Kufuatia ruzuku ya mgao wa vyeo vya ma-DC , vilivyotolewa hivi majuzi na Baba mwenye kaya .
Aliyekua RPC mkoani Dodoma na baadae Mwanza na kisha kustaafu akiwa Kamishna makao makuu D'salaam Bw. Zelothe Stephen , ameruzukiwa u-DC Musoma .
Kimtazamo wangu sioni kama inanipa Afya ya akili , Aliyekua Boss wa Mkoa , kwenda kua Boss wa Wilaya ! Siamini kama imekaa njema!
Aidha sielewielewi uteuzi wake umetumia vigezo gani .
Kwa hili , itaniepukaje niamini pasipo mawaa , kwamba Kamanda huyu alikitumikia Chama kilichompa u-DC vizuri na leo kimemruzuku ajira? .
Tanzania tamu sana !