Kutoa ushuhuda kuhusu suala la ajira

Kutoa ushuhuda kuhusu suala la ajira

Hongera sana mkuu kwa kupata kazi na kushare na sisi. Na sie wengine bado tunasubili nafasi yetu. Mungu atasaidia soon tutapata pia.
Bless.
 
Hongera sana mkuu kwa kupata kazi na kushare na sisi. Na sie wengine bado tunasubili nafasi yetu. Mungu atasaidia soon tutapata pia.
Bless.

thanks sana! naamini nafasi yenu pia itakuja. my duty now is to pray kwa ambao bado wanatafuta kaz kama ilivyokuwa kwangu! Good Luck!
 
Amina natamani nami nije nitoe ushuhuda kama wako. Hongera sana mkuu
 
Nikisikia kazi ya kuajiriwa natamani kutapika, utumwa mtupu., yaani dume zima unapangiwa muda wa kuamka, kuingia kazini, kunywa chai, kula lunch, kuondoka, kupumzika, aisee,,hayo yanaitwa mateso bila chuki, KUJIAJIRI NDIO MPANGO MZIMA.

Nidhamu ya kazi ndio mpango mzima, kama huna hiyo hata ukijiajiri ni kazi bure, Sasa wewe jiajiri alafu uwe unaamka saa 6 mchana kila siku ndio utaona matokeo yake. Kujiajiri haina maana uhuru wa kupitiliza na uliokosa nidhamu katika mipangilio yako ya kila siku. Wise up kijana!
 
Nikisikia kazi ya kuajiriwa natamani kutapika, utumwa mtupu., yaani dume zima unapangiwa muda wa kuamka, kuingia kazini, kunywa chai, kula lunch, kuondoka, kupumzika, aisee,,hayo yanaitwa mateso bila chuki, KUJIAJIRI NDIO MPANGO MZIMA.
Khaa we si umeajiriwa kwa posho ya buku saba kwa siku ama??
 
nashukuru sana mdugu akiomwa, unazid kunipa matumain kwa asilimia 100, kuendelea kukomaaa...

uwezi hamini, mm pia jumapili ya tareh 10/5/2015, nilisafili kutoka mkoa wa kagera kuja kufanya usail ambao tulikuwa tumeitwa watu 278, na waliweza kuhudhuria watu 102, lakin nilijikuta nakuwa wa 6 kwa alama 54, ingawa nilipitiw na mstari na kupewa status ya unselected, nilijikuta napata nguvu ya ajabu pamoja nakuombea hii tume iendelee kusimama katika haki..

kiufupi umeendelea kunijaza matumain, thank u
 
Hello ndugu zangu wana jamiiforums!

Natumaini wote ni wazima. Mimi pia ni mzima. Binafsi si mkongwe sana jamiiforums lakini lazima nikiri kuwa jamiiforums imenifungua mengi sana na kunisaidia katika mengi kwa namna moja au nyingine.

Kama ilivyo kwa wengi na mimi pia nilikuwa katika mahangaiko ya kusaka ajira hasa serikalini kwa muda mrefu; nilikuwa nikikatishwa sana tamaa baada ya kuona linatolewa tangazo na sekretariati ya ajira huku nafasi ni 1 lakini wanaoigombania ni zaidi ya watu 300; nlikuwa siamini kuwa bahati kama hii inaweza ikaangukia upande wangu lakini kupitia ushuhuda ambao wadau walikuwa wakiutoa humu jamiiforums kuwa walifanikiwa kupata kazi serikalini katika competition/ushindani kama huo tena kwa njia halali kabisa na mimi nilikata shauri kupambana nikiamini siku moja mambo yatakaa poa.

Namshukuru sana Mungu na pia nawashukuru sana wanajamiiforums kwa moyo wenu wa kufunguka na kushare ideas kwani hatimaye jana nilipigiwa simu kuwa nimefaulu kupata kazi katika mamlaka moja ya serikali (TMA/mamlaka ya hali ya hewa) na ndio nipo katika michakato ya kukamilisha taratibu zao ili nianze.

My dear brothers and sisters, never give up!, ukimshirikisha Mungu na kuamini na kuweka juhudi pasipo kukata tamaa kila kitu kinawezekana duniani hapa. nothing is impossible (Neno lenye impossible ukilitenganisha linasema I'M POSSIBLE).

Msikate tamaa wanaharakati wenzangu, when your time comes no one will be able to stop anything. Thanks and be blessed much! Nawasilisha!

Congratulations mkuu ngoja na sisi tupambane I hope kitaeleweka Kwa uwezo wa mungu!
 
Back
Top Bottom