Kutapeliwa

hao hao walio sajili ndio watakamatwa, na hao ndio watawataja tu...
Shida unakuta kadi iliyotumika kusajilia siyo yake. Hawa wasajili laini ukienda kusajili wanafanya janjajanja wantumia kitambulisho chako kusajili laini 3 baadae wanaziuza
 
Aisee hawa jamaa wanabadili mbinu za kuiba kila leo...Asante kwakututoa tongotongo
 
Hiyo mbinu yako ndiyo muarobaini wa hao washenzi!

Pia usipokuwa makini kama ulivyofanya wewe, kuna mbinu nyingine ya kutuma na kublock!

Pesa inaweza ikaingia muda huo, ukiangalia salio linasoma, kimbembe kinakuja kwenye kutoa ama kuhamisha!

Ingawa mbinu hii ni rahisi ku follow up, lakini wezi hawajali kujivisha mabomu.
 
Moja ya sehemu akili inapaswa kua sharp ni kwa wafanya biashara mambo ya online business haya yanaliza watu. Mambo ya online business haya bana, bahat mbaya tz yetu hatujajikita kwatech. Hivyo tunapigwa kirahisi sana.

Ukienda polisi process ndefu kiasi cha kupoteza pesa nyingi na muda pia.

Pole mkuu sana, sioni ukitapelewa tena.
Muamini binadamu akiwa nje ya pesa.
 
Wala simumunyi maneno

Wewe jamaa Huna Akili sawasawa. Unafanya biashara halafu unapangiwa pesa yako itumwe kwa namba fulani!? Mfanyabiashara hata siku moja hamuogopi Mteja wake. Pumbavu kabisa
 
Hao wanakwambia uende Cyber crime, sijui uende polisi nikushauri tu wewe endelea na shughuli zako ushaliwa hivyo. Siku hizi laini zinauzwa kama pipi, haina cha kutia dole gumba wala namba yako ya Nida. Mjini shule
 
mjini shule
 
Huwa nikifanya biashara na mtu nisiyemjua ,huwa nataka cash mkononi ,ikishindikana akitumia muamala basi nahakikisha nauhamisha hapo hapo ili tukiachana akitaka kuhamisha iwe hola. lkn kitendo cha kuuwacha kwenye simu anaweza urudisha kwake
 
Matapeli wamekua wengi mjini kuna huyu nae ni tapeli,anajitangaza kua anauza vifaa vya electronics Instagram,kumbe ni tapeli,jihadharini nae kaliza watu wengi sana mjini.
Matapeli washughulikiwe wamezidi sasa
 

Attachments

  • Screenshot_20200626-135738_Instagram.jpg
    86.5 KB · Views: 7
Ila me sijaelewa hii..mbn mitandao yote inaingiliana? Yaan Sasa hv hakuna masuala ya kuulizana una voda? Si unatuma tu kwaoption ya "mitandao mingine"
Mitandao yote inaingiliana, tatizo linakuja unapotaka kureverse muamala ukiokosea mitandao inagoma, hapo ndipo Pana shida sana.
 
Anatuma kwanza pesa unahakikisha imeingia ndio unakabidhi mzigo Bro.

Watu mpo Darisalama bado mnapigwa kizembe hivyo.
Kupigwa hakuna mjanja Mkuu, hata wapigaji huwa wanapigwa nao pia.
 
Wapo waganga wa kweli, Kama huwajui sema usaidiwe, hachukui. Hela yako mpaka suala lako lifanikiwe. Ndiyo utaenda kumshukuru wewe mwenyewe
 
Umetoa Elimu Nzuri Mkuu.
 
Mfumo huu huwa hawatumi pin code zote kwako, zingine zinabaki kwa aliyekutumia hela ukifika ATM ndipo anakupatia zilizotumwa kwake mtumaji. Hapa nazungumzia kwa Uzoefu wa CRDB.
 
Huu mchezo umeanzia kwenye kampuni ya mtandao wa simu. Kwann

Kuna uwezekani mkubwa kabisa aidha jamaa akawa mmoja wa it wa airtel au ana mtu wake pale ndio maana akaprefer iwe airtel na si vinginevyo.

Meseji imekuja na jina kabisa, means imesajiliwa kikamilifu kama special number, kwahiyo airtel wameiruhusu ipite kwenye server zao kwluwa hawajaitilia shaka hata kidogo na ndio maana wakaongeza na kinukta ili isifanane na NMB wenyewe. Kwenye system haya mambo yapo. Kwawale mliomiliki simu za nokia haikuruhusiwa kutumia jina moja mara mbili, lazima uongeze herufu,namba au alama ili kuitofautisha. Sauti inatosha au niongeze? Wewe anzia tcra wana data zote maana wanahusika katika zoezi la usajili wa namba maalum (mfano, *150*00# n.k)
 
Mfumo huu huwa hawatumi pin code zote kwako, zingine zinabaki kwa aliyekutumia hela ukifika ATM ndipo anakupatia zilizotumwa kwake mtumaji. Hapa nazungumzia kwa Uzoefu wa CRDB.
Kisichotumwa kwako ni namba ya simu ya aliyekutumia tuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…