Kutoa ushuhuda kuhusu suala la ajira

akiomwa

Member
Feb 4, 2015
34
19
Hello ndugu zangu wana JamiiForums,

Natumaini wote ni wazima. Mimi pia ni mzima. Binafsi si mkongwe sana JamiiForums lakini lazima nikiri kuwa JamiiForums imenifungua mengi sana na kunisaidia katika mengi kwa namna moja au nyingine. Kama ilivyo kwa wengi na mimi pia nilikuwa katika mahangaiko ya kusaka ajira hasa serikalini kwa muda mrefu; nilikuwa nikikatishwa sana tamaa baada ya kuona linatolewa tangazo na sekretariati ya ajira huku nafasi ni 1 lakini wanaoigombania ni zaidi ya watu 300.

Nilikuwa siamini kuwa bahati kama hii inaweza ikaangukia upande wangu lakini kupitia ushuhuda ambao wadau walikuwa wakiutoa humu JamiiForums kuwa walifanikiwa kupata kazi serikalini katika competition/ushindani kama huo tena kwa njia halali kabisa na mimi nilikata shauri kupambana nikiamini siku moja mambo yatakaa poa.

Namshukuru sana Mungu na pia nawashukuru sana wanaJamiiForums kwa moyo wenu wa kufunguka na kushare ideas kwani hatimaye jana nilipigiwa simu kuwa nimefaulu kupata kazi katika mamlaka moja ya serikali (TMA/mamlaka ya hali ya hewa) na ndio nipo katika michakato ya kukamilisha taratibu zao ili nianze.

My dear brothers and sisters, never give up!, ukimshirikisha Mungu na kuamini na kuweka juhudi pasipo kukata tamaa kila kitu kinawezekana duniani hapa nothing is impossible (Neno lenye impossible ukilitenganisha linasema I'M POSSIBLE). Msikate tamaa wanaharakati wenzangu, when your time comes no one will be able to stop anything.

Thanks and be blessed much

Nawasilisha
 
bado mtihan mgumu unakusubiri unaitwa "jinsi gani utayamudu maisha" hiyo mishahara ya vilak lak hku umekaa ofcn tu mda wote ni shiida
 
Good na Praise him all the tym. Achana na mtu anakuambia kilaki laki.
 
bado mtihan mgumu unakusubiri unaitwa "jinsi gani utayamudu maisha" hiyo mishahara ya vilak lak hku umekaa ofcn tu mda wote ni shiida

Kama aliweza kuishi bila ya hiyo kazi ambayo anaona sasa hivi ni mkombozi zaidi yaalivyokuwa awali basi amini emeishapiga maendeleo hatua nyingi mbele
Na chamsingi ni kuridhika na ulichokuwa nacho siyo kujiringanisha na watu fulani hapo kweli utaumia na maisha yatakuwa balaa sana kwako
 
Hongera mkuu ni funzo tosha na mimi sitokata tamaa najua kuna siku nitapata.Amina.
 
Nikisikia kazi ya kuajiriwa natamani kutapika, utumwa mtupu., yaani dume zima unapangiwa muda wa kuamka, kuingia kazini, kunywa chai, kula lunch, kuondoka, kupumzika, aisee,,hayo yanaitwa mateso bila chuki, KUJIAJIRI NDIO MPANGO MZIMA.
 
Nikisikia kazi ya kuajiriwa natamani kutapika, utumwa mtupu., yaani dume zima unapangiwa muda wa kuamka, kuingia kazini, kunywa chai, kula lunch, kuondoka, kupumzika, aisee,,hayo yanaitwa mateso bila chuki, KUJIAJIRI NDIO MPANGO MZIMA.

mbona vijana wa lile jukwaa la kule wanasema umeajiriwa Lumumba au wanakutania tu mkuu.
 
Back
Top Bottom