Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,934
Wakuu kuna hiki kitu kimekuwa kikinitatiza saana kujua chanzo halisia cha wanandoa kutoelewana kila kukicha wakati wa uchumba wao walikuwa wanaelewa na walikuwa pamoja kwa kila kitu.
Na je pindi tatizo ndani ya ndoa litokeapo ni nani hasa anastahili kuja kutatua na kupatanisha toafuati zilizopo?
Nisaidie tafadhali
- Hivi hiki kitu kinatokana na mmoja wa wanandoa kuridhika na hali ya ndoa? au
- Inatokana na kutikubali kujishusha hata kama amekosea ila atalazimikia kuawa juu wa wababa? au
- Inatokana na watu kutokubaliana kumaliza tofauti zao pindi zitokeapo na kualika watu wa njee ili waje kuzimaliza kana kwamba ndoa ya watu wawili ni ndoa ya jamii?au
- Inatokana na mmoja wao kutokubali kubadilika na hali halisia ya ndoa kuwa kila kitu kina kuwa kimoja badala yake kila mmoja anaendelea kukumbatia tabia aliyokuwa nayo kipindi cha uhuru wake kabla ya kuoa au kuolewa?
Na je pindi tatizo ndani ya ndoa litokeapo ni nani hasa anastahili kuja kutatua na kupatanisha toafuati zilizopo?
- Je ni wapambe wa harusi?
- Je ni wazazi wa pande zote mbili?
- Je ni marafiki wa karibu hata wale ambao hawajaoa japo ni marafiki?
- Je ni washenga ?
Nisaidie tafadhali