VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hii sasa ni zamu rasmi ya Zitto Kabwe. Zamu ya kuongea ukweli mchungu kwa wenye nyadhifa serikalini na kuwachomoa walipo. Kuwafanya wajiuzulu kwa kashfa za moja kwa moja au kuwajibika kwa pamoja kama si mkuu wa mahali fulani. Zitto amekabidhiwa penati ya mwisho ya ushindi au kushindwa.
Mwaka 2008 ilikuwa zamu ya Dr. Harrison Mwakyembe. Alilishughulikia ipasavyo suala la Richmond na kuwaangusha wahusika, akina Lowassa,Karamagi,Msabaha na wengineo. Dr. Mwakyembe,akisaidiwa na weledi wake wa sheria,alikusanya nyaraka na shahidi nyingine kuuambia umma ukweli na kusafisha serikali.
Mwaka 2013,ikawa zamu ya Ndugu yangu James Lembeli. Akaishughulikia ipasavyo kadhia ya Operesheni Tokomeza kwa ustadi mkubwa. Hatimaye,akina Mathayo,Nahodha na Kagasheki wakaacha nyadhifa zao. Serikali ikajivua gamba.
Zitto,ambaye kitaaluma ni mchumi,anapaswa kuvaa viatu vya Mwakyembe na Lembeli. Kuibuka na uthibitisho wa uharamu wa jambo husika na kusafisha serikali. Kiukweli, Zitto ana kazi ngumu mbele yake. Ushahidi,watuhumiwa na hatma yao.Vyote viwepo.
Kuna jambo halijulikani kwa wengi. Kwa kadhia kama hizi,mwenye nchi huwa na taarifa na amesharidhia la kusemwa lisemwe;la kutendwa litendwe. Hivyobasi,waongozaji kama Mwakyembe, Lembeli na Zitto "hulindwa".Na waongozaji wote huwa watu wa "mfumo".
Twende taratibu tujionee. Ni zamu ya Zitto
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam