Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Saa ingine kuna kuchokana tu na suluhisho la hilo ni kila mtu kuanza kivyake. Unajua kuwa na mtu huyo huyo day in day out kunachosha? Binadamu tumeumbwa kuwa na matamanio na matamanio yetu hutufanya kuchoka na kutamani vingine.
Kwa mfano, wakati bado mko wapenzi wapya mlikuwa mnapendana sana. Mlikuwa mnakumbukana sana. Mwenzio ndio alikuwa mwanzo na mwisho. Lakini baada ya kuwa pamoja kwa muda, mnaanza kuonana wa kawaida sana. Ule u-special unapungua. Katika muda huu unakuwa tayari unajua ushuzi wa mwenzako unanukaje. Harufu ya mdomo wake ikoje asubuhi akiamka. Unakuwa unajua harufu ya mavi yake. Mwishowe anaanza kukutia kinyaa. Haya yote yanapelekea kuanza kumwona mwenzako kuwa wa kawaida sana na pengine kuanza hata kukuudhi. Na ukishaanza kuudhika basi ujue huo uhusiano umefikia hatua mbaya.
Mahusianio ni mambo magumu sana. Yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
Ili kuzuia matatizo ya kutoelewana, dawa kamili ni mapenzi ya kweli. Kama mlikuwa mnapendana kwa dhati, hamtachokana. Watu wanaishi maisha bwana!