Ukosefu wa ajira usidumaze umuhimu wa elimu yako

Aug 30, 2023
86
111
Natumaini Sote wazima, kuna watu wanawahi sana kukata tamaa, inafika hatua mtu anaona borea asingesoma, Elimu ina umuhimu mkubwa sana katika Jamii na maisha kiujumla , kwa hyo suala la ugumu wa upatikanaji wa ajira usikufanye ukaona kama hauna thamani na usiithamini elimu yako.

Kitu chochote huwa ni kibaya Ukiwa nacho, ndio maana Ukiwa hauna unakua inakitamani, kwa wale tuliokulia vijijini Jamii zetu zina imani sana na sisi wasomi na wanaamini tunaweza kufanya mageuzi makubwa kupitia elimu zetu tulizopata.

Wadogo zetu pia wanatuangalia sisi watangulizi wao kama mifano ya kuingwa katika suala la elimu, hivyo tusijikatie tamaa.

Kikubwa kuongeza ujuzi kulingana na mabadiliko ya teknolojia, kuongeza ujuzi zaidi na kufanya mambo katika mtazamo wa kipekee na sio kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom