Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Ripoti ya Awali Kuhusu Matukio Yasiyo ya Kawaida Katika Zoezi la Upigaji Kura kwa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Magogoni, tarehe 23 Mei, 2009
Wapendwa Wanahabari,
Wakati upigaji kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni, lililo kwenye Wilaya ya Magharibi, Unguja, ukiendelea hivi sasa, tunatoa tarifa ya mwanzo inayohusu matukio yasiyo ya kawaida yanayohusiana na uchaguzi huu.
I. KITUO CHA WELEZO SKULI
- Aliyekuwa OCD wa wilaya ya Mjini, Bwana Nurdin, amewapeleka watu ambao si wakaazi halali wa jimbo la Magogoni kwa sheha wa shehia ya Welezo, Bi Mgeni, kwa ajili ya kupatiwa shahada za kupigia kura.
- Sheha, Bi Mgeni, anapeleka watu wasiokuwa na shahada za kupiga kura na anasimamia kuwapigisha kura. Angalau watu watatu (miongoni mwa hao waliopelekwa) wamesharipoti katika ofisi zetu kuthibitisha hili.
- Katika Chumba Na. 4, wapiga kura wanapewa shahada mbili za kupigia kura. Kwa uchache, watu wanne wamesharipoti kwetu kwamba wamepewa shahada mbili mbili.
- Katika Chumba Na. 5, wapiga kura wamegundua kwamba karatasi zao za kupigia kura haziandikiki. Ni baada ya kujaribu mara zaidi ya tatu, ndipo kwa mbali alama waliyoweka imejitokeza
- Saumu Kitwana Mussa mwenye shahada halali Na. 630003322 iliyoandikishwa kupigiwa kwenye kituo cha Welezo Skuli, Chumba Na. 6 amekataliwa kwa madai kwamba jina lake halimo kwenye Orodha ya Wapiga Kura
II. KITUO CHA KINUNI
- Kundi la Janjaweed likiongozwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) limezunguka maeneo ya kituo kwa ajili ya kushinikiza kupiga kura
III. KITUO CHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO
- Gari Namba ZNZ 45948 inatumika kupakia vijana kutoka ofisi ya CCM Mkoa na ambao si wakaazi wa jimbo la Magogoni, iliyopo Amani, kupeleka kituo cha Viwanda Vidogo Vidogo kwa ajili ya kupiga kura
IV. KITUO CHA WELEZO HOSPITALI
- Kijana mwenye kipande kilichoandikwa jina la Omar Hashim Mohammed, chenye namba ya usajili 620 001 358, amekutwa na shahada ya kupiga kura ambayo ni feki. Wenzake wenye shahada kama hiyo wameweza kupiga kura katika kituo hicho cha Welezo Hospitali.
Wapendwa Wanahabari,
Hii ni taarifa ya awali juu ya matukio yanayoendelea sasa na ambayo hadi sasa yameripotiwa kwenye ofisi yetu kwa ushahidi kamili. Tutawatumia taarifa nyengine kadiri zitakavyokuwa zinatufikia.
Pamoja na salamu za Chama,
Dawati la Habari na Mahusiano,
Civic United Front
(CUF Chama cha Wananchi)