Kutoka Mwakyembe hadi Zitto Kabwe

Kutoka Mwakyembe hadi Zitto Kabwe

Hao ambao walio bora wana kipi cha kitaifa wanachokisimamia?kazi yao ni kupiga hela ili kufifisha harakati
 
Mwakyembe na Lembeni ni kutoka chama tawala. Sasa kwa mara ya kwanza mwenyekiti wa kamati kutoka chama pinzani anapewa nafasi ya kuishikisha adabu serikali,tusubiri tuone.
Mwanzo nilikuwa na mashaka kidogo na dhamira ya Zitto ila nilipokumbuka matusi ya Werema kwa Zitto na jinsi alivyomuaibisha wakati ule wa sakata la fedha za Uswiss na jinsi alivyo apa kumkata kichwa swahiba wa Zitto aliyeibua mambo yaani Kafulila na pia kumwita Tumbili naiona kabisa kasi na shambulio la nguvu za hoja atakalokuja nalo Zitto wallah linatisha.
 
Kwa jinsi Hamasa ya huu mchezo ulivyo naona dhahiri Zitto Kabwe akipaisha hii penalt Au kuigongesha mwamba na ushindi uende pasipotarajiwa..........binafsi nimekaa moyo unadunda Zitto atatutoa kimasomaso Au kichwa ChiNi? Nasubiria hiyo Siku.
...penalt hii itakua mpira wa kurushwa...
 
Zitto afanikiwe asifanikiwe bado ni mtu wa kupigiwa mfano katika Taifa hili.
 
Tofauti ya hawa watu watatu ni mwakyembe na lembeli walikusanya data wenyewe ndo mana kwa riport ya mwakyembe mkuu wa pccb dr hosea alipaswa kung'oka, tofauti na zito ameletewa data ambazo zimepitia kwa hosea na waziri mkuu hapa nn unategemea, ni kiini macho, kuna manaibu mawazir wadogo sana wamekwisha andaliwa kisaikolojia watolewe kafara
 
Hii kashfa na ufisadi huu sio tu kwamba watu waachie ngazi, bali kwa mara ya kwanza tuone wakizitema hizi fedha za umma. Kwa hili labda nitaukumbuka utawala huu kwa kitu ilichokifanya.
 
Naona kwa karibuuu PINDA AKIJIUZULU...!!! Nimeona...!!!
 
Yaani Baraza la Mawaziri livunjwe na Raisi ajiuzuru
 
hili limuvie sijui litaishaje maana tayari scrash tayari zimeanza na na ndo maana najiuliza hii muvi itaisha salama kweli.
 
Kwa jinsi Hamasa ya huu mchezo ulivyo naona dhahiri Zitto Kabwe akipaisha hii penalt Au kuigongesha mwamba na ushindi uende pasipotarajiwa..........binafsi nimekaa moyo unadunda Zitto atatutoa kimasomaso Au kichwa ChiNi? Nasubiria hiyo Siku.

Mpira utapita juu ya goli na kudondokea nje ya uwanja na vijana wataoenda kuuokota hawatauona kamwe.
 
Mwenyekiti wa PAC {zitto} simwamini ila makamu mwenyekiti wake {Filikunjombe} namwamini.
ila ngoja tuendelee kuvuta subira.
 
Hiyo ripoti itasomwa lini? Hebu tujuzane ili tutege masikio yetu
 
Back
Top Bottom