina
R I P
- Oct 12, 2013
- 24,688
- 28,850
Hongera kwa hiloUlichokifanya ni kitu kizuri sana na kinaweza kudumisha urafiki wenu ukawa sio wa kutenda dhambi ...
Nakumbuka kuna dada mmoja nilimkaribisha, alipofika nikampeleka hotelini akapumzika, nilipotoka kazini nikampigia sim akaja nilipokuwa tukaendelea na maongezi .. vinywaji na samaki choma kama kawa (enzi za Rolay Pub - Mwanza city); ilipofika mida ya saa moja usiku tukatoka kwenda kiwanja kingine kikubwa tu; (ilikuwa Ijumaa). Mida ya saa 4 usiku nilimsindikiza na kumrudisha hotelini - mi nikaenda zangu nyumbani. Kesho yake mida ya saa 4 asbh alinipigia simu hili tukutane kwa ajili ya breakfast; nilienda na tulikaa vizuri tukaendelea na maongezi mengi tu zaidi ikiwa ni kufahamiana kwa undani zaidi.
J/mosi jioni aliondoka kurudi kwao ....
Tuliendelea na mawasiliano ya hapa na pale ...
Baada ya hapo ... amekuwa rafiki mkubwa sana kiasi kwamba hadi nyumbani kwangu anakuja, nami kwake naenda. Hatuna hata dalili za kutenda dhambi hiyo .. tunashirikishana kwenye mambo mengi ya kimaisha ... ila ...
Kitu alichonambia baada ya kuwa na ukaribu kwa zaidi ya miezi sita ni kwamba ni hivi .. namnukuhu... "Nilikuona mwanaume wa tofauti sana kulipa chumba alafu ukaniaga na kwenda nyumbani kwako"