Wadau wa Bandari waomba TICTS isiongezewe mkabata

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
Na Marato Sinda, Dar es Salaam

Kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS) inadaiwa kushindwa kutekeleza makujukumu yake na wadau wa sekta za biashara na usafirishaji ambao wameitaka serikali kutoipa mkabata mpya kampuni hiyo kwa kushindwa kufikia lengo la kuongeza wingi wa mzigo kwa asilimia 37 kwa mwaka.

Wadau hao wameeleza kwamba kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa TICTS, kumesababisha ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam na kulikosesha taifa mapato kutokana na wafanyabiashara kuamua kuikwepa bandari na kukimbilia Kenya, Afrika kusini na Namibia zenye ufanisi.

Takwimu zinaonyesha kwamba TICTS walihudumia makontena ya futi 21 (TEUs) 606,169 mwaka 2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.8 kulinganisha na mwaka 2020 hivyo kushindwa kufikia lengo la kimkataba la kuongeza mzigo wa kontena kwa asilimia 37 kwa mwaka mmoja.

Wadau hao wamesema pia kwamba, kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa TICTS imefanya bandari ya Kenya kuwa kitovu yenye kupitisha makontena ya TEU milioni 2 kwa mwaka huku bandari ya Durban nchini Afrika Kusini ikijipanga kuongeza ufanisi hadi kufikia TEU milioni 11 ndani ya miaka michache ijayo.

Wabia wa TICTS ni pamoja na waziri wa zamani Nazir Karamagi na mfanyabiashara maarufu Yogesh Manek, wakishirikiana na mwekezaji wa nje, kampuni ya Hutchinson Ports ya Hong Kong.

John Tarimo, mfanyabiashara wa Dar es Salaama anayeagiza bidha kutoka China alisema serikali isiwape TICTS mkataba mpya tena kwani wameshindwa kufanya kazi kwa miaka 20 sasa na hivyo tenda hiyo ipewe kampuni nyingine itakayoweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan ametoka kulalamika kuhusu ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam hivyo akamtengua Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi na nafasi yake kumpa Plasduce Mbossa ambaye aliahidi kuongeza kufanisi wa bandari.
 
Ubaya Rais anatenguwa kwa kusikiliza minong’ono ya uwongo wa watu wanaotaka nafasi hizo Kwa wenyewe na jamaa zawo. Watu wanatenguliwa Kwa uwongo. Kuna mtu anaweza kunielezea kesi ya Kakoko iliishia wapi? Je alishitakiwa Kwa uwongo uliosejeiana kakutwa na Mabilioni ya dolla? Rais anatumbuwa bila kuchunguza kinachoendelea. Kuna watu wameishika nchi kupitia tenda zinazo ipa nchi hii hasara. Fedha hizo hizo wanazopata kwa kuitia hasara nchi, ndizo wanazotumia kuifanya viongozi ndani ya serikali kukaa kimya huku nchi inapata hasara. kwa nini Kenya waweze na sisi tushindwe? Wakati Tanzania geographically ipo vizuri kushinda Kenya? Je ni uongozi wetu?
 
Ni kweli TICTS wazembe ila usifanye comparison ya bandari ya Dar vs Durban/mombasa..katika africa India ocean hizo ndo zinazoongoza kwa ukubwa mbili za kwanza..nadhani sisi tupo ya nne...ukitaka tujilinganishe na hao serikali ipanue ukubwa wa bandari
 
Na Marato Sinda, Dar es Salaam

Kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS) inadaiwa kushindwa kutekeleza makujukumu yake na wadau wa sekta za biashara na usafirishaji ambao wameitaka serikali kutoipa mkabata mpya kampuni hiyo kwa kushindwa kufikia lengo la kuongeza wingi wa mzigo kwa asilimia 37 kwa mwaka.

Wadau hao wameeleza kwamba kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa TICTS, kumesababisha ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam na kulikosesha taifa mapato kutokana na wafanyabiashara kuamua kuikwepa bandari na kukimbilia Kenya, Afrika kusini na Namibia zenye ufanisi.

Takwimu zinaonyesha kwamba TICTS walihudumia makontena ya futi 21 (TEUs) 606,169 mwaka 2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.8 kulinganisha na mwaka 2020 hivyo kushindwa kufikia lengo la kimkataba la kuongeza mzigo wa kontena kwa asilimia 37 kwa mwaka mmoja.

Wadau hao wamesema pia kwamba, kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa TICTS imefanya bandari ya Kenya kuwa kitovu yenye kupitisha makontena ya TEU milioni 2 kwa mwaka huku bandari ya Durban nchini Afrika Kusini ikijipanga kuongeza ufanisi hadi kufikia TEU milioni 11 ndani ya miaka michache ijayo.

Wabia wa TICTS ni pamoja na waziri wa zamani Nazir Karamagi na mfanyabiashara maarufu Yogesh Manek, wakishirikiana na mwekezaji wa nje, kampuni ya Hutchinson Ports ya Hong Kong.

John Tarimo, mfanyabiashara wa Dar es Salaama anayeagiza bidha kutoka China alisema serikali isiwape TICTS mkataba mpya tena kwani wameshindwa kufanya kazi kwa miaka 20 sasa na hivyo tenda hiyo ipewe kampuni nyingine itakayoweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan ametoka kulalamika kuhusu ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam hivyo akamtengua Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi na nafasi yake kumpa Plasduce Mbossa ambaye aliahidi kuongeza kufanisi wa bandari.
Nyie ni kati ya machawa mliopewa hela kuisemea Ticts uongo Ili mabwana zenu kutoka Uarabuni wapewe Bandari badala ya Ticts.Tokea Ticts ianze kufanya Kazi hapa Dar haijawahi kufanya chini ya kiwango,mara zote imekuwa ikipitiliza na kuvunja viwango vya record ya upakiaji na ushushaji wa makontena,iliyowekewa na serikali.
 
Naona umepaniki mkurugenzi. Kwani madudu ya hiyo TICTS yenu yalianza leo? Mbona hata wabunge waliwalalamikia aana miaka ya nyuma kwa kupewa tender ambayo hamkuwa na uwezo nayo? Binafsi nitafarijika kuto kuongezewa mkataba mpya.

Ni ukweli hamna uwezo! Na huenda mna mchango mkubwa tu kwenye kuzorotesha huduma hapo bandarini. Na kama mnaonewa, si mkatafute tenda kwenye bandari nyingine! Mfano Mombasa, Beira, nk!

Kwani ni lazima muwepo bandari ya Dar es Salaam?
 
Una uhakika atayekuja baada ya ticts atafanya vizuri?
 
Back
Top Bottom