Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,932
Habari watanzania.
Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezimungu,kwa kunisimamia na kunilinda mara zote,natoa shukrani zangu za dhati kwa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) chini ya mkurugenzi wake Onesmo Olengurumwa Kwa kusimamia uendeshaji wa kesi yangu kuanzia mwanzo hadi mwisho, bila kusahau kituo cha haki za binadamu Tanzani (LHRC),pia shukrani zangu za dhati kwa Mawakili wangu Jebra Kambole(based in Dar) na Chance luogo(based in Iringa).kwa uwezo wao wa utetezi imara katika kesi yangu,na kusimama kwangu pia kama washauri na wafariji kwangu Mungu awabariki sana.
Pia napenda kutoa Shukrani za dhati kwa viongozi na wanachama wenzangu wa TSNP ,pia ndugu zangu,jamaa , marafiki na watanzania wote kwa maombi yao,faraja na matumaini kwangu,Mungu awabariki sana.
Mwisho,napenda kupongeza Mahakama ya hakimu Mkazi Iringa kwa kutenda haki kwa kufuata sheria na taratibu zote katika utoaji haki,bila kusahau nawashukuru pia wanasheria wa Serikali (State attorneys) kwa kuleta mashahidi wao kwa wakati kufanya kesi yangu kuwahi kuisha ndani ya miezi 9.
Nilisimamishwa chuo kutokana na sheria iliyopo ,sasa kesi imeisha namshukuru Mungu,utaratibu rasmi utafanyika mimi kuendelea na masomo hilo ndio jambo kubwa lilopo mbele yangu,kuhakikisha namaliza masomo yangu salama kwa muda uliobaki (one semester)
Sina nia ya yeyote ya kufungua shauri ,au kuomba madai kwa mtu yeyote au taasisi yeyote hili kwangu sio jambo la msingi ,na sina chuki na Mtanzania yeyote, au taasisi yeyote yote yametokea yametokea(Forward Ever Backward Never).Namshukuru mwenyezimungu kwa yote.
Nawaomba watanzania wote ,au taasisi yeyote kwa kipindi nilichokuwa katika changamoto kama niliwahi udhi au kukosea yeyote naomba radhi naomba kusamehewa .mniruhusu kuanza maisha yangu yakawaida kwa upendo na amani.
Hakika nina upendo wa dhati kwa kila Mtanzania ,kwa Taasisi yeyote, kiongozi yeyote ,bila kujali rangi,dini,kabila au chama cha siasa.
Mungu atujalie Afya njema,upendo na amani kwa maslahi ya jamii yetu na Taifa letu kwa ujumla.
Wako.
Abdul Omar Nondo.
abdulnondo10@gmail.com
Mwenyekiti mstaafu wa TSNP.