Kutoka Bungeni, live

Ameanza kwa kutokuunga hoaja mkono,kwa sababu
1}ukubwa wa baraza la mawazi kiasi cha mawaziri 54,
2}Uonevu wa wanafunzi
3}Serikali kukataa kuhamia Dodoma
 
Anataka rais na ikulu nzima ihamie Dodoma pamoja na mawaziri na wizara yote
 
Aongelea migomo kuwa ni kitu cha kihistoria kilichoanza miaaka ya 196....,enzi vyama vya upinzani havikuwepo,na vitaendelea kuwepo endapo maslahi ya wanafunzi hayataboreshwa,
 
Asisitiza maandamano yataendelea Serikali na CCM wamekatwa pabaya,amsisitizia Mbowe Dr kuendeleza maandamano mpaka kieleweke,maana serikali sasa imeshikwa pabaya ndo maana wanapinga
 
Mbona hotuba ya Pinda tupu sana. Bado wanaendelea kuijadili! Wanahalalisha posho tu hao.
Bado sijaelewa,inaonekana kama wanataka kujihalalishia posho maana wameongeza siku mbili juu ya kujadili hotuba ya waziri mkuu coz wachangiaji ni wengi
 
Naaaaaaaaaaaam,bunge limesitishwa mpaka saa 11 jini,thus tutakutana baadaye
 
vichwa vya CDM utavijua tu, yaani wakisimama kuongea km unataka kutoka hutatoka hadi wamalize, akisimama wa magamba kuongea lazima km upo sehemu hutasubiri aongee, utaondoka bila hata kuaga.
Ni kweli kabisa.
 
Bunge limeisha mi nimependa Suzan Lyimo alivyochangia kawachana serikali na kawataka Mh Mbowe na Slaa waendlee kuichachafya serikali kwa maandamo yao kwa kudai CDM imewashika pabaya serikali.

Kadai Migomo ilikuwapo tangu miaka ya 60 hapakuwapo na Chadema, Cuf wala TLP sasa hizi kejeli kwamba vyama pinzani vinachochea maandano imetoka wapi??
 
Juzijuzi niliandika sredi moja kuhusu Dodoma ambayo Suzan Lyimo kaiongea sana leo bungeni kuhus ugumu wa serikali kuhamia dodoma...yeye kadai Rais kwanza ndio ahamie dodoma na wengine wafuatie, na katoa kashfa kwamba ikulu ya Dodoma imegharimu mabilioni ya sh kila mwaka kugharamia service..hii haijakaa fresh


Sredi yenyewe hii hapa:

Jamani dodoma kuna nini??katikati ya nchi, kama tulivyofundishwa tangu tupo skuli kwamba ndiyo makao makuu ya nji hii njema. Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa hii ndiyo makao makuu ya nchi na wizara kibao zitajengwa huko badala ya Daslam. Ndiyo tangu kitambo hicho mpaka sasa nchi yetu imegubikwa na matatizo lukuki na tunajitadi kupambana nayo na kwa mafaniko yanayoenda kama kobe, lakini ni nani aliyetuaminisha kwamba wizara nyingi zitahamishiwa huko?mchawi ni nani hapa??

Tunaaminishwa kila siku kwamba taifa hili ni changa na maskini, kumbe kuna watu wamejilimbikizia mimali/mipesa mingi ya kuweza kuilisha nchi ya burundi kwa zaidi ya miaka 8, can u imagine this?? sasa hii ya dodoma ni kweli au changa la macho?? Wabunge sasa hivi wapo mjengoni, hakuna hata anayethubutu kuuliza kuhusu dodoma, why??

Ngoja ni-hit point!! Hivi inaingia akilini mawaziri, wabunge na viongozi wengine kuhamisha familia zao toka daslam kwenda kuishi dodoma?? Agenda ya kuhamisha wizara kwenda dodoma ipo miaka na miaka lakini hakuna kinachofanyika..ni siasa tu!! Ardhi ipo, climate nzuri, infrastructure bora, lakini kwanini hii kitu ni sumu hata kwa viongozi wetu kuona kwamba dodoma inakuwa replacement daslam??nani anajua siri ya hii kitu kugonga mwamba??naamini kuna wabunge/mawaziri wengine tangu wapo kindegaten walisoma hii kitu, lakini wapi, siasa bana!! Sijui kwanini kuhamia dodoma kwa viongozi wetu imekuwa 'inshu ngumu' hivyo! Miaka nenda rudi sasa imekuwa kama alfu-lela-ulela, ni mambo ya kufikirika tu!!

Hivi inawezekana ugumu wa kuhamisha makao kwenda dodoma ni kwasababu ya starehe za daslam??inawezekana!! maraha yote ya daslamu nani aende dodoma??ndio kusema ile lunch ya Movenpick, New Africa Hotel, Kempisky na kwingineko ndiyo kusema is over??aagh hapana bana hatuwezi kuhamisha makao dodoma asilani!! Can u imagine, mbunge siku zote utamwona bungeni lakini malazi yake yapo daslam daily!! Kunani dodoma jamani??Twende kule ndio kusema ni mwisho wa kupigwa na kipupwe cha bahari nzuri ya Hindi hapa daslam?? Nikapigwe vumbi jekundu dodoma??Nikipata mafua nikatibiwe dodoma hospital??niende huko niwafate akina Matonya?? Big No.

Hivi vitu vyote,ugumu wote hapa daslam, msongamano, ajali nyigi, joto kupanda kwa sana, mvua haba, polution, population na mengineyo ni matokeo/zao ya serikali yetu kukaa zaidi kisiasa badala ya kihalisia/kifikra/kiutendaji!! Huko mikoani hakuna kinachofanyika. Hii ni nchi gani bana??Hivi kuna ugumu gani kwa mfano balozi za Malawi, Mozambique, South Afrika,Shelisheli n.k zisiwe Mtwara na Lindi?? Balozi za Kenya, Ethipoia, Rwanda nk zisiwe Mwanza??Balozi za Congo , Zambia nk zisiwe Mbeya n.k? Kwanini??

Hembu angalia barua za mkopo kwa wanafunzi lazima uje daslam, ukitaka visa lazima uje daslam, malipo ya wazee EAU daslam, kusafiri nje ya nchi lazima uje daslam,bidhaa flani-daslam, saloon za nywele-daslam,maombi ya chuo-daslam, maombi ya kazi daslam...jamani dodoma patakalika kweli?? Jamani Daslam sasahivi ndio Tanzania..hahaaaa!!nani anapenda kukaa bush bana??? Sasa ukiwauliza wanasiasa/viongozi hembu angalia majibu yao mepesi...''tunasubiria zijengwe ofisi kwanza''..hivi tatizo ni ardhi au fedha??cha kushangaza hata hapa Daslam kuna wizara na ofisi nyingi tu ni za kupanga.
Serikali haijajenga ofisi zote hapa daslam. Viongozi wanamiss kweli raha za jiji.

Ushauri wangu ni kwamba ujenzi wa kumbi za starehe uanze mara moja kabla hawajafikiria kuanzisha ujenzi wa wizara mbalimbali-zijengwe kumbi nyingi za starehe., club nyingi za usiku, migahawa ya 3, 4 na 5 star, madanguro na vinginevyo vingi, baada ya hapo nadhani wabunge wote watakuwa radhi kuhamia dodoma!! na kama hili halitekelezi basi hii kauli kwamba wizara zitahamishiwa dodoma ifutwe mara moja!!

Tuchangie hoja...Jioni njema!!
 
Bunge limeisha mi nimependa Suzan Lyimo alivyochangia kawachana serikali na kawataka Mh Mbowe na Slaa waendlee kuichachafya serikali kwa maandamo yao kwa kudai CDM imewashika pabaya serikali.

Kadai Migomo ilikuwapo tangu miaka ya 60 hapakuwapo na Chadema, Cuf wala TLP sasa hizi kejeli kwamba vyama pinzani vinachochea maandano imetoka wapi??
That is true mkuu,mi mwenyewe nimependa sana huyu mama alivyotoa mchango wake na kuivua serikali nguo
 
Back
Top Bottom