Kutoka Mahakama Kuu kanda ya Dar: Usikilizwaji wa uamuzi wa pingamizi la Zitto

Status
Not open for further replies.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Wakuu kumepambazuka vema,

Viunga vya mahakama kuu vimetulia, watu wakiendelea kuwasili tayari kwa usikilizwaji wa pingamizi la Zitto Kabwe kutaka kamati kuu ya chadema isijadili utetezi wake,

Tumejiandaa vema kuwaletea kinachojiri na kuzuia upotoshaji mkubwa uliofanywa jana na kundi la wasaliti hawa wa mageuzi,

NB

Kamati kuu ya chadema inaanza kikao chake kama kawaida hivi punde na Zitto ataanza kutajwa ndani ya vikao hivyo baada ya saa tatu kamili asubuhi hii,

Pipoooooz!!!!!!!


UPDATES

Bado ukumbi wa kusikiliziwa shauri husika haujapangwa, nimeelezwa na mapokezi kuwa hivi punde watapanga na shauri litaanza kusomwa saa tatu,

Makamanda wengi wamashawasili, pikipiki zenye bendera za chadema zimetanda mahakamani,

Hali ya hewa ni nzuri ambapo nyuzi joto linakadiriwa kuwa 26 tu hivyo makamanda waliovalia suti wapo salama kabisa,


Tunaendelea .....


APDATES


Zitto yupo hapa mahakamani tangu saa 12 asubuhi, amejificha kwenye gari aina ya Carina no T564 CAS, anawalinzi wa nne wenye miili dhaifu (fizikali), kwakumuonyesha kuwa nimemuona, nimeenda kuengemea gari hiyo hiyo na huku napost updates,


Naaaam

Tumeruhusiwa kuingia ukumbini na kila mtu ametakiwa kuandika jina lale kwenye kitabu cha wageni wa mahakama,


Haya Zitto nae ameshushwa kwenye gari na wapambe wake wanne, anaingia sasa nae mahakamani,


Wooooooooiiiiii Zitto anazomewaaaaaa CCMmmmmmmmmm, duuuuuh hii hatari ukumbi mzima umelipuka kwakumzomea, alianza kuwambia watu pipoziii, hahaa watu wakamjibu kwa kumzomea sana,

naaam watu wametulia wakimsubili jaji Utamwa aje akate mzizi wa fitina

UPDATES,

Wakili wa Zitto Bwana Msando ameshawasili, hahaa kaja moja kwa moja kunishika mkono, sijasita, nimemsalimia tena kwakicheko huku nikimwambia leo mnapigwa chini rasmi,


Bado mawakili wa Chadema bado hawajafika, tunawasubiri


UPDATES,

Mwanasheria mashuhuri katika ardhi ya Tanzania ndugu Tundu Lissu ndio anawasili, wapi pipooooooz!!!!

Watu wanashangilia hamna mfanoooooooo!


Heheeee kweli nguvu ya umma ni balaaa


UPDATES,

Wakili Kibatala ameingia, watu wanaendelea kushangilia,


Saaa tunamsubiri jaji Utamwa tu


UPDATES

Mawakili wa pande zote waliitwa ndani kwaajili ya kuambiwa kinachoendelea,

Mh Lisu ametoka na kutuambia tutulie kwa sasa Jaji anaandaa, na shauri la msingi litaanza saa nne, vivyo hivyo ametuasa tutulie tusizomee wala kupiga kelele wasije pata nafasi maccm ya kule ffu na kuvuruga utaratibu wetu wakusikiliza shauri hili,


Makene
Mahakama ipo mapumzikoni kumpa nafasi Jaji kuandika mwenendo wa shauri ulivyofikiwa jana na itarejea saa nne na nusu kuendelea na shauri.


UPDATES

Tayari jaji ameshaingia watu wanaambiwa wasubiri kidogo wataruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha kesi,


UPDATES,

Nimepewa taarifa rasmi kutoka kwa Mh Tundu Lisu kuwa kesi ya msingi itasikilizwa saa sita mchana,

Tuweni wavumilivu, matumaini ya ushindi nimakubwa sana,

Watu ni wengi sana, inatia moyo sana!

UPDATES


Tumeingia mahakamani na sasa tunasubiri uamuzi wa Jaji Utamwa


Pipoooooooozi

UPDATES,

Mawakili sasa wanaingia katika chumba cha kesi,

Mh Lisu anatoa kichekesho, baada ya kuingia tu akawauliza makutano, "mbona hamsimami kwa heshima?" watu wote tukasimama akiwemo Zitto, baada ya hapo Lisu akaanza kucheka basi ukumbi mzima ukalipukawa vicheko

kwiii kwii kwii


UPDATES,

Naaaaam

Maaajabu
Karani anashindwa kusoma jalada anazomewa, amejichanganya kusoma akasema ni kesi kati ya Chadema na ccm,

(kimsingi hajajichanganya kwakuwa ndio tafsiri ya kesi hii)

Tunaamriwa tuzime simu, ukibainika kukaidi amri hii ni miezi sita jela,


Jaji ameshaingia, sasa ni utambulisho wa Mawakili,

Kaanza Msando, kwa lugha ya kiingereza,

Lisu katumia lugha ya kiswahili,


Vuteni subira simu chiniiiiii,

UPDATES

Jaji ameanza kusoma uamzi na kuandika,



UPDATES,

Jaji:

-Zitto ameweka pingamizi kufukuzwa uongozi kinyume na katiba.Amemshtaki katibu Mkuu kwa kumtumia barua ya wito kuhudhuria kikao ambacho ni kinyume na katiba kwa kuwa ana rufaa ngazi ya juu

Jaji:

Kibatala alitaka pingamizi litupwe kwa kuwa halina misingi ya kisheria kwa kuwa taratibu zilifuatwa kwa hiyo akataka pingamizi litupwe

Jaji:

Lissu aliwasilisha hoja kuwa matumizi mabaya ya kutumia vifungu vibaya vya sheria vinakiuka katiba ya nchi ibara ya 107(2)


Jaji:

Bw:Msando hakupinga hakupinga hoja ya matumizi ya vifungu visivyo sahihi

Jaji

Jaji anatoa mfano wa kesi ya JUWATA vs Kiwanda cha uchapishaji ya mwaka 1998

Ambayo mahakama iliona tatizo la matumizi mabovu ya vifungu vya sheria kama athari ya maamuzi


Jaji:

Circar Code book page 227 ya Mahakama kuu ya India ,toleo la 11 mwaka 1980 iliamua kuwa pingamizi linapowekwa ni lazima kanuni zinazoongoza taasisi zisomwe pamoja na sheria zake

Ordera 37 inasema mahakama inatoa injuction kwa ajili ya kuzuia mali zisitumike,zisiharibiwe au kupanguliwa


Lissu alijenga hoja kuwa suala hili halihusiani na properties hata kama ni common knowledge ya reference ya circula book

Pia anasema applicant hakuvunjiwa natural justice

Pia mahakama lazima izingatie kuwa taasisi za kidini,kisiasa au mpira haziamuliwi kwenye civil courts

Ametoa mfano wa Aman Vs Lutheran Church ambayo mahakama iliamua


Paragraph 18 inasema kikao cha kamati kuu ni kuwa kitazuia baraza kuu kujadili rufaa yake.Lissu alijibu kuwa baraza kuu huitishwa kwa mujibu wa katiba na na CC ni surbodinate body



Mabishano ya hoja yanaendelea kati yamawakili wa Chadema vs Msando,


Lissu anaomba kwa interest ya public sasa kiswahili kitumike


Msando amepanic sana, Lissu aliomba kiswahili kitumike kwa public interest.Msando alipoulizwa akaanza kuongea.Jaji akamuuliza nimekuruhusu?Watu wakashangilia


Msando kapoteza umakini kutokana na jaji kuamua kutumia kiswahili na yeye kinamsumbua, watu wameshangilia


Msando

Mabishano.Msando anafanya reference ya kesi ya General Tyre VS HSBC bank kuhusu chanzo cha taarifa maana hakuna mumbukumbu

Pia Paragraph 21.Applicant(Zitto) amesema kuwa amenyimwa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa 22 November 2013 mbele ya baraza kuu.Hoja ya Msando aliyotoa


Itetezi wa Msando,

Pia anaomba mahakama iepushe irrepareble injury unaoweza kutokea.Kuwa applicant ni mbunge kwa msingi wa kuwa mwanachama wa chama cha siasa kama katiba ya Tanzania onavyotaka

Na pia ni mwenyekiti wa PAC hivyo anahofia kama kamati kuu itakaa na kutoa uamuzi utakaopelekea kupoteza uanachama wake matokeo ya uamuzi yatamuumiza beyond recovery na pia wananchi waliomchagua itaumiza waliomchagua

Watu wanafyonza na mnong'ono juu

Pia anadai Katiba ya Chadema kanuni ya 6.5.10 inasema"Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinatakiwa kutoa taarifa kwa ngazi ya juu baada ya siku 14'

Kwa hiyo kusema kuwa taarifa hiyo itakamilika baada ya kupitiwa na kikao. cc cha leo inakiuka katiba

Mosando amemaliza kutoa utetezi wake,


Sasa Mh Lisu amesimama na kuanza kuhibu mapigo,


Lissu anasema reference anayofanya ya barua ya kikao cha kamati kuu haikua kwenye record ya documents zikizowasikishwa

Msando anasima na kusema issue ya barua imekuja kwa kuwa counter affidavit imefika saa tano asubuhi.Kwa hiyo ameiondoa sasa amekubali hiyo reference

Msando anaomba mahakama ipokee ombi la mteja wake kwakuwa ni ya msingi,


.......

Lisu:


Lissu sasa. anasema. katiba ya Chadema ibara ya 7:7:14(t) inasema wajumbe wa CC ni pamoja na wakurugenzi wasiokua na kura.Pia Msando ambaye ni diwani wa CHADEMA kata ya mabogini Moshi anatakiwa afahamu Wakili Kibatala ni mkurugenzi wa katiba na sheria ambaye ni mjumbe wa kamati kuu.Kwa hiyo hoja ya kuwa preliminary point of law kuwa hakuwepo kwenye kikao ni suala la ushahidi na tayari mh.Jaji tayari umeamua hapa kabla kuwa ushahidi si hoja za kesi za pingamizi .Kwa hiyo Peter Kibatala kama alikuwepo kama mkurugenzi au la ni suala la ushahidi


Lisu:


Lissu"Mhe.Jaji nakubaliana na kanuni za msingi za utoaji wa zuio kwamba lazima kuwe na primafacie grounds whether the balance of convinience is in favour of reality.Kwamba muombaji anaweza kupata madhara yasiyotibika.Kwa hiyo mere proof of those conditions will not automatically lead to automatically injuction(Amri ya zuio inayoombwa).

Sheria ni lazima ilinde interests of majority against the interest and comfort of an individual for the sake of balance of convinience


Hoja ya apllicant kama ni kuhofia kutotendewa haki angeleta file mahakama kuu ya kuomba baraza kuu liitishwe na si kuzuia kikao cha kamati kuu


UPDATES,

Mh Lisu anaendelea kupangua hoja,


Wakuu simu inakaribia kukata chaji,

Tuvumiliane mkiona kimya,


UPDATES

Kwasasa ni mapumziko

Tutarejea baada ya dakika 20


UPDATES

Wakuu ngumi zinataka kupigwa kati ya msando na mashabiki wa chadema,

Haahaaa ngoja nikaamue ugomvi kwanza


Naaam mzozo umeisha, msando tumemuomba arudi ndani ya chumba cha mahakama kuepusha shari,


Watu wanauchungu na chadema sijawahi kuona,

Jamaa anaongea mpaka analia, hahaaa



UPDATES


Mahakama imerejea,

Sasa Msando anaomba doc moja wapo ambayo Lisu aliiwasilisha mahakamani kama sehemu ya kielelezo ikataliwe,

Nyaraka hiyo inasema "Ripoti ya Zitto Zuber Kabwe kuhusu kuvuliwa uongozi ndani ya chama changu"

Msando anasema nyaraka hiyo itaharibu mwenendo mzima wa shauri, anasema kwanza haina uhakika kama nyaraka hiyo ni ya Zitto kweli kwakuwa haina saini yake,

Zingatia nyaraka inayotajwa ni ile taarifa ya Zitto aliyoitoa pale Serena Hotel


Lisu

Nyaraka tajwa ni halali na ipo kwenye kiapo tulichokiwakilisha leo asubuhi,

Vilevile wakili msomi Msando anayo mkononi hapo,

Kitendo cha nyaraka hii kukosekana mezani kwako mh jaji hilo haliwezi kuwa nyaraka hii ni batili,

Hata stakabadhi ya malipo ya kiapo hiki hii hapa, "anampa Msando"

Kwahiyo nyaraka hii ni halali, Labda wakili msomi Msando atusaidie ubatili wake uko wapi?


Msando kimyaaaaa! Jaji anamuomba ajibu,


Viambatanisho vilikataliwa na Wakili msando kwa kuwa havijalipiwa na kupewa mhuri halali wa mahakama

Lissu amepinga na kuchukua risiti za vielelezo vya Msando.Akasema hata hizi risiti hazina vielelezo vyenye malipo halali kwa kuwa pia sio bei halali ya rekodi za mahakama.Baada ya hapo Akamrudishia risiti kwa kumrushia kwa dharau


JAJI:

Mahakama inatoa amri ya kumruhusu Mh Tundu Lisu kutumia nyaraka hizi kama sehemu ya rejea za kesi hii, hivyo imetupilia mbali ombi la Wakili msomi Msando.


Lisu anaendelea kuisoma taarifa ya Zitto ya Serena Hotel,

Anasoma tamko la Zitto alilodai kuwa atafuata taratibu za chama.Na pia alitangaza nia ya kukataa rufaa.Kwa hiyo alisema mwenyewe kuwa atafuata taratibu zote za chama na kwa hiyo alitangaza nia ya kukata rufaa.Sasa hizo taratibu za chama zimefikaje mahakamani?

Pia taarifa aliyoomba ya kamati kuu ili akate rufaa inahitaji kuhakikiwa na chombo kile kile cha kamati kuu.Ziwe certified na sio mara ya kwanza kuchelewa kuhakiki taarifa.Kwa hiyo kwa CHADEMA hakuna jambo la ajabu.

Na kama kuna ushahidi kuwa CHADEMA imekataa hapo kuna hoja.Kwa hiyo taarifa inaandaliwa na hakuna haja ya ugomvi(premafacie case)


Lisu

Lissu:Hoja kuwa kikao cha kamati kuu kinaweza kutoa maamuzi yenye irrepareble injury haina msingi maana ushahidi uko wapi kuwa kamati kuu ikikaa itamfukuza uanachama?


Lisu

Lissu:Maslahi anayoyazungumzia wakili Msando kuwa wapiga kura wa mteja wake watapata madhara,uenyekiti wake wa PAC na ubunge wake hayalingani na athari ya shughuli za chama kikuu cha upinzani na wanachama wake nchi nzima.Equivoically and categorically where is the balance of convinience?

Anaiuliza mahakama je Ikitokea Kamati Kuu ikitoa onyo kwake je kutakua na madhara yasiyotobika?Yaani irreparable injury?

Je,Akifukuzwa uanachama si siku 90 tu uchaguzi utakua umeitishwa na wapiga kura wa Kigoma watakua na mbunge?Irreparable loss iko wapi?Atakachokosa ni maslahi yake binafsi ya posho tu.Kwa hiyo hakuna hoja .Irreparable loss ni kuangalia maslahi ya wengi kuliko posho zake za Ubunge na uenyekiti wa PAC Tu

Anaendelea..

Lissu ametaka mahakama itupilie mbali pingamizi hili halina msingi

Lisu amemaliza sasa ni Msando tena,

Msando,

Hoja ya Chadema iliyosababisha mteja wangu kuja mahakamani ni mbili tu, kwenye barua ya 26/11/2013 inayosema, "kamati kuu imeadhimia kuchukua hatua zaidi kwa kukuvua uanachama au kukufukuza"


Mawakili wote wamemaliza kutoa hoja zao,


Jajiji anaahirisha kesi mpaka jumatatu siku yakusikiliza UAMUZI rasmi,


Asanteni sana kwakunivumia, wale mliokereka mtanisamehe, nilikwenda Mahakamani kwaajili ya Chama changu dhidi ya Msaliti Zitto na si vinginevyo.

Kibatala amesimama na kuiomba mahaka pia imzuie Zitto na mtu yeyote kujadili suala lake mpaka hapo jumatatu,


Msando nae kasimama anasema hoja hiyo haina msingi kwakuwa mahakama haina uwezo wakuzuia watz 45ml kutozungumzia suala hili,


Kibatala tena amesimama, anasema mahaka inao uwezo wakumzui Zitto na mtu yeyote kutofanya siasa (za Zitto)

Sasa jaji,

Ametoa amri kwa mawakili wa chadema kama watabaini kuna mtu analizungumzia jambo hili lililopo mahakamani basi wachukue sheria,


NJE YA MAHAKAMA

maandamano ya mabango ya kufa mtu, nyimbo kibaraka waccm kibaraka wa ccm

Ooooooya ngumi zinapigwaaaaaaaaaaaaaa haaahaaa hii balaaaa

Kuna vijana kama ishirini hivi wanaleta vurugu kweli wanaimba mtatutambua kuwa sisi ni vijana wa Mwandiga,

Polisi wameingilia kati na kuwachapa makofi sasa wamekimbia kuelekea Hyatt hotel,

walianza kupigana wao kwa wao, hali imetulia sasa ni nyimbo za pipozi pawaaaa, kibaraka wa ccm x2
 
Namkumbuka Ludovick Joseph alivyopewa kazi maalumu na Dr Slaa kule Zanzibar lakini yalipomkuta Dr Slaa alisema hamjui na wala hajawahi kumuona. Endelea kutumika Yericko siku yako inakujaa. Ushauri in politics kuwa neutral ili uchukue kura za wooote na hasa kambi hasimu, Kataa kutumika kama kondomu
 
Ukianza kutoa taarifa utulie na uwe makini.....habari ya kuandika na kukosea( spelling errors) kama unakimbizwa au kuwa na papara kama kuku anayetetea hatuitaki.......by the way hivi una cheo gani hapo CDM maana umedamka kweli
 
Twakuaminia kamanda wasaliti kipindi hichi lazima waonyeshe mzigo ulipo.

Utetezi wao wamekanusha tuhuma zote bila kujua watu makini cc watakapowabana na ushahidi wataonyesha mzigo ulipo
 
Namkumbuka Ludovick Joseph alivyopewa kazi maalumu na Dr Slaa kule Zanzibar lakini yalipomkuta Dr Slaa alisema hamjui na wala hajawahi kumuona. Endelea kutumika Yericko siku yako inakujaa. Ushauri in politics kuwa neutral ili uchukue kura za wooote na hasa kambi hasimu, Kataa kutumika kama kondomu

Una matatizo wewe..any rational person lazima awe na side yake..whether bad or good.

Desmond Tutu once said " A neutral person in the situations of injustice is always on the side of the opressor".

Ndugu yangu..kuwa neutral siyo ujanja bali ni sign kubwa ya kutojielewa.
 
Usitetemeke Kama jana saa moja usiku!!Nani yupo Katika Kikao chenu cha Kichen Party(Majungu),
#Ex CDM simper aliquid novi#
 
Ukianza kutoa taarifa utulie na uwe makini.....habari ya kuandika na kukosea( spelling errors) kama unakimbizwa au kuwa na papara kama kuku anayetetea hatuitaki.......by the way hivi una cheo gani hapo CDM maana umedamka kweli

anzisha thead ya kutaka kujua cheo cha yericho, thread hii inahusu kesi ya pingamizi la zito.
 
Wakuu kumepambazuka vema,

Viunga vya mahakama kuu vimetulia, watu wakiendelea kuwasili tayari kwa usikilizwaji wa pingamizi la Zitto Kabwe kutaka kamati kuu ya chadema isijadili utetezi wake,

Tumejiandaa vema kuwaletea kinachojiri na kuzuia upotoshaji mkubwa uliofanywa jana na kundi la wasaliti hawa wa mageuzi,

NB

Kamati kuu ya chadema inaanza kikao chake kama kawaida hivi punde na Zitto ataanza kutajwa ndani ya vikao hivyo baada ya saa tatu kamili asubuhi hii,

Pipoooooz!!!!!!!

Kumbe kimbele-mbele chote hata kamati kuu haumo?
 
YALIYOJIRI MAHAKAMANI LEO


Leo Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe, mbunge wa Chadema, Kigoma Kaskazini. Kamati Kuu ya Chadema inatarajia kuanza kikao chake kesho na moja kati ya agenda zake ni kupokea utetezi wa Zitto Kabwe kuhusu uanachama wake dhidi ya tuhuma 11 zilizotolewa hapo awali. Hata hivyo ikumbukwe kuwa baada ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa Zitto Kabwe, aliandika barua ya notisi ya kukata rufaa kupinga maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba, kanuni na taratibu za chama.


Katika barua hiyo aliomba mwenendo wa mashtaka ili kukamilisha rufaa rasmi. Mpaka sasa hajajibiwa badala yake Zitto Kabwe ameitwa na chombo kilekile, kwa kosa lilelile, kwa adhabu kubwa zaidi. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya haki asili (natural justice).


Hivyo amekwenda mahakamani kuomba mahakama izuie Kamati Kuu isijadili au kuamua chochote juu ya uanachama wake mpaka atakapopata fursa ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.


Baada ya majibizano ya kisheria ya masaa 4 yaliyotokana na pingamizi 3 zilizowekwa na jopo la mawakili wa Chadema, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za wakili msomi Albert Msando na kutupilia mbali pingamizi hizo.


Mahakama imetoa amri ya kuzuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe. Pia mahakama imeagiza Chadema ipeleke majibu yao dhidi ya haki ya kiapo ya Zitto hapo kesho tarehe 03/01/2014.


Ieleweke kuwa kesi iliyopo mahakamani ya 01/2014 ni ya Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na Kitila Mkumbo au Samson Mwigamba.


Kesi ya msingi imepangiwa kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom