Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
-
- #61
upo sahihi kabisa rafiki,...umeongea jambo la maana sana,
ni jukumu letu wanaume 'kumlinda' mke na hao ndugu.
Wakati huo huo, ni jukumu letu pia kulinda hadhi ya familia kwa huyo mke,
sio mwanaume unakuwa haujitambui,...unapelekeshwa tu kama bendera fata upepo!
Kwenye ndoa hakuna classes kusema ati mama mzazi ndio 1st Class, 2nd Class mawifi, na 3rd Class Mkeo
au Vice Versa...! Kwenye ndoa kila mtu ana mipaka yake, na hiyo mipaka izingatiwe na kuheshimiwa hata ikibidi
kwa 'kununiana!'
kuna wamama hawana say kwenye familia.....yap, ni kizaazaa kiukweli, yote yawezekana, lakini kutokana na hili mwanamke ulishindwa kucheza nafasi yako kunusuru haya yasitokee? nimesoma pia wamehama kwenye villa waliyokuwa wanaishi pamoja, sasa wewe mwanamke unaejua una ishu na hii familia ungecheza part yako kuweka mambo sawa ili wao ndio wajione wajinga, sidhani kama kuna mwanamke aliyeolewa hajapitia kashkash za ndoa, kama wapo wamebarikiwa, mie nilipitia na wifi/mama mkwe, mgogoro haswaaaa, lakini nilipambana baba mkwe wangu ni bonge la muelewa alinisaidia sana katika kizaazaa nilichopitia, hapo ningesema ninunue kesi ingekuwa mtafaruku mkubwa sana,msukuma alikuwa hakubaliani na mama/dada yake hata kidogo, na kama sio mimi kumtuliza ingeshazaa mtafakuru haswaa, nililaumiwa kwa kila namna lakini nilipambana na sasa hivi ni marafiki zangu wakubwa sana, tunapopitia changamoto kwenye ndoa tusizikuze/chochea, bali tuangalie namna ya kupambana nazo.
Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?
hata mke/mume siyo mmiliki wa mwenzi wake, mmiliki ni Mungu pekee ndo maana anakuleta na kukuchukua siku anayoitaka yeye.
Malezi yanakuwepo kwa zamu. Mama anaanza..... baba/dada/shangazi n.k wanaendelea...... mume/mke anamalizia. tumia ujuzi wako woote kumlea mtu anapokuwa mikononi mwako, akiondoka kubali kuwa sasa ni zamu ya wengine kulea.
Kuna kaswali najiulizaga, hivi wazazi wa wanawake huwa hawana uchungu na watoto wao? mbona hakuna migogoro hii ya kijinga inayotoka huko? binti akishaolewa wazazi hujiweka kando kabisaaaaaa.
Lile swala la kuacha baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzio huwa ni kwa wamama tu?
kuna wamama hawana say kwenye familia.....
mume akisema leo woooteeeee tunavaa bukta kwenda mazoezi basi ndo hivyo inavyokuwa, hata kama wewe si mtu wa mazoezi. Mke wa Peter anachukiwa tu, na wanadhani labda kwa sababu ya umri wake kumzidi mume basi yeye ndo msemaji wa familia. Inawezekana kabisa Lola hana say kwa Peter, kwa hiyo hata swala la kuhama asingekuwa na uwezo wa kubishia.
Kuna mkaka alihama nyumba akamwacha mke na watoto ndani sababu mke alikuwa anakataa kuhama. ni stori ndefu, lakini mwisho wa siku bibie mwenyewe alifungasha virago na kumfwata huko alikoenda
Umeona eeeh! nasi tunapendwa sana kwetu na wazazi wetu wanatamani sana wangeendelea kubaki na sisi. Nikiangalia mamangu kwa sasa yupo peke yake (baada ya baba kufariki) amebaki kuokota tu watoto wa barabarani akae nao. unafikiri asingetamani angalau mmoja wetu abaki naye?umenikumbusha mbali, enzi nikikorofishana na msukuma nilikuwa nakimbilia kupumzika kwa mama nyamayao, basi nikifika kule nampa stori weee, anaishilia kusema yaani jamani sijui kwanini hamkuwa wanaume wanangu, mana nina nyie wawili tu lakini hizo familia za waume zenu wapo wanne kuendelea mbona hawanionei huruma na wanangu? hahahaha akimaanisha tungekuwa wanaume tusingekuwa tunakimbia kimbia vile, malalamishi/masimango huku kule, mweeh, lakini kila kitu kina muda wake, wengine tumepitia hiyo michakato sasa hivi tupo shwari kabisa, tumebakia kuwa wasikilizaji/watazamaji.
huo ni upepo tu, utapita......hilo linawezekana sana pia, naona Jude mwenyewe ameshindwa kuweka mambo sawa mana na yeye ni mmoja wa mlalamishi kuhusu kuolewa kwa Lola, anasema mbona hakumuoa Lola wakati mama yao yupo hai, kitu kinachoonyesha kwamba familia ilikuwa haimkubali Lola kuanzia mwanzo, lakini hii mitafaruku ya familia hii aisee, kama inaweza kuombewa/kuepukwa na iepukwe kwa gharama yoyote ile, imagine P2 walivyotoka mbali, walivyojitahidi kupata mafanikio waliyonayo mpaka kufikia hapo, leo "mtafaruku" unasambaratisha familia.
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana
AMINA!!!!!!mimi huwa namwambia wife bila wewe siwezi fanikiwa na nikweli Mungu ametubariki kwa kila eneo. Na ndio mpango wa Mungu mke ana sehemu kubwa sana kwa mafanikio ya mme wake. Na sisi tunaoamini katika Yesu mke akilia, akikwazika, akisikitika, akinuna mwanaume tambua hutafanikiwa hata iweje. wanawake Mungu awabariki sana maana bila nyie sisi hatujakamilika na itabaki hivyo milele!!
Khe kumbe umeoa........... too bad for me lol
Umeona eeeh! nasi tunapendwa sana kwetu na wazazi wetu wanatamani sana wangeendelea kubaki na sisi. Nikiangalia mamangu kwa sasa yupo peke yake (baada ya baba kufariki) amebaki kuokota tu watoto wa barabarani akae nao. unafikiri asingetamani angalau mmoja wetu abaki naye?
huo ni upepo tu, utapita......
Ila Jude ana uhakika gani kama Peter asingemuoa mkewe mamake angeendelea kuishi?
wamama wangapi wamekataa wanawe kuoa mwanamke fulani na still wakaoa na wao wapo hai?
Muda wao wa kuona haukuwa tayari hata kama walishaanza kuzaa watoto
AMINA!!!!!!
Ila na ndugu zako wanafahamu hilo?
Je unapokuwa na mgongano kidogo na ndugu zako (wazazi, siblings, ndugu), mkeo hashutumiwi kuwa ni chanzo?
...hii yote inatokana na dhana ya kwamba nani ana haki zaidi juu yako (Mume)...
1. Mama mzazi anajiona yeye kalea mimba, amezaa na kuteseka na ulezi wa kichanga mpaka kufikia kutembea, kusema na mwishowe kujitegemea...
2. Madada (Mawifi) hawa huona wao ni ndugu toka nitoke....wamezaliwa tumbo moja na ndugu yao, wanajihisi wanauchungu wa damu kuliko weye Mke mtu baki tu ambaye hata ukiachika ataolewa mwingine...
3. Mke, ....huyu anajiona yeye ndiye aliyechaguliwa kuwa mama wa watoto wa huyo Bwana Mkubwa, Mwenza na mengineyo mengi yakiwemo faragha faraghani....!
Ni ubinafsi na "wivu" wa kijinga tu ambao wanawake wengi wamejaaliwa nao!
watu kutojua mipaka yao.Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?
hata mke/mume siyo mmiliki wa mwenzi wake, mmiliki ni Mungu pekee ndo maana anakuleta na kukuchukua siku anayoitaka yeye.
Malezi yanakuwepo kwa zamu. Mama anaanza..... baba/dada/shangazi n.k wanaendelea...... mume/mke anamalizia. tumia ujuzi wako woote kumlea mtu anapokuwa mikononi mwako, akiondoka kubali kuwa sasa ni zamu ya wengine kulea.
Kuna kaswali najiulizaga, hivi wazazi wa wanawake huwa hawana uchungu na watoto wao? mbona hakuna migogoro hii ya kijinga inayotoka huko? binti akishaolewa wazazi hujiweka kando kabisaaaaaa.
Lile swala la kuacha baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzio huwa ni kwa wamama tu?
.....Enheee! Umeona sasa...!? Misuguano ya kifikra huanza namna hii.
....mimi nimetumia neno HAKI kwa maana ya Rights,
wewe umetafsiri na kumaanisha UMILIKI kwa maana ya OWNERSHIP au sio?
Once watapoweza kutofautisha "dhana" hizi mbili na wote kujitambua haki za msingi
hakutakuwa na mivutano namna hii....
Ni kiasi cha kujitambua tu.
Topic nzuri, naifuatilia kwa karibu beste.
Wakwe ni janga la dunia, ingawa kwa nchi maskini linakuwa kubwa zaidi.
wanajua sana! im very tough. issue inabakia wewe mwanaume unasimama wapi. yani mme akiwa bendera fuata upepo mke anapata shida sana. mke wangu ni mpole sana na wala sio muongeaji sasa akikutana na ndugu mdomo mdomo ni shughuli sana sasa hapo mme ndo usimame. ili ufanikiwe inabidi muwe na by-laws za nyumbani and should be adhered