Ushauri wa bure!

martial arts

martial arts

Senior Member
Jun 26, 2014
183
225
*Dear Anko,*
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu. Nilimkabili mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu akasema atalazimika kumuacha huyo binti polepole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo anasoma college. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri Mzee wangu.
Mimi,
Fransiska wa Mwenge.

*JIBU*
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizimike? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo. Inawezekana plug mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye injini. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi hapo karibu warekebishe hivyo nilivyovitaja. Gari ikiharibika tena usiiache peke yake barabarani kuna vibaka sana.
Natumaini ushauri huo utakusaidia mwanangu.
Mimi Anko.
 
Mkuu wa Kibiti

Mkuu wa Kibiti

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
678
1,000
Pilipili za kutwanga kwenye kinu lazima ukohoe.Mshauriwa anaweza jitenga na dunia baada ya ushauri kufika.Naye akiondoka aache kurudi rudi nyumbani
 
Masanjehalima

Masanjehalima

Member
Oct 20, 2018
76
125
Cjakuelewa Mkuu
Uxhauri Gani Unataka
 
Y

Yukina

Senior Member
Feb 2, 2017
184
225
Hiyo anampenda sana huyo bint kwa hiyo kumwacha ghafla ataumia sana!! Ni huyo mumeo ndiye aliyeoza kwa huyo bint wala siyo kama unavyodangaywa !! Poleni sana
 
Top Bottom