Mkuu matapeli wamezidi kua wajanja mimi nilipigwa laki 3 tu,nikaona ni kama milioni 3 hiv,kumbe watu wanapigwa vibunda virefu hivi.yaani tapeli wakikamatwa saiv nao sio wakuwaonea huruma.wanaliza watu na kuvuruga mipango kabisa na kama ni biashara wanakuingizia loss kubwa sana.Polee we,na karibu ndani ya club ya wahanga wa MITANDAONI. Juzi nilileta uzi wa kujinjwa pesa kupitia tigo pesa wachangiaji wakaninanga saana. Jàmani haya mambo yanaweza kukutokea ukabaki unashangaa hasa baada ya kuibiwa. Pole tena Jamaa yangu.
Hatari sanaHapa sasa ndo nimeelewa..
Huyo wala sio ndugu ni matapeli itakua walijipanga kumuibia mdauDah mkuu mimi jana nimefua suruali tatu nikaanika kama saa tatu usiku, nikalala maana hazikuwa zimekauka, nimeamka asubuhi hazipo, nimekuwa na uchungu mkali kwa suruali tu, sasa nakufikiria wewe, dah! Mtafute huyo ndugu yake uliyempa mzigo ule naye sahani, OVA
Sio ujinga hizo mambo zinatokea sana watu wanatapeliwa nyumba na mashamba sembuse milioni 1.Kila kukicha wajinga wanazaliwa.
............pesa ndefu kama hiyo kwanini hukumpa akaunti namba akadeposit huko?
hapa ni ushauri mzuri sana fika waeleze ishu nzima na toa namna zote zilizohusikahao mbona wepesi tu,nenda polisi kitengo cha cyber.
Mkuu pole hapo umepigwa. Wametumia bulk SMS na kwenye jina la sender wameweka (NMB.)
Next time hakikisha salio linasoma ndo utoe bidhaa. Yaani kufanya hivyo naandika script ya mistari michache sana ya Python + Bulk SMS API yoyote faster kitu kinatumwa
Pale mlinzi hawezi kukusaidia lolote zaidi inabidi upige simu benki husika ambapo watakupa maelezo utembelee branch yao na risiti then hela itarudi kwenye account baada ya masaaLakini Kuna Jambo nimekumbuka wiki mbili zilizopita nikiwa foleni NMB IRINGA aliingia Dada mmoja kutia hell ATM akafanya transaction akiomba na risit pesa haikutoka, ikatoka risit tu..ilikua saa moja jioni Dada wawatu akadata hataki kutoka kwenye mashine Hadi hela itoke...nikamuuliza km kwenye rist salio limepunguzwa jibu likawa nindio! Kuna muda huduma za bank zetu nazo nitatizo, je kwa wakala Hali ikoje? Sijawahi kuweka hell ndefu kwa wakala...yule Dada sijui walimalizana VP na mlinzi asiejua lolote kuhusu banking!
Kama nihivyo mifumo bank zetu haipo stable inawapa loophole wanaoweza kucheza nayo sasaHili la fedha kukataa kutoka na ikatoka risiti tu tena imeandikwa kuwa umetowa fedha huwa linatokea mara kwa mara. Hata mimi lilishanipata. Mwanzoni nilichanganyikiwa ila nilipoulizia benki wakanimbia kama fedha hazikutoka basi nisubiri kesho yake nione kama zimepungua kwenye account yangu. Mimi nilicheki muda ule ule na nikakuta hazijapungua. Limeshanipata kama mara tatu na muda wote fedha hazikupungua kwenye account yangu.
sasa mbona message imeingia kwa jina la NMB wakati hizo number mbili za airtel hazijawahi kuwasilianaAme edit meseji ya benki akaongeza tarakimu!!huu mchezo tumechezeana sana kwenye upatu na washkaji zangu !!!
Na si imeingia tu. Na wewe unaihamisha kwenda benki kwa simu na kuhakikisha zimeenda.Anatuma kwanza pesa unahakikisha imeingia ndio unakabidhi mzigo Bro.
Watu mpo Darisalama bado mnapigwa kizembe hivyo.
mzee wewe ni introvert?imekuaje message yake ije kwa jina la NMB? wamefanya mchezo gani hapo.maana I guess wewe na hiyo number ya mke wake hamjawahi kuwasilianaHiyo ishawahi nitokea Maeneo ya Kimara(Dar) .
Mchezo ulikuwa kama ifuatavyo.
Nimepewa mzigo toka zenji niufikishe kwa muhusika alouagiza. Mzigo ulikuwa unadhamani ya laki 7 na nikifika anipatie hiyo hela.
Muhusika alilalamika yuko bize muda wa mchana hivyo anaomba tukutane mida ya sa moja na nusu (Hiyo sa moja na nusu nilikuja elewa maana yake badae).
Muda ulipofika bado akachelewa akafika sa 2 . Alikuja na boda boda sehemu aliposema anikute na makubaliano ni kwamba anataka anitumie hiyo hela kupitia NMB maana nikatoe mimi kwani ataweka hadi ya kutolea.
Wasiwasi ukanijaa pia body language yake nilimuona sio mzuri(Kwenye kumsoma mtu nashukuru Mungu ninakipawa cha juu sana) . Nikaitikizia, akatuma hiyo hela tena sio yeye alidai mke wake ndo ataituma ,akampigia kweli mwanamke pale pale nikimskia baada ya dakika 2 nikaona msg imekuja kwangu kutoka NMB kwani alimpa namba zangu . Kilichonihakikishia kuwa sio hela ni hiyo NUKTA ambayo hata wadau wameisema ,Pia msg hiyo ilikuwa inakubali sehem pa ku reply(Navyofaham msg za huduma kubwa nyingi haziruhusu hilo)
Baada ya kuona haufu ya utapeli nilimwambia twende Kimara stendi pale hatuwezi kosa mawakala wakubwa wa ki benk tutoe hiyo hela.
Akadai. Akadai ana haraka ndo maana amekuja na bodaboda wa kukodisha.
Niligoma kataka kata . Na kuna muda nilipanick nika mwambia sababu ya mimi kukataa ni kwamba hii sio hela ila ni msg ili kuondoa huu utata twende tukaitoe wote nikupe mzigo wako.
Akasema kwa vile mimi simuamini basi ngoja anamwambia mkewe aombe wairudishe alafu kesho ataniletea cash. Niliitikia maana niliona nikupotezana Muda . Na baada ya hapo K namba yake haikupatikana ten ndo ikawa pona ya huo mzigo.
HAPO MTOA MADA NI USHATAPELIWA MAANA NILISHAKUMBANA NAYO HII
Kwa uzoefu wangu bwana Bongo kila kitu kindaendeshwa kwa uzembe. Nchi yetu ina watu wavivu na wazembe mno. Umeshakuwa ni utamaduni wetu.Kama nihivyo mifumo bank zetu haipo stable inawapa loophole wanaoweza kucheza nayo sasa
Shida unakuta kadi iliyotumika kusajilia siyo yake. Hawa wasajili laini ukienda kusajili wanafanya janjajanja wantumia kitambulisho chako kusajili laini 3 baadae wanaziuzahao mbona wepesi tu,nenda polisi kitengo cha cyber.