Kutekwa kwa Mohammed Dewji: Ni uharamia wa kimataifa?

MLETA MADA NAONA MMEANZA KUTULETEA NGONJERA ZA KUTUPOTEZA NI SAWA NA KIVUKO KUZAMA KWA UZEMBE AFU MNAANZA KUTOA HISTORIA KUWA HATA HUKO NANII KIVUKO KILIZAMA HAITA WAONDOA KTK DHAHAMA YA KUTOWAJIBIKA SASA KWA HILI LA MO MAVUVUZELA MMEPEWA MADODOKI NA MSASA YA KUSAFISHA HAKIKA KWA HILI WAHUSIKA HATACHOMOKA HATA KAMA WANA MAPEMBE KIASI GANI HAIJARISHI ANA CHEO GANI MUHUSIKA LAZIMA TUTAJUA MBIVU NA MBICHINA NA HAPA TUTAPATA PA KUANZIA KUJUA AKINA SAA NANE WALIPO, AZORY WAPIGA RISASI WA LISSU NA WENGINEO KWA HILI HATA MJE NA MSASA WA CHAINSAW HAPA KUNA KITU KIKUBWA KITAJULIKANA
 
Hahahaa kule Mkuranga, Kibiti na Rufiji wanajeshi wetu walikufa kama.kumbikumbi huku Mwigulu anakula bata pale ofsini kwao.

Hakuna tunachoweza hapa tanzania chini ya ccm, hakuna hata kimoja.
Natamani nikutukane ila basi tu.... 😷😷 jiangalie sana!
 
Kama waliomteka MO ni wazungu kweli basi hili sakata linatupeleka kwenye mashirika ya kujasusi (c.I.a,mossad na wengineo)pengine wanahitaji ushahidi fulani au wanataka kujua pesa zake zinatumika kusaidia vikundi vya kigaidi?

Mzungu atoke kwao aje kumteka Mo alafu atake pesa (ransom) sidhani kama inaingia akilini,nyuma ya pazia kuna kitu kikubwa mno ambacho muhusika na watekaji wanajuana(kama watekaji ni wazungu).hatujui ni mambo ya kibiashara labda yamepelekea kwa hawa wazungu kumteka lakini yote kwa yote bado inashangaza inakuaje wazungu waje kumteka Mo??
Ukweli wa tukio hili litakuja kutuacha mdomo wazi
Mawazo yako yanaishia chalinze tu
Huamini kuwa kuna wazungu majambazi!
 
Police wa Tanzania wajifunze mbinu wawalete hata FBI sio kukaa kushangilia ccm wameshinda jimbo la ukonga
 
Masikini Mo kaponzwa na mawasiliano yake na Hanz Pope... Uhasama wa Taifa wazee wa Makumbusho awamu yao hii wanafanya wanavyotaka bila ya kubughudhiwa wala kuulizwa
 
yan umentia aibu kwel,
hv bado unaamini kisa mzungu, ndo hawezi kuiba..? navyo vijizi
View attachment 894771Mohamed Dewji
View attachment 894772View attachment 894772
Liyaqat Parker Mfanyabiashara maarufu nchini Afrika ya kusini aliyetekwa na kuachiwa baada ya kulipa Randi milioni 3.4

Na. Habibu mchange

Leo Oktoba 11 mfanyabiashara maarifu nchini Tanzania Mohamed Dewji ametekwa na watu wasiojulikana katika hotel ya Collosium ambapo alikwenda kufanya mazoezi majira ya saa 11 Alfajir

Tukio la kutekwa kwa Mo linafuatia na kufanana kwa kiasi kikuvwa na mfululizo wa matukio ya kutekwa kwa wafanyabiashara wengine maarufu wenye asili ya kiasia kusini mwa bara la Afrika ambao wametekwa na baadae kuachiwa baada ya kupewa masharti kadhaa

Mo dewji anakuwa ni mfanyabiashara wa tano maarufu kutekwa barani Afrika ambapo wawili kati ya hao waliotekwa wanatokea Afrika ya kusini, mmoja Malawi mmoja msumbiji na Dewji wa Tanzania

Katika wote watano mashughuli waliotekwa, wane kati yao ni waafrika wenye asili ya kiasia (WAHINDI) huku mmoja akiwa ni mwafrika mweusi

Taarifa zinasema kuwa kwa miezi kazaa sasa kumejuwepo na kikundi cha kijangili kinachajihusisha na kufanya uharamia wa kuwateka wafanyabiashara wakubwa ili wajipatie fedha

Taarifa zinasema kuwa kikundi hicho kinaundwa na watu wenye asili ya kizungu wanaoishi sana Afrika ya kusini na Nigeria na wamekuwa wakifanya uhalifu huo kuzunguka maeneo kadhaa ya Afrika.

Ifuatayo ni orodha ya matukio ya wafanyabiashara waliotekwa katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

1.DAR ES SALAAM, TANZANIA


Kama ambavyo imeandikwa hapo juu, Mohamed Dewji, mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni mdau mkubwa wa michezo na sehemu ya mmiliki wa timu ya simba ametekwa hii leo katika eneo la hotel maarufu kabisa ya Colosium iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam

Imeripotiwa ametekwa, bado jitihada za kumuokoa zinaendelea kwa kasi kubwa na haijajulikana bado ni kina nani waliomteka na kwa nini?

Walioshuhudia wanasema Mo ametekwa na watu wawili wenye asili ya kizungu ambao walipaki gari karibu na gari yake na kufyatua risasi kisha kimteka

2. MAPUTO, MSUMBIJI

Tarehe 22 April 2018 mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye asili ya kiasia (Jina lake lilifichwa) alitekwa akiwa nje ya Gloria Hotel mjini maputo na kwenda kufichwa katika nyumba zilizo jirani na hotel aliyotekewa.

Katika tukio hili, watekaji waliomteka mfanyabiashara huyu walihitaji kulipwa jumla ya Dola za kimarekani 162,000/= sawa na wastani wa Shilingi 368,000,000/= za kitanzania
Bahati nzuri jeshi la polisi la nchi hiyo lilifanikiwa kumuokoa siku moja baadae na kuwakamata watekaji
Soma Zaidi
Police rescue Indian kidnap victim in Maputo - AIM report

3. LILONGWE MALAWI

Mfanyabiashara mwengine mwenye asili ya kiasia Atul Manek alitekwa nje ya nyumba yake iliyopo Eneo wanaloishi watu mashuhuli liitwalo area 9 mjini Lilongwe

Watekaji waliomteka Manek ambaye ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na anayesimamia kampuni kubwa kubwa Malawi na Afrika kwa ujumla, aliendelea kushikiliwa na maharamia watekaji hao hadi pale familia yake ilipolipa kiasi cha Dola 1,000,000/= sawa na zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni miambili themanini za kitanzania (2,280,000,000/=)

Watekaji hao waliielekeza familia na wasaidizi wake mahala pa kwenda kuiweka fedha hizo na walipohakikisha wameziona walimuachia huru
Soma Zaidi hapa

Malawi police treating Asian disappearance as kidnapping: Criminal gang took Atul Manek in Lilongwe | Malawi Nyasa Times

4. CAPE TOWN, AFRIKA YA KUSINI

Mfanyabiashara maarufu nchini Afrika ya kusini Liyaqat Parker mwenye umri wa miaka 65 ameachiwa kutoka kwa watekaji tarehe 18.09 mwaka huu baada ya kushikiliwa na watekaji kwa Zaidi ya miezi miwili mfululizo

Maharamia waliomteka mfanyabiashara huyo walitaka walipwe jumla ya Randi milioni 3.4 za Afrika ya kusini sawa na Zaidi ya shilingi Milioni 532,766,221/= za kitanzania soma Zaidi kwenye link hii
Kidnapped Cape Town businessman released


5. DURBAN, AFRIKA YA KUSINI

Mfanyabiashara mwengine maarufu nchini Afrika ya kusini Sikhumbuzo Mjwara aliripotiwa kutekwa tarehe 30 Agosti mwaka huu nje ya mahakama ya hakimu mkazi ya Verulam jijini Durban
Mfanyabi9ashara huyo anayemiliki mgahawa maarufu wa Barrio Restaurant uliopo Umhlanga‚ anasimamia pia biashara kadhaa nchini Afrika kusini

Mpaka sasa mjwara bado haijulikani alipo na jitihada za kuokoa maisha yake zinaendelea.

Soma Zaidi kwenye link hii Hunt continues for 'kidnapped' Durban businessman

MTAZAMO WANGU

Kwa kipindi cha miaka kadhaa nyuma, pwani ya Afrika na hasa Afrika mashariki iligubikwa na wimbi la maharamia wa kisomali waliokuwa wanateka meli za mataifa mbalimbali na kutaka kulipwa kiasi kikubwa sana cha fedha


Tunamshukuru Mungu serikali za ukanda huu zilishirikiana na taasisi za kimataifa kukomesha uharamia huo na kwa hivi sasa kwa kiasi kikubwa uharamia huo umekoma
Aidha miaka si mingi sana palikuwepo na wimbi la matukio ya mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakifanyika katika pwani hiyo hiyo ya afrika mashariki, mengi ya matukio haya yalikuwa yakifanywa na taasisi zilizojitambulisha kabisa kuwa ni Alshabab zilizopelekea kufanya mashambulizi makubwa na kuua atu wasio na hatia ikiwemo lile la Wetigate jijini Nairobi


Kudhibitiwa kwa matukio na majaribio haya kunasababisha maharamia kutunga mbinu na namna mpya ya kufanya uharifu, ndio maana kipindi cha tangu kuanzia mwezi April mwaka huu mpaka leo matukio kadhaa ya kitekaji yametokea na niliyoandika mimi ni haya makubwa tu mengine mengi sijayaandika


Ni wakati mahhsusi sasa wananchi wa maeneo haya yanayotokea matukio haya kushikamana na kila mmoja kuwa mmlinzi wa mwenzie
Mwezi Aprl limetolea Maputo, Msumbiji, mwezi june likatokea cape town South Afrika, Mwezi Augusti limetokea Durban Afrika kusini na mwezi huo huo Augusti limetokea Lilongwe Malawi huku mwezi Oktoba mwaka huu huu likitokea tukio kama hilo Dar es salaam Tanzania, ni nani anayejua Nairobi litatokea lini?, Kigali ama kampala ama popote Afrika

TUSHIKAMANE

TUMUOMBEE MO AACHIWE AKIWA SALAMA

Ndimi,
Habib Mchange
0762178678
mchangemchange@gmail.com
 
Itikadi za kijamaa wapatao tabu ni wasomi na matajiri, tabu huja wanapogoma kuishi kama mashetani,wenye kujua kuhusu itikadi za kijamaa huwa wanawahi kusepa mapema kuhamisha mitaji yao toka nchi za kusadikika. Matajiri Na wasomi watapata tabu sana,sie masikini tuko Salama. Masikini ni marafiki wa madikteta.
 
Kama waliomteka MO ni wazungu kweli basi hili sakata linatupeleka kwenye mashirika ya kujasusi (c.I.a,mossad na wengineo)pengine wanahitaji ushahidi fulani au wanataka kujua pesa zake zinatumika kusaidia vikundi vya kigaidi?

Mzungu atoke kwao aje kumteka Mo alafu atake pesa (ransom) sidhani kama inaingia akilini,nyuma ya pazia kuna kitu kikubwa mno ambacho muhusika na watekaji wanajuana(kama watekaji ni wazungu).hatujui ni mambo ya kibiashara labda yamepelekea kwa hawa wazungu kumteka lakini yote kwa yote bado inashangaza inakuaje wazungu waje kumteka Mo??
Ukweli wa tukio hili litakuja kutuacha mdomo wazi
Wazungu wengi tu Makapuku mzee,wazungu wametumika kama Mercenaries vita za Katanga huko Congo, Biafra war enzi hizo,washindwe kuja kumteka Mo wakihakikishiwa kuna pesa ya maana??
 
Shida kubwa ya an WaTanzania hawana free mind , kila Mtu anataka kusikia kile kinachoipendeza nafsi yake other wise unaonekana kituko na matusi juu
 
Logic yako imempandisha sana mzungu, kunu wazungu kibao hawana kazi, wana ujuzi wa kuteka.

Inawezekana kabisa wakaangalia mabilionea wa dunia, wakaangalia wapi hakuna ulinzi mkubwa, wakamuona MO anajiachia sana, wakaamua wamteke.
Niliwahi kupigiwa simu na Mzungu akiwa Dar akitaka nimtumie 50,000 kwa MPESA. Yeye alijifanya ni mteja wangu na kwa hiyo atanirudishia akifika Arusha. Nataka kusema kuna wazungu wengi biashara yao ni diverse ni pamoja na hizo ilegal business kama za utapeli, utekaji, pornography, madawa ya kulevya nk wamejaa hapo Dar. We kila ukimuona mzungu yuko kwenye jumba zuri au hoteli ya kifahari au anaendesha gari zuri unafikiri ana kazi ya maana kule ni tapeli, mwizi, mtekaji, pornographer, anauza unga nk
 
Back
Top Bottom