Kwani tangu lini walikuwa kambi ya upinzani?

nani kasema cdm wanatetea maslahi ya umma? hawa ni wahuni waliokuwa vijiweni wamekutana na upepo wa kisiasa wamepata ubunge huenda hata wanapuliza kiji.. hongera cuf mna busara mtu mmoja anaweza kuwafanya nyie wote hamna maana mbele ya macho ya watz.

sishangai kabisa! cuf ni chama cha wapemba na wako kwa ajili ya interest za wa Pemba,kwa hiyo sawa tu alivyo sema maana wao tayari wakopamoja na ccm visiwani wakisimamia interest za nchi yao.tunasubiri siku warudi kwao basi

Kama ilivyo CDM chama cha Wachagga hilo halina ubishi
Haya ndio matatizo ya vyama vya Upinzani nchini... Tatizo kubwa ni Wanasiasa Uchwara kama huyu..
Haya mambo huwezi kuyakuta CCM hata kidogo, ila vyama vya Upinzani tu siku zote sababu ya kutofautiana ni watu na maamuzi yao binafsi..
Jambo moja muhimu sana nawaomba wanasiasa uchwara walifahamu. Kwanza ni heshima kwa viongozi wako hata kama hukubaliani nao kwa maana kwamba ndani ya CCM toka Nyerere huwezi kukuta migogoro ya kiuongozi ndani ya chama. Nyerere alikuwa na sekretariet yake na akabadilisha mara kibao, akaja Mweinyi na yake akaja Mkapa na yake na leo hii JK anayo yake baadaye kubadilisha hivi majuzi tu...
Pamoja na mabadiliko yote haya haijatokea hata siku moja viongozi wake kudharauliwa na wanachama ama viongozi hata kama hawapendwi. Tulikuwa na Rostam kama mweka hazina wa chama na alikuwa na maadui lakini haikutokea mtu kuodnoka chama wala kubishana na uongozi kwa sababu kachaguliwa Rostam..Na hata wakati wa misukosuko ya Rostam hakuna kiongozi wala mwanachama aliyejitoa chama kwa sababu Rostam ni mweka fedha isipokuwa walitafuta njia za kumwondoa kuilaini na wakaweka kundi jingine.. majuzi tu wamebadilisha tena hakuna kinyongo maanake nafasi za chama ktk uongozi ngazi za juu hazifiki 100 na wanachama ni zaidi ya 2mil.. utaweza vipi kuwadhirisha wote!
Lakini tazama vyama vya Upinzani..kila mtu anataka kuwa kiongozi makao makuu ya chama, kila mtu anataka kuwa mwenyekiti, katibu au mweka hazina..Usipofanikiwa kuna mchawi wako na unaunda uadui..Kuna watu wanahama CDM kwa sababu ya Mbowe au Dr.Slaa au Zitto sijui Lema kafanya hivi ama vile. Nenda CUF, NCCR, TLP kote kumejaa wanasiasa ambao kwao chama ni MTU, ukiwa na ugonvi na Mbowe basi chama hicho hakikufai unaondoka kwenda NCCR au CUF, vivyo hivyo toka CUF na NCCR ili mradi maamuzi yako yanatokana na MTU sio SERA wala hoja..
Haya tazama mbunge kama huyu, ni kiongozi wa chama na anathubutu kusema CUF inajiondoa ktk kambi ya Upinzani kwa sababu Tundu Lissu hana nidhamu! kweli hii inaingia akilini kukiweka chama ktk nafasi mbaya ya kutetea maslahi ya wananchi..Ukijiondoa ktk Upinzani unajinyima fursa ya uwakilishi ktk maswala ambayo ni muhimu zaidi kwa wananchi halafu basi kinachochekesha zaidi sii ajabu huyu mbunge anakubaliana na maudhui ya hoja isipokuwa kitendo cha kutolewa Lissu..CUF kuingia kambi ya Upinzani ni kazi iliyofanywa kwa nguvu kubwa sana pamoja na kwamba haikuwa halali. Wamewezeshwa kupata fursa hiyo leo unaitupa kwa sababu ya Lissu? huu si ukichaa jamani?
Wanasiasa wa Bongo kweli ni kichwa cha mwendawazimu..