Ifahamu PID kwa kina sehemu ya kwanza: maana ya PID, inavyotokea, dalili zake na madhara yake

Jul 24, 2017
31
17
1: MAANA YA PID.
PID ni kifupisho cha neno Pelvic Imflammatory Disease.
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria, bakteria hawa huenda na kushambulia via vya uzazi vya Mwanamke na kumletea mdhara mbalimbali.

PID huwashambulia wanawake tu na umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanawake. Tafiti inaonesha kuwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 25 ndio wamekuwa wahanga sana wa ugonjwa huu.

2: PID INATOKEAJE NA INAAMBUKIZWAJE?
PID hutokea pale ambapo bakteria kutoka katika uke au seviksi kusafiri hadi kufika katika via vya uzazi vya mwanamke ambavyo ni Uterasi, mirija ya falopio na ovari.

Chanzo cha bakteria hao kinaweza kuwa ni magonjwa ya kuambukiza/zinaa ambayo mtu huyapata kwa njia ya kujamiiana. Mfano wa magonjwa hayo ni Gonorea na klamadia na hii hutokea endapo magonjwa haya hayatatibiwa haraka.

Lakini pia PID inaweza kusababishwa ba bakteria wasiokuwa wa magonjwa ya zinaa. Na pia watu wenye U.T I na Fangasi sugu na kukaa nayo bila kuitibia wapo kwenye hatari ya kupata P.I.D.

NJIA ZA KUAMBUKIZWA PID.
Kama tulivyoona hapo juu kuwa chanzo ni Bakteria. Mtu anaweza kuwapata hawa Bakteria kwa njia zifuatazo.

(A) Kujamiiana
Kujamiiana kunaweza kumfanya mwanamke kupata magonjwa ya zinaa,fangasi au U.T.I endapo atakutana na mwanaume mwenye matatizo moja kati ya hayo.

(B) kutofuata kanuni za usafi pia kunaweza mfanya mwanamke kupata maambukizi ya PID.

3.DALILI ZA PID
: kutokwa na uchafu sehemu za siri (ukeni)
: maumivu ya tumbo chini ya kitovu
: maumivu ya tumbo upande wa kulia kwa juu
: bleed isiyo ya kawaida
:Homa isiyo ya kawaida
:kichefuchefu na kutapika
:maumivu wakati wa tendo la kujamiiana.

4. MADHARA YA PID
: UGUMBA

PID husababisha kovu katika mirija ya falopia na hivyo kufanya mbegu za kiume kushindwa kurutubisha yai la kike na hatimaye kusababisha kusiwe na utungisho wa mimba. Na hali hii ikitokea ndipo tunasema ugumba umetokea.

: MIMBA NJE YA MFUKO (ECTOPIC PREGNANCY)
Wakati mwingine inaweza ikatokea yai kurutubishwa vizuri na mbegu za kiume na hatimaye utungisho kufanyika. Lakini kwasababu ya kovu hilo kuwepo kukapelekea mimba iliyo tungwa kushindwa kusafiri hadi kwenye uterus ambao ni mji wa mimba. Na hii kulazimisha mimba kukua ikiwa ndani ya Falopia. Hii hupelekea falopio kupasuka na mimba kuharibika.
Hali hii ya mimba kutunga na kukua ndani ya falopio ndiyo huitwa Ectopic Pregnancy au mimba nje ya mfuko.
Na tiba ya ectopic huwa ni upasuaji.

: UPUNGUFU WA DAMU.
kumbuka moja ya dalili za PID ni bleed isiyo ya kawaida. Hali hii hupelekea kutokea kwa upungufu wa damu mwilini.

: KIFO
PID inaweza kusababisha kifo kwa mwanamke kama haito tibiwa mapema.

:MIMBA KUHARIBIKA.
PID inaweza kusababisha mimba kuharibika kila wakati. Hii ni kutokana na via vya uzazi kuwa na hitirafu.

ITAENDELEA...

KWA USHAURI NA MATIBABU JUU YA PID UNAWEZA WASILIANA NAMI KWA
WHATSAPP/CALL: 0625932259
IMG_20200719_143003_377.jpg
 
Utafiti unaonesha kuwa wanawake waliochini ya umri wa miaka 25 ndio wanao ongoza kushambuliwa na PID.
Na wanawake ambao wapo kwenye hatari zaidi ni wale wanaofanya mambo yafuatayo.

1. Wenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Mfano Gonorea na clamadia.

2. Wanawake wenye wapenzi wengi. Hawa nao wapo kwenye hatari ya kukumbqa na PID.

3. Wanawake wenye mpenzi mwenye wapenzi wengi.

4. Mwanamke ambaye alishawahi kuugua PID ni rahisi sana kwake kuugua tena kwa mara nyingine.

5. Wanawake wenye tabiabya kujisafisha ukeni kwa kutumia Sabuni.

Nukuu: kujisafisha uke kwa kutumia sabuni si njia sahihi ya kufanya usafi wa sehemu zako za siri. Sabuni inaweza sababisha kuzalishwa kwa bacteria ambao wanaweza kwenda hadi kwenye via vya uzazi na kukusababishia PID.

ITAENDELEA...
 
Wasomi wetu bhana, sasa wewe ulivyoikariri hiyo PID, unadhani ni watu wote wanaijua? Au hadhira yako pekee ndio yenye wanawake wanaoweza kuipata PID? Wanawake wasiojua kusoma na kuandika hawawezi kupata PID?
 
sio siri kila nikiona PID akili inaruka kwa Proportional Integral Derivative Controller
 
Back
Top Bottom