Kutoka viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe Mbeya, Mkutano wa Edward Lowassa

Mbona Kama Alikuwa Wanataka Kuhutubia Muda MREFU, Sasa Iweje Ameondoka Saa 11!! Mbona Hajaendelea Hadi Saa 12!! Mkutano Wenyewe Kisukuma Tu, Mgombea Urais Kisukuma, Mgombea Ubunge Charles Kitwanga Kisukuma, Wagombea Udiwani Ndio Balaa Kisukuma Tupu! Kama Majukwaani Tena Live Hali Ndio Hivi, Je Huko Mitaani!!!?
 

ITV kama ITV hawajawahi kuwa na OB Van, hivyo ITV kama ITV yenyewe tuu, hawawezi kutangaza live kutoka Mbeya au kutoka mahali popote nje ya jiji la Dar es Salaam kwa sababu wanatumia teknolojia ya Microwave link!.

Ili ITV waweze kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka mahali popote nje ya Dar es Salaam, ni lazima matangazo hayo yapitie satelite link ama ya TBC, Star TV au Azam TV!. Hivi ndivyo vituo vitatu pekee nchini Tanzania vyenye satelite link!. Star Times pia wana satelite link ila link yao kwa Tanzania ni downward link tuu, yaani unaweza kupokea, na sio upward link, huwezi kupandisha!. Upward link yao iko China!. Wengine wenye downward link ni DSTV, wao upward link yao iko South Afrika!.

Hivyo kama ITV hawana satelite upward link hivyo wanarusha kupitia link ya Azam, sielewi kabisa kwa nini matangazo yakatike unless wanaozingua ni hao Azam!. Kama Azam yuko hewani na hakatiki, then, ITV inachotakiwa ni kuacha pride tuu ya kuwapaisha Azam kupitia ITV, wanachotakiwa ni ku loop na kurusha Azam watu tuone kinachoendelea hata ikibidi kumkosa Spenser Lameck na tumkose tuu ila Lowassa tumpate!.

Pasco

Umeeleweka Mkuu Pasco. Ila niko najiuliza haya unayoyasema ina maana hawa viongozi wa UKAWA (Chadema NLD NCCR na CUF) walikuwa hawajui mapunguifu haya ya ITV kufikia hatua ya kuikabidhi jukumu hili la kurusha matangazo??? This is ridiculous, sarcastic and unthinkable!!!!

UKAWA waanze kujipanga upya wanapopanga kurusha matangazo ya siku ya kufunga kampeni kutokea maeneo mawili Jangwani (Timu: Lowassa, Duni, Kingunge & Mbowe) na Mwanza (Timu: Sumaye, Wenje, Mgeja). Kama wanaweza wakomboe hela zo huko wazipeleke zote huko Azam.

Hao waliowachagua ITV kuwa Super Brand nawaona hawakuwa makini. Super Brand gani hii ni Inferior brand, kudadeki
 
kwa mara ya kwanza kuangalia mkutano wao live kupitia azamtv ni vituko au maigizo mgombea urais sijamuelewa wala sijaona akitangaza ilani ya chama mr ziro naye ni vituko kama mchezo wa maigizo mbowe akimuonya jk ni maajabu
 

Umeeleweka Mkuu Pasco. Ila niko najiuliza haya unayoyasema ina maana hawa viongozi wa UKAWA (Chadema NLD NCCR na CUF) walikuwa hawajui mapunguifu haya ya ITV kufikia hatua ya kuikabidhi jukumu hili la kurusha matangazo??? This is ridiculous, sarcastic and unthinkable!!!!
Ni uzembe wako wa kutonunua Azam decoder.
 
Ni kweli mwanzo tulikosa Rais hapa mbeya kwani hatuwezi kuongozwa na mtu dhaifu kama jk kwa sasa tumepata Lowassa rais wetu mpya.
You are very right.

Sugu aliupata huo wadhifa wa 'Urais' kutokana na udhaifu wa JK.

Kwa kuwa hivi sasa kuna mgombea 'strong' Edward Lowassa ambaye anagombea Urais kwa tiketi ya Chadema na anaelekea kuupata hapo Oktoba 25 na yeye Sugu anagombea ubunge wa Mbeya mjini, kwa hiyo naamini EL yuko sahihi kabisa kuwaambia wakazi wa Mbeya wamwite yeye Rais na wamwite Sugu mbunge.
 
umasikini mbaya leo startime imenizingua mwanzo mwisho yaani sioni kitu hapa
 
Ndio hivyo... am very disappointed..!!
This is very disgusting...hujuma hujuma iko wazi kwa mikutano ya Live yote ya UKAWA ikiwa ITV inarusha...

Ukidhania utani, ngoja narusha picha hapa.... nimevunja vunja KINGAMUZI CHA STAR TIMES.. nimenunua mwenyewe, nimevunja mwenyewe, Kesho mapema naenda AZAM TV... kununua king'amuzi chao...!!!

ITV, TBC1, TBC2, Star TV... i deleted you katika UCHAGUZI HUU...!!!

Azam TV... ndio mpango sasa..!!

Masikini wewe, umevunja king'amuzi bure!, tatizo sio king'amuzi tatizo ni signal!. Kazi ya king'amuzi ni kupokea tuu signal, na kuzionyesha kwenye TV yako!, tatizo la live ya leo ni kukatika katika kwa signal kutoka Mbeya na sio king'amuzi!.

Kazi ya mkono ni kuchota chakula kutoka kwenye sahani kupeleka mdomoni!. Unapokuta hakuna chakula kwenye sahani cha kupeleka mdomoni, utaukata mkono?!.

Kingamuzi ni mkono too wa kufeed signal wewe uone!, signal hakuna kosa la king'amuzi ni lipi?!.

Pasco
 
ITV kuna uzembe fulani!

We unatumia kingamuz cha star time? Unajua star time ni mali ya nani? Halafu ndani ya star time ndiyo kunapatikana chanel ya itv star time ndiyo wamefanya hujuma! Azam walikuwa wanarusha matangazo na ilikuwa clear
 
mbona azam tv wako live ....mda wote tena wanaonekana vzuri sana.....ndio maana ukawa walichukua coverage ya vituo viwili itv na azm tv...vipi una lingine la kusema
Unalinganisha coverage ya Azam TV na ITV, anachotaka adui ni kufanya maximum damage inawezekana amechagua ITV kwa sababu inaonekana nchi nzima.
 
...
1. Hawafuati sheria na taratibu za chama...
Poh, kwa hiyo Chadema walifuata "taratibu" za chama kuhusu Lowassa? Usitake kufanya watu wengine wajinga. aisee. Huyo mzee wenu amechanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom