Ushuhuda wa Injili
JF-Expert Member
- Nov 12, 2012
- 427
- 160
Tumsifu Yesu Kristo mwana wa Mungu.
Jana tuliangalia kwa kiwango fulani jinsi maandiko yanavyotuambia kuwakumbuka maskini katika zaka na dhabihu zetu. Tuliona pia kwamba Mungu anawapenda sana maskini na ili nasi tuonyeshe upendo wa Kristo uliomo ndani yetu basi ni vema tukajifunza kuwasaidia. Tulijifunza kwamba si vizuri kumruka maskini jirani yako hapo karibu ana uhitaji unakimbilia kupeleka zaka kanisani tu (Labda kama unataka ukaonekane kwa mchungaji wako kwamba nawe huwa unatoa zaka hapo sawa waweza kufanya hivyo na utapata thawabu yako hapo hapo kwa kutaka uonekane).
Leo tutaangalia namna ya kutoa zaka na dhabihu zetu kwa ajili ya kuwahudumia wajane.
Mjane mara nyingi huwa tunatafsiri kuwa ni mwanamke alifiliwa na mumewe. Lakini mwanamume aliyefiliwa na mkewe huwa anaitwa mgane. Biblia inawaangalia sana wanawake wanaofiliwa na waume wao kwa sababu ya mfumo tuliokuwa nao wanawake mara nyingi waume zao wakifariki huwa wanapata shida. Hata kama nyumbani mume alikuwa na mali siku akifariki ndugu wa kiume hukimbilia kuzigawana mali za mjane.
Majuzi tu ndugu yetu katika Kristo alifiwa na mumewe. Kabla mwili wa marehemu haujafika eneo la nyumbani kwao kuzikiwa tayari mawifi walishaanza kugombania mali za marehemu pasipo kujali marehemu kaacha mke!!
Mwezi wa nne mwaka huu nilikutana na bibi ambaye nilikuwa nimepotezana naye miaka 20 iliyopita. Bibi huyu ni mjane zaidi ya miaka karibu 30. Amekulia ndani ya wokovu. Ameokoka zaidi ya miaka 40. Roho wa Mungu ametulia sana ndani yake. Ukitaka kupata hekima nenda kwa huyu bibi. Nilikuwa nikijaribu kumdodosa ni namna gani kanisa kama kiongozi, kama mwalimu, na kama mhubiri namna gani kanisa linawajali wajane katika jamii. Bibi yule akaniambia mjukuu wangu sitaki nionekane nagombana na viongozi wa kanisa. Lakini ukweli viongozi wetu wa sasa wamewasahau sana wajane katika jamii. Si tu kanisani lakini hata huko mitaani. Nilijisikia vibaya sana.
Viongozi wa kanisa la leo lazima tujifunze kusikia tunaowaongoza wanasema nini. Tukijifunza kuwasikiliza hao tutakutana na sauti ya Roho Mtakatifu kwa wingi ikisema nasi. Hakika viongozi tumewasahau wajane. Huduma za wajane hata tu makanisani (mtu anihukumu) leo zimekuwa chache mno mno. Nina ujasiri wa kusema kwenye makanisa mengine zimeshafutika!!.
Maandiko yanasema katika #Mdo 6:1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Hawa walikuwa ni wajane wa kiyunani ambao walikuwa wamesahaulika katika huduma ya chakula na mavazi huduma ambazo kanisa la kwanza lilijitolea kuifanya kila siku kwa wajane. Angalia vizuri mpendwa, kanisa lilifanya huduma hii kila siku!! Na sasa likajisahau. Mpaka watu walivyoanza kunungunika ndipo viongozi wa kanisa la kwanza wakawa kama wamefumbuliwa macho. Wakaibuka na kuwateua watu kushughulika na huduma za wajane ili wasikose huduma.
Ndugu yangu hata leo wajane wanalia kila kona. Wengine wao hawana watu wa kuwasaidia. Wanaishi maisha ya shida. Na watu tunaojiita wakristo tupo mitaani humo humo. Tumejaa ubinafsi hatuna hata muda wa kuwahudumia kikombe cha chai. Ndugu huwezi kujitolea hata vinguo viwli vitatu vya kumsitiri mjane huyu? Au kwa sababu si Mkristo? Una nguo ngapi ambazo huzitumii? Kwanini zingine usiwape wajane na maskini nao wafurahie upendo wa Kristo uliomo ndani yako? Unakula chakula na kusaza humkumbuki mjane yule jirani yako. Ukibeba kilo moja ya sukari, na kilo moja ya mchele na maharage mara moja kwa wiki ukawa unampitishia mjane yule nakuhakikishia katika jina la Yesu baraka za Mungu zitakuwa juu yako. Baraka zitafurika ndani yako. Haiwezekani mjane apate chakula kwa ajili yako halafu Mungu asifungue milango ya Baraka. Nakuhakikishia katika jina la Yesu Kristo Mungu atafungua madirisha ya baraka juu ya kazi zako, biashara zako, familia yako, watoto wako na wazazi wako. Mungu aliye hai na mwaminifu atafanya hivyo katika jina la Yesu.
Maandiko yanamtanabaisha Mungu kama Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane. Yeye anayewapa mema wajane kwa kunitumia mimi na wewe anatukumbusha leo tuwakumbuke wajane. Waangalie wajane walioko katika jamii yako ndugu yangu. Waangalie uhitaji walio nao. Wasaidie. Ukiziba masikio naye ataziba masikio juu yako.
Kuna watu wanapenda sana kutoa ili waonekane. Nataka nikufundishe mpendwa utoaji wenye baraka. Utoaji wa kimya kimya yani hata asante ikitolewa usiisikie. Tena ikibidi umkataze asimwambie mtu (Huwa napenda kufanya hivyo maishani mwangu. Sipendi nimsaidie mtu halafu aanze kunitangazia huko). Napenda utoaji wa kutoa halafu Baba aliye sirini anakushushia baraka zake mwenyewe. Bwana Yesu ametufundisha habari hii akisema Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Jifunze kuwasaidia watu hata kama hauabudu nao. Yamkini unaishi nao mitaani kwako. Jishughulishe na mahitaji yao hata kama utaweza kujiushughulisha na mahitaji madogo madogo. Mtume Paulo anatukumbusha akisema Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu. Hebu ewe mkirsto nakusihi jifunze kupata baraka za Mungu kwa kujishughulisha na wajane unaoishi nao mitaani. Jiwekee tu kautaratibu angalau hata mara moja kwa wiki mpelekee mjane fulani kilo moja ya mchele na sukali. Mjane mmoja tu mara moja kwa wiki kama hutoweza kufanya kila siku. Fanya mara moja tu halafu uupime uaminifu wa Mungu katika kukutolea hivyo uone.
Pia lazima kanisa lifundishwe kwa mtu mmoja mmoja kujua wajibu wa kuwahudumia wajane katika jamii tunazoishi. Sio kusubiri kutoa kwa maskini na wajane makanisani tu. Kanisa halisi linaanzia nyumbani kwako na kisha katika mtaa wako. Huko ndo kanisa halisi liliko. Huko ndo uhitaji halisi wa watu unakutana nao. Kama ambavyo tunapaswa kuwahudumia maskini katika jamii tunazoziishi ndivyo tunapaswa kutoa kwa ajili ya wajane pia. Na ili kanisa lisielemewe na majukumu mengi sisi wakristo tunaowajua wajane kweli kweli huku mitaani tujitolee kuwasaidia kwa namna iwayo yote. Mtume Yakobo anasema DINI ILIYO SAFI, ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGU BABA NI HII, KWENDA KUWATAZAMA YATIMA NA WAJANE KATIKA DHIKI YAO, NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO MAWAA #Yak 1:27
Nitafurahi wewe uliyeko katika jiji la Dar es salaam unayemjua mama ambaye ni mjane kweli, huduma yetu ya Neno la Uzima ingependa kuja kuomba pamoja naye na kushiriki neema ya Mungu pamoja naye. Si lazima awe Mkristo. Tutapenda kuja kushare naye neno la Mungu na upendo wa Mungu tuliyo nao. Kama unamjua hebu tujulishe. Naamini hata wewe unayesoma post hii tukitaka tushiriki baraka za Mungu pamoja nawe kwa nguo, sabuni au chakula hutosita kushiriki nasi kwa mjane kama huyo. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu ni Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao.
Imeandikwa Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina #Kumb 27:19
Mungu akubariki. Ukiwa na jambo unataka utushirikishe tuombe pamoja nawe, tutumie kwenye whatsapp tu kwa namba hii 0758443873. Ikiwa unataka kutupigia au kututumia sms ya kawaida basi tumia namba 0712204937. Kama unataka tuombe kwa ajili ya mtu fulani au kwa ajili yako tafadhali utupe majina yako kamili unayoyatumia ili tuombe mbele za Baba wa mianga kwa ajili yako.
Yamkini unataka upate mafundisho haya kila siku kwa whastapp basi save namba 0758443873 na kisha tuambie majina yako ili tuwe tunakutumia mafundisho.
HUDUMA YA NENO LA UZIMA