pakamwam
JF-Expert Member
- May 28, 2013
- 516
- 653
Naleta huu uzi kwa masikitiko makubwa sana juu ya unyanyasaji wa wanawake unaondelea maeneomengi sana kwenye mfumo wetu dume, mwanaume ukiona hupati mtoto kwenye ndoa miaka kadhaa wakati unahitaji na unajitahidi kukuruka.
Usikimbilie kumlaumu mkeo kuwa hazai njoo hospitali upime na upate uhakika
kutoa manii na kusimamisha hakumaanishi wewe sio tasa. Ili mbegu za kiume ziweze kurutubisha yai la mwanamke zinahitaji vitu vingi sana wapo watu wengi wanatoa manii kweli lakini unakuta ute wao ni mzito saana na hivyo mbegu haziwezi kuogelea ufikia yai, high viscosity.
Wapo wengine anatoa mbegu unakuta zimekufa kwa sababu mbali mbali, wapo wengine wanatoa mbegu lakini unakuata ni kidogo sana, wapo wanaotoa mbegu unakuta hazina mikia na mengine mengi sio vizuri sana unapokuta hampati mtoto kukimbilia kumlaumu mwenzako au kukimbilia kwa waganga wa kienyeji.
Ukienda hospitalini na ukafuata utaratibu unaweza ukapata majibu na ukasaidika
ni rahisi kupima utasa wa mwanaume kuliko mwanamke nimekuwa nikikutana na watu wengi sana ambao unakuta mwanaume anakomaa kumlaumu mwanamke lakini ukija kufanya vipimo unakuta shida iko kwake na akishajua unakuta anaanza kukuomba eti mdanganye mke wake aonekane yeye ndiye mwenye shida.
Tuache kuwakandamiza wanawake naamini tukitenda haki kuanzia kwenye familia zetu na kuwa wakweli tunaweza kuunda taifa zuri na kuishi kwa amani naomba leo niishie hapo kwa kusema wanaume tujitahidi sana kuepuka kuwanyanyasa wake zetu bila sababu.
Mungu aliwapa wanawake adhabu mbili tu, kuzaa kwa uchungu na kuwa na wivu juu ya mume wake. Nawaombeni wanaume wenzangu tusiwaongezee adhabu zaidi ya hizo mbili. zinawatosha sana. Kabla ya kuwalaumu baadala ya kuwalaumu tujichunguze na tuzielewe maana halisi za ndoa.Pia matatizo ya ugumba yanaweza kutibika au kutotibika kwa hiyo ni vyema kuwafuata madaktari na kuwa na subira.