Kutoka Cheo cha kuwa RPC hadi kuwa DC

Kutoka Cheo cha kuwa RPC hadi kuwa DC

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Kufuatia ruzuku ya mgao wa vyeo vya ma-DC , vilivyotolewa hivi majuzi na Baba mwenye kaya .

Aliyekua RPC mkoani Dodoma na baadae Mwanza na kisha kustaafu akiwa Kamishna makao makuu D'salaam Bw. Zelothe Stephen , ameruzukiwa u-DC Musoma .

Kimtazamo wangu sioni kama inanipa Afya ya akili , Aliyekua Boss wa Mkoa , kwenda kua Boss wa Wilaya ! Siamini kama imekaa njema!
Aidha sielewielewi uteuzi wake umetumia vigezo gani .

Kwa hili , itaniepukaje niamini pasipo mawaa , kwamba Kamanda huyu alikitumikia Chama kilichompa u-DC vizuri na leo kimemruzuku ajira? .
Tanzania tamu sana !
 
Kamanda amezawadiwa ajira, chezea stress za ustaafu. Pia Mkulu anatuma ujumbe kwa makamanda kuwa watakumbukwa Tu kwa hiyo wafuate amri za wakubwa na sio sheria
 
Ndio usije kushangaa Said Mwema akiwa Mkuu Wa mkoa
 
Katika teuzi zoote madudu zilizowahi kufanyika hii ndio BABA LAO

Nadhani ni uteuzi wa Nape siamini kama mzee anajua
 
Ndio maana wakuu wengi wa polisi huwa wanaleta ukakasi baada ya kustaafu wawekwe wapi.
 
Kamanda amezawadiwa ajira, chezea stress za ustaafu. Pia Mkulu anatuma ujumbe kwa makamanda kuwa watakumbukwa Tu kwa hiyo wafuate amri za wakubwa na sio sheria

Yaani kawaambia wawasifu viongizi hata wakiwa uchi! Ili waneemeke siku zote!
 
Charles Mlingwa aliwahi kuwa Naibu waziri- Sasa ni mkuu wa wilaya.

somebody Mwananzila aliwahi kuwa Naibu Waziri- Sasa ni mkuu wa Mkoa.

Joel Bendera aliwahi kuwa Naibu Waziri-Sasa ni mkuu wa mkoa.

Huenda kuna wengine wengi tu ambao walikuwa na vyeo vya kitaifa au kimkoa na sasa wapo kimkoa au kiwilaya.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Kufuatia ruzuku ya mgao wa vyeo vya ma-DC , vilivyotolewa hivi majuzi na Baba mwenye kaya .

Aliyekua RPC mkoani Dodoma na baadae Mwanza na kisha kustaafu akiwa Kamishna makao makuu D'salaam Bw. Zelothe Stephen , ameruzukiwa u-DC Musoma .

Kimtazamo wangu sioni kama inanipa Afya ya akili , Aliyekua Boss wa Mkoa , kwenda kua Boss wa Wilaya ! Siamini kama imekaa njema!
Aidha sielewielewi uteuzi wake umetumia vigezo gani .

Kwa hili , itaniepukaje niamini pasipo mawaa , kwamba Kamanda huyu alikitumikia Chama kilichompa u-DC vizuri na leo kimemruzuku ajira? .
Tanzania tamu sana !

Najua kila mutu ana mtazamo wake jinsi aonavyo, hata mteuliwa na mteuwa nao pia wana mtazamo wao katka najinsi wanavolichukulia. Maswali ya kujiuliza: 1. Ungekuwa wewe umeteuliwa ungefanyaje? 2. Kama wewe ungekuwa unateua ungefanyaje? 3.Ni nani anastahili kwa nafasi hyo? 4. Kuna ukiukwaji wa katiba ama kanuni za utumish vimekiukwa?
 
Kufuatia ruzuku ya mgao wa vyeo vya ma-DC , vilivyotolewa hivi majuzi na Baba mwenye kaya .

Aliyekua RPC mkoani Dodoma na baadae Mwanza na kisha kustaafu akiwa Kamishna makao makuu D'salaam Bw. Zelothe Stephen , ameruzukiwa u-DC Musoma .

Kimtazamo wangu sioni kama inanipa Afya ya akili , Aliyekua Boss wa Mkoa , kwenda kua Boss wa Wilaya ! Siamini kama imekaa njema!
Aidha sielewielewi uteuzi wake umetumia vigezo gani .

Kwa hili , itaniepukaje niamini pasipo mawaa , kwamba Kamanda huyu alikitumikia Chama kilichompa u-DC vizuri na leo kimemruzuku ajira? .
Tanzania tamu sana !

hii ndio Tanzania,Najua wajua nami ntazidi kukujuza.
 
Huyo amekwenda kwa kazi maalum mkuu na hasa ikizingatiwa kwamba miongoni mwa watumishi ambao wamefanya kazi zao kwa uadilifu bila kashfa za kijinga kijinga ni Zelothe Steven kumbuka hata baada ya kustaaafu bado aliendelea kuitumikia jeshi katika chunguzi mbalimbali.

Kwa hiyo hata huo uteuzi wake ni wa kazi maalum na hasa ukizingatia mahali alipopelekwa.
 
Jenerari Ulimwengu aliwahi kusema kuwa uDC hauna qualification inayoeleweka. Mi mapenzi tu ya anayeteua. Si ajabu kukuta DC aliyeishia darasa la saba au kidato cha nne(uliza elimu ya Rugimbana) na wingine ana Phd. Unaweza kumpata DC kopro na mwingine Major General(kuna kipindi Major General Ndomba alikuwa DC Ngara kabla ya kurejea jeshini). Ni cheo cha ajabu sana.
 
Kama mtu hujapata uongozi kwe kipondi hiki cha uongozi wa J.K wa pili katu hutapata uongozi maisha yako yote,huwa natamani ningekuwa mbunge kwe uongo-inzi huu labda ningelikuwa nishanusa cv ya uwaziri kwani ulikuwa unagawiwa kama jungu vile.Big up JK umeweka record ngumu kuvunjwa
 
Huyu sasa amekuwa mtawala kumbuka polisi si mtawala bali ni mfanyakazi wa umma kama wafanyakazi wengine na wanapokea Amri kutoka kwa watawala. Mleta mada nina shaka na kiwango chako cha elimu hadi unamuhita RPC ni boss wa mkoa, wakati hii ni civics ya darasa la nne kabisa.
 
Udc ni cheo cha ajabu,haiangalii una elimu kiasi gani,kuna bw akiitwa Gerald Guninita,hata sijui walimteua kwa sifa gani,elimu hakuna kabisa
 
Yaani mleta mada umewapaisha polisi hadi kuwa mabosi wa wananchi? Au kwa kuwa wanatandika viboko wananchi?Kwa hiyo hata afisa elimu mkoa na yeye ni bosi wa mkoa?Mkuu wa wilaya au mkoa wale ni viongozi wanawaongoza wananchi wote katika eneo wanaloongoza, ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ambazo zinaundwa na majeshi ya ulinzi na usalama kwa hiyo hayo majeshi yanapokea amri kutoka kwa wakuu wa mikoa au wilaya, vilevile wakuu wa mikoa na wilaya wanamwakilisha raisi kwenye maeneo yao.
 
Mi naona ni sawa kabisa, maafisa wengi wanaoteuliwa vyeo hivyo ni kutoka Jeshi kuu, ni jambo jema kulikumbuka Jeshi letu hili dogo.
 
Back
Top Bottom