Kutoa Msaada Hadi Ujitangaze/uite Media?

aghalabu misimu ya sikukuu kama hiz makundi mbalimbali ya watu hujitokeza kusaidia hususan vituo vya watoto yatima, ni jambo jema lakn inaonekana ni kama sehemu ya kujitangaza hivi na mtu haridhiki kutoa hadi aite media au ku-post kwenye social media picha za tukio etc

maoni yangu

  1. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
  2. maandiko yanasema utoapo mkono wa kulia hata wa kushoto usijue
  3. ......................wewe unasemaje katika hili?

if you are in business you know it that 'The only thing worse than being talked about is not being talked about'
 
aghalabu misimu ya sikukuu kama hiz makundi mbalimbali ya watu hujitokeza kusaidia hususan vituo vya watoto yatima, ni jambo jema lakn inaonekana ni kama sehemu ya kujitangaza hivi na mtu haridhiki kutoa hadi aite media au ku-post kwenye social media picha za tukio etc

maoni yangu

  1. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
  2. maandiko yanasema utoapo mkono wa kulia hata wa kushoto usijue
  3. ......................wewe unasemaje katika hili?

Hahahahahahaaa!
Amavubi sasa mtu atoe bila kupata maujiko???
Kama mwakani anataka kugombea ubunge je?
Sasa nani ataproof utoaji wa mhusika?
...
Teh teh teh!
 
Hiyo sio misaada, ni UWEKEZAJI huo. Kuna mgombea udiwani mmoja alitoa msaada wa mifuko ya saruji, alivyoshindwa kwenye uchaguzi akaenda na mabaunsa kudai saruji yake, akakuta jamaa wamechanganya zege wanajenga kanisa alinyang'anya zege. Wanaojitangaza wana malengo hao.

Hii kiboko!
 
Iko hivi, nia au dhamira ya mtoaji ndio inaamua kipi ni cha msingi. Kama mtu lengo lake ni kutoa kwa maana ya kutaka kubarikiwa na Mungu hatafanya showoff, lakini kama ni kibiashara lazima afanye showoff kwa sababu hilo ndio hasa lengo lake (Kujitangaza) hakuna jambo la thawabu hapo.

Mtu akitaka kufanya kwa nia au lengo la kupata thawabu kisha akajitangaza, hapati kwa sababu Maandiko yanasema, tayari umeshapata ujira wako kutoka kwa wanadamu, Mungu hana cha kukupa tena.
 
Msaada wa kweli hautangawzi hata siku moja. Msaada wenye malengo ya baadae ndio huo unatafutiwa mpaka mpaka waandishi wa habari.
 
unapotoa msaada kwania ya
kujitagaza sawa sawa km umetupa kwa maana dhamira yako ilikuwa ni
kushowoff but not give for humanity,kamwe bwana mungu awezi
bariki!
tuliosoma business au advertizing wanajua misaada ni moja ya promo na kujitangaza kibiashara na kujenga mahusiano na jamii inayokuzunguka
 
aghalabu misimu ya sikukuu kama hiz makundi mbalimbali ya watu hujitokeza kusaidia hususan vituo vya watoto yatima, ni jambo jema lakn inaonekana ni kama sehemu ya kujitangaza hivi na mtu haridhiki kutoa hadi aite media au ku-post kwenye social media picha za tukio etc

maoni yangu

  1. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
  2. maandiko yanasema utoapo mkono wa kulia hata wa kushoto usijue
  3. ......................wewe unasemaje katika hili?

Ndugu yangu kuna kitu kimoja ume-overlook hapa. Kuna watu wengine wanatembea wako na media muda wote hadi anakwenda kuachana nayo kwenye mlango wa kuingia chumba chake cha kulala, na anapoamka tu anakutana nayo mlangoni tena hadi jioni anapokwenda kulala tena. Watu wa aina hii hata ukishikana naye mkono wewe si ajabu baada ya lisaa limoja ukajikuta na wewe unaonekana kwenye media, kwamba ulishikana mkono na mtu kama yule. Watu kama hawa wanapotoa misaada yaweza pengine wao wenyewe huwa hawapendi isikike kwenye media ila wanajikuta tayari mambo yao yakohuko na hawana haki ya kuiziuia media kufanya hivyo kwa sababu ndiyo kazi yake. Tafadhali naomba hili uliangalie kwa mtizamo huo isije hadi ukasababisha watoaji wakajisikia vibaya, au wakaacha kutoa kabisa. After all, yupi bora, yule anayetoa kwa ajili ya attention ya media, au yule ambaye hatoi kama mimi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom