Kutoka Bungeni: Fao la kujitoa halipo badala yake limeletwa fao la kutokua na ajira

Nashengena

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,016
3,694
Kutoka bungeni Dodoma

Mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari. Fao la kujitoa halipo kwenye mapendekezo hayo, badala yake limeletwa fao la kutokua na ajira

Inapendekezwa kuwa, mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18 atalipwa 30% ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Na atalipwa kwa miezi 6 mfululuzo, baaada ya hapo malipo hayo yatasitishwa.

Mfanyakazi anayestahili malipo haya, ni yule tu ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation)

Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha michango yake kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme), kwenda mfuko wa hiari (supplementary scheme). Hapo atakuwa na hiari kuchukua pesa yake kulingana na mfuko wa hiari aliojiunga nao na pia atakuwa na haki ya kuendelea kuchangia.

Mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa amechangia chini ya miezi 18, atakuwa na haki ya kuchukua 50% ya michango yake mara baada ya ajira kukoma.

Hapa ndio wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi tunatakiwa tuunganishe nguvu kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao hawana ajira za kudumu.

Updates

Vyama vya wafanyakazi na mashirika yanayotetea haki za binadamu wametoa tamko. Soma hapa
 
Attachments

  • Tamko kuhusu FAO la kujitoa.pdf
    502.9 KB · Views: 487
Huu ni zaidi ya udikteta,.....serikali ya kutetea wanyonge kamwe haiwezi ruhusu haya......wameloose mapato bandari now naona wameamua kutukamua sisi.

Anyway-hii sheria inaanza lini....maake kama bado ntaacha kazi mwezi huu ili nichukue changu mapema...then ntatafuta ingine baadae.....so bad
 
Kutoka bungeni Dodoma

Mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari. Fao la kujitoa halipo kwenye mapendekezo hayo, badala yake limeletwa fao la kutokua na ajira

Inapendekezwa kuwa, mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18 atalipwa 30% ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Na atalipwa kwa miezi 6 mfululuzo, baaada ya hapo malipo hayo yatasitishwa.

Mfanyakazi anayestahili malipo haya, ni yule tu ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation)

Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa haja pata ajira ataruhusiwa ataruhusiwa kuhamisha michangoyake kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme), kwenda mfuko wa hiari (supplementary scheme). Hapo ataruhusiwa kuchukua 50% ya michango yake.

Hapa ndio wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi tunatakiwa tuunganishe nguvu kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao hawana ajira za kudumu
duuh hii ngoja tuone itavyofanya kazi
 
Hawaoni kama huu ni uonevu hii serikali? Mfano mtu anayeilipwa mshahara wa 180,000 ukimpa 30% ya mshahara wake (54,000) kila mwezi baada ya kupoteza ajira yake na jinsi ughali wa maisha haya ulivyo atafanyia nini hasa? Na baada ya hiyo miezi 6 wakisitisha na mtu asipate kazi mpaka baada ya miaka 3 hapo kati anaishi vipi? Hii nchi inaendeshwa kiuonevu sana. Iweje pesa ya mtu aliyoitumikia ipangiwe matumizi na wengine? Uhalisia wa hii mifuko iko wapi endapo haina manufaa yeyote kwa wachangiaji? Lakini kama yalivyopitishwa mengine kiholela na hili pia litapita.
 
Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa haja pata ajira ataruhusiwa ataruhusiwa kuhamisha michangoyake kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme), kwenda mfuko wa hiari (supplementary scheme). Hapo ataruhusiwa kuchukua 50% ya michango yake.

Huu hapo juu ni ukiritimba :rolleyes:.
Mtu huna kazi, then uanze kuangaika kuamishiwa pesa zako
 
Huu ni zaidi ya udikteta,.....serikali ya kutetea wanyonge kamwe haiwezi ruhusu haya......wameloose mapato bandari now naona wameamua kutukamua sisi.

Anyway-hii sheria inaanza lini....maake kama bado ntaacha kazi mwezi huu ili nichukue changu mapema...then ntatafuta ingine baadae.....so bad
Mswada wa mapendekezo ya mabadilko ndio utasomwa kwa mara ya kwanza kisha kamati husika itapewa majukumu ya kukusanya mapendekezo ila hawajatoa ratiba lini utajadiliwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom