Kutoka Bungeni: 2006 - 2010



Mbona wanazungumza - si huyo Hamad Rashid na yule mwenzake anaeitwa Khalifa wote ni wa CUF hao au wewe hujawasikia?
 
cuf pengine wamegundua mitego maana wao ndio weshaingizwa mjini sana tu hao ccm, ila hilo la kuondoa hoja ikiwa wamegundua ina mapungufu ni nzuri, wakae wajipange upya.

tuukubali ukweli, wapinzani imara wanahitajika, si wapinzani kiromo romo.

hakuna asiejua kuwa ccm inakula nchi, kuna baadhi ya wanaccm hutanguliza maslahi yao kwanza. na nnaweza kusema hata wapinzani baadhi yao ni hivyo hivyo.

cha msingi mnapopeleka hoja iwe hoja ilioenda shule.

suala la msingi ambalo kwanza la kupigania kuwekwa mazingira sawa( adala) ya kupata information, upinzani idai hilo kuwa na wao wanahaki ya kupata information wanazozihitaji ktk kufanya uchambuzi wao wa kuwakilisha hoja.

na waseme wazi bila ya kuwa information yakinifu ni vigumu upinzani kuisaidia serikali kuleta maendeleo.

na pia mbadilike, kuwepo kwenu bungeni ni kuisukuma serikali kuleta maendeleo na sio pahala pa kujitoa kwa ajili ya chaguzi, nnaona siku hizi vyama vyote huko bungeni hufanya vitu vya kujinadi kwa wananchi kuwa wao wanawajali wao wanawatetea, just kwa kutaget kura. huo nbi upuuzi wekeni maslahi ya taifa kwanza
 
Naomba kuuuliza, wakati ule Basil Pesambili Mramba, aliposema kuna hela za ujenzi wa barabara ya singida wakati alijua si kweli, hadi Lowasa na Sitta wakaingilia kati kuokoa jahazi,
yeye hakusema uongo?
 
Kasama,

Uwongo ni relative quantity, akisema Mramba au Malima tunasema alikosea lakini hakukusudia kudanganya bunge, kwa hiyo "busara za spika" zinatumika kumaliza jambo hilo. Akisema Zitto tunasema amechanganya sheria mbili tofauti kwa hiyo kwa makusudi amedanganya bunge, ni lazima afukuzwa bungeni kwa miezi mitano.
 


CUF inasubiri "kukomboa" Unguja na Pemba kwanza halafu ndio watumikie ya Tanzania....Na hapa ndipo wanapoharibu. Jaribu kufikiria CUF wangemuunga mkono Zitto kama alivyofanya Zitto wakati wa ile hoja ya Ubunge wa Afrika Mashariki...

Katika CUF mtu pekee ambaye anaweza kusimama kama mtanzania ni Kiongozi wa Upinzani, HAMAD RASHID na hilo linamfanya wamshuku kuwa ni msaliti na sio wa kumuamini kwa maslahi ya chama.

Tanzanianjema
 
taratibu tanzania njema, unaanza kuwafitinisha wapinzani.

hayo unayoyasema una uhakika nayo? au ndio sera yenu ya kukandamiza kichadema?

mapokezi na part CUF hawamo? waliosimama kumuunga mkono CUF hawamo? sababu moja ya upinzani kushindwa kusonga mbele kwa ujumla wao hawaaminiani, CUF anajiona yeye ndio anastahiki kuwasaidia watanzania, Cha Dema(kudema nnakusudia hapa) nao wanaona kudema dema kwao kwa ajili ya wananchi.

na hapo sasa CCM ndipo inapotesa, jipangeni msigawanyike.
 

Kaka moja mimi sio CHADEMA lakini ukweli ni kuwa najitahidi kuwajua vizuri ndugu zangu hawa. Uchambuzi wa kisiasa ni fani yangu na sio ushabiki....Na yote haya huwa nawaambia wale ninaodhani kuwa wana masikio kwa faida ya Tanzania yangu kwani naamini wote wana mchango mkubwa kujenga Tanzania yetu tunayopenda kuiona na kuipusha huko inapokwenda tunapohofia kufika...

Tanzanianjema
 
ebwana naam mambo yanaanza kujipa,na BREAKING NEWS nyingine ni kuwa yule mama wa UWT aliyemuuzia Manji jengo la pale Morocco walipokuwa wanatumbuiza wananjenje kajiuzulu,mamo hayo jamani...walafi wanzidi kuumbuka.
 
ebwana naam mambo yanaanza kujipa,na BREAKING NEWS nyingine ni kuwa yule mama wa UWT aliyemuuzia Manji jengo la pale Morocco walipokuwa wanatumbuiza wananjenje kajiuzulu,mamo hayo jamani...walafi wanzidi kuumbuka.

eeh kumbe ni kweli pale gogo kauziwa Manji...Anaitwa mama nani?
 
ebwana naam mambo yanaanza kujipa,na BREAKING NEWS nyingine ni kuwa yule mama wa UWT aliyemuuzia Manji jengo la pale Morocco walipokuwa wanatumbuiza wananjenje kajiuzulu,mamo hayo jamani...walafi wanzidi kuumbuka.


eeh kumbe ni kweli pale gogo kauziwa Manji...Anaitwa mama nani?


Wandugu kumradhi tusichanganye mambo...naomba niwasihi muazishe topic nyingine kuhusu Manji + Gogo Hotel na huyo Mama wa UMT. Hii topic ya Dr Slaa MB kuondoa hoja bungeni ina unyeti wake, tuipe nafasi.
 
Mimi sidhani kama kuna chance ya Chadema kuishinda serikali/ccm bungeni. Hivyo wao kwenda kujinga upya sioni kama kuna lolote wanaweza kuongeza au kupunguza iwapo hoja ilishaandaliwa kwa makini tangu mwanzo. Kwa maoni yangu Dr Slaa na Chadema wasingeiondoa hoja, wao wangeipeleka na kuwapa watanzania nafasi ya kuwasikiliza wakiwawakilisha bungeni. Kuondoa hoja ni kunapeleka ishara kuwa huenda haikuwa imeandaliwa madhubuti au ni dalili za woga.

Naomba kuwakilisha.
 
CUF wapo na kwa taarifa yako ndio wanaofanya upinzani wa kweli, hawa wengine wote ni wasanii tu na hawana tofauti na sisiemu.

Au unataka nao waanze kampeni za propaganda hapa JF ndio uwakubali? tunapozungumzia wapinzani kuwafikia wananchi vijijini basi CUF wajaribu sana katika hilo, kama huamini angali msuli wanaoutumia serikali dhidi yao.
 
Kakalende,
CUF nadhani wapo JF sema tu hawajapenda kujitambulisha kama CHADEMA
 
ebwana naam mambo yanaanza kujipa,na BREAKING NEWS nyingine ni kuwa yule mama wa UWT aliyemuuzia Manji jengo la pale Morocco walipokuwa wanatumbuiza wananjenje kajiuzulu,mamo hayo jamani...walafi wanzidi kuumbuka.


..kwenye chama waende serikalini!

..au wanajipanga?
 
Tunahitaji akina Zitto 200 na akina Mudhihir 0 bungeni!

kitilamATyahoo.com
0754 301 908
 
nikiwa nafuatilia mchakato mzima wa suala la BoT, nimesikitishwa sana na kitendo cha mheshimiwa Slaa kuondoa hoja yake bungeni.

Mheshimiwa Slaa na Wananchi wanaamini kuna mchezo mchafu umechezeka pale BoT.

Yeye kama mbunge, shughuli yake kubwa ni kuwatetea wananchi bungeni na pia kuihoji serikali kwa mambo kadhaa. Kitendo cha yeye kuondoa hoja ambayo ingeweza kuibana serikali kuwajibika ipasavyo katika suala hili la BoT mimi nakichukulia kwamba hakikubaliki.

Kama mheshimiwa Slaa anaiamini hoja yake,kama hana wasiwasi hata kidogo na vielelezo vya hoja hiyo anavyo ,kama mheshimiwa Slaa anaamini kwa dhati kwamba uchunguzi wa suala hili la BoT ni la muhimu kwa maslahi ya taifa letu kwa nini aondoe hoja yake bungeni?.

Mheshimiwa Slaa ni mbunge, na bungeni ndo mahala muafaka kabisa kupeleka hoja yake ya kuibana serikali, badala yake anaitoa hoja kutoka mahala palipo muafaka kabisa eti anakwenda kushitaki kwa wananchi,ala! mheshimiwa Slaa atuambie ANATAKA SISI WANANCHI TUFANYE NINI? Hii ni aibu kubwa, tena si kidogo!

Kwa nini asiiache hiyo hoja ijadiliwe bungeni halafu "at the same time" akatafuta namna ya kushitaki kwa kwa wananchi kama anavyodai?

Mheshimiwa Slaa anasema eti anazibwa mdomo,what! ,Yeye mheshimiwa Slaa mbunge ambaye ametumwa na wananchi kuwatetea wananchi bungeni anadai amezibwa mdomo! mheshimiwa atuambie, NA YEYE AMEKUBALI KUZIBWA MDOMO ASIIJADILI HOJA HIYO BUNGENI?

Mheshimiwa Slaa anataka kutufanya tuamini kwamba kuipeleka hoja hiyo kwenye mihadhara ni bora kuliko kuipeleka bungeni?

Mimi nitamuelewa mh Slaa iwapo atatueleza kwamba ameito hoja hiyo bungeni ili kuiboresha na kuisuka zaidi hoja hiyo halafu airudishe bungeni,na si tu eti anaiondoa bungeni kwenda kushitaki kwa wananchi,sijui anataka sisi wananchi tufanyeje,kwani sisi tuna mamlaka ya kuunda kamati kuchunguza suala hilo?
 
Wana JF nyinyi mna maoni gani kuhusiana na mheshimiwa slaa kuondoa Hoja ya msingi Bungeni na badala yake eti kwenda kushitaki kwa wananchi wakati anafahamu wazi kwamba wananchi hawawezi kuunda kamati ya bunge kuchunguza mkataba huo bila kupitia bungeni? je mnakubaliana na maelezo ya mheshimiwa huyu?
 
Gamba hata ile hoja alivyoiweka bunge ilikuwa ni aibu kwake pia yeye ametumiwa email bila kudhibitisha na kufanya utafiti akakurupuka je ingeundwa tume maalumu ya kuchunguza mambo yale si wangekuja mpaka jambo forums tuanze kushikana mashati ?

Bora amejua ukweli
 
Shy mimi nakubaliana na wewe kabisa kwa sababu haiingii akilini mbunge aondoe hoja isijadiliwe mahala muafaka kabisa bungeni ambako "meaningful action inaweza kuchukuliwa" badala yake eti aipeleke kwa wananchi ambapo hata wakinungunika hakuna kitakachofanyika .

Mimi nasema kwa hatua hii mheshimiwa Slaa amerudisha nyuma harakati za kumkomboa Mtanzania
Au mheshimiwa Slaa ameishakatiwa Percent? na hizi kauli za kwenda kushitaki eti kwa wananchi ni blah! blah! tu za kutuzuga ili aonekane alikuwa serious?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…