Kutana na mshauri bashite

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
Dear Adviser
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri
Fransiska wa Mwenge

JIBU
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo. Inawezekana plag mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye injin. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.
Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu.
 
Jamani nyie
e1de8d3a96df5c2294f7de9961c82803.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom