Kutamani wafiwa hakufai!

Kutamani wafiwa hakufai!

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,508
Reaction score
13,974
Heshima kwenu wakuu?

Imekuwa ni tabia ya walio wengi kuanza kutamani wake/waume za watu,mara tu msiba unapotokea,wengine huanza kusema vibaya watu kuwa je ataweza kuvumilia bila ya kuwa na mwenza?

Kwa mfano hivi sasa waheshimiwa wabunge wamefariki,ila nimeona kwenye mitandao ya kijamii wakiposti picha za wenzi wao na kuanza kuwasifia kwa matamanio,nimeshindwa kuelewa hivi huu utamaduni wa kuwataka wajane kabla ya msiba kuisha umeanza lini? Mtu amefiwa na mwenza wake,wengine wanafika msibani ili kuona neema za Allah jinsi mjane alivyoumbika badala ya kumuombea kheri marehemu huko aliko,binafsi nimekerwa sana na wenye tabia hizo.

Tuelewe kwenye msiba ni sehemu ya maombolezo na sio sehemu ya kutamaniana hasa kwa wafiwa,pia kila nafsi itaonja mauti,ingekuwa wewe ungejisikiaje mkeo/mumeo atamaniwe/atongozwe wakati wewe bado hata kuzikwa/kuoza?

Tubadilike!!!
 
Wewe ndo una matatizo
sababu binaadamu jinsi walivyo huwezi ku wa control
watu wanatongoza hadi makaburini...
huku wanajua aliekufa pengine amekufa na AIDS..

Dunia hii ina 'vichaa wa kila aina'
ukianza kukemea vichaa wa aina hii mara ile utaishia na wewe kuugua kichaa
 
Nipe ushauri nifanyaje mkuu?

Wewe ndo una matatizo
sababu binaadamu jinsi walivyo huwezi ku wa control
watu wanatongoza hadi makaburini...
huku wanajua aliekufa pengine amekufa na AIDS..

Dunia hii ina 'vichaa wa kila aina'
ukianza kukemea vichaa wa aina hii mara ile utaishia na wewe kuugua kichaa
 
Sema mtu kupewa sifa sio tatizo, tatizo ni kumtamani.... Hata mimi nimpongeze bro Deo (R.I.P) pale alichagua mke haswa.
 
Mtu akishatamani anapelekea kutenda dhambi ya ngono,na wengine huwateka wajane kimapenzi na kupelekea kutelekeza familia,shida kubwa ya kutamani wajane hutokea kwenye familia zenye uwezo.Akina mariooo huwa hawachezi mbali.!!

Sema mtu kupewa sifa sio tatizo, tatizo ni kumtamani.... Hata mimi nimpongeze bro Deo (R.I.P) pale alichagua mke haswa.
 
Pale jamaa kachagua. Ngoja tumtafutie kauzu mmoja wa kule bungeni akaendelee kula neema za mungu.
 
Heshima kwenu wakuu?

Imekuwa ni tabia ya walio wengi kuanza kutamani wake/waume za watu,mara tu msiba unapotokea,wengine huanza kusema vibaya watu kuwa je ataweza kuvumilia bila ya kuwa na mwenza?

Kwa mfano hivi sasa waheshimiwa wabunge wamefariki,ila nimeona kwenye mitandao ya kijamii wakiposti picha za wenzi wao na kuanza kuwasifia kwa matamanio,nimeshindwa kuelewa hivi huu utamaduni wa kuwataka wajane kabla ya msiba kuisha umeanza lini? Mtu amefiwa na mwenza wake,wengine wanafika msibani ili kuona neema za Allah jinsi mjane alivyoumbika badala ya kumuombea kheri marehemu huko aliko,binafsi nimekerwa sana na wenye tabia hizo.

Tuelewe kwenye msiba ni sehemu ya maombolezo na sio sehemu ya kutamaniana hasa kwa wafiwa,pia kila nafsi itaonja mauti,ingekuwa wewe ungejisikiaje mkeo/mumeo atamaniwe/atongozwe wakati wewe bado hata kuzikwa/kuoza?

Tubadilike!!!

Agano la urithi lina nguvu MTU anapokua hai,na halina nguvu asipokua hai.(Ebr.9:17-19)
 
Kwa kifupi ulichozungumza ni maneno ya kweli kabisa. Kwenye miji mikubwa kama Dar siku hizi imekuwa ni fasheni msibani ni sehemu ya mtu kwenda kujaribu bahati yake (meeting place W4M or M4W). Utakuta mademu wakiwa mkao wa kuopoa dume au wanaume kuopoa ngoma🙂 (na wakati mwingine ikawa umeopoa ngoma ya u-kweli🙂

Wee si unaona hata misiba yenyewe siku hizi wajane na waombolezaji wanavyowaka (wako sopusopu na nini) wakiwa washatoka saloon, wamepiga suti na wanawake dresses na dark glasses. Na sio yale mambo ya kuwa ukifiwa huogi siku saba, kujirusha mavumbini huku mjane akijivika matenge na kanga au kaniki zinawaporomoka kama zamani. Na wala wajane hawalii kwa sauti (huku wakinena kilugha🙂 kama zamani....sijui ya mambo eti unakaribia msibani unasikia yowe... 'Mayoooooo weeee murume wangu ooooh Mayoooooo weeee oooh"...aaah wapi siku hizi!. kwi!

Kwa hiyo tuseme yote haya ni matokeo ya utandawazi. Na ukweli ndio 'USASA' wenyewe.
 
Shida iko wapi kufariji wajane?

Mjane akifiwa maana yake ile nafasi ya marehemu iko wazi ni juhudi zako kuipata na kuziba pengo.

Jamaa yangu mmoja ni mtaalam kwa wajane ananiambia wajane wazuri sana, hawana shida kabisa.
 
Heshima kwenu wakuu?

Imekuwa ni tabia ya walio wengi kuanza kutamani wake/waume za watu,mara tu msiba unapotokea,wengine huanza kusema vibaya watu kuwa je ataweza kuvumilia bila ya kuwa na mwenza?

Kwa mfano hivi sasa waheshimiwa wabunge wamefariki,ila nimeona kwenye mitandao ya kijamii wakiposti picha za wenzi wao na kuanza kuwasifia kwa matamanio,nimeshindwa kuelewa hivi huu utamaduni wa kuwataka wajane kabla ya msiba kuisha umeanza lini? Mtu amefiwa na mwenza wake,wengine wanafika msibani ili kuona neema za Allah jinsi mjane alivyoumbika badala ya kumuombea kheri marehemu huko aliko,binafsi nimekerwa sana na wenye tabia hizo.

Tuelewe kwenye msiba ni sehemu ya maombolezo na sio sehemu ya kutamaniana hasa kwa wafiwa,pia kila nafsi itaonja mauti,ingekuwa wewe ungejisikiaje mkeo/mumeo atamaniwe/atongozwe wakati wewe bado hata kuzikwa/kuoza?

Tubadilike!!!

Mkuu kwani unadhani masihara kuhusu uKIFAA wa mama Filikunjombe?
 
mauti,ingekuwa wewe ungejisikiaje mkeo/mumeo atamaniwe/atongozwe wakati wewe bado hata kuzikwa/kuoza?
Tubadilike!!! mkuu kwa kweli umeniacha hoi..sasa utajisikiaje kivipi wakat tayar umwkufa..okey nitajiskia vibaya sana asee mtu aanze kumnyemelea wife wakat mwenyewe hata sijaanza kuoza na bado nina ham na mke wangu...yan tena hasira zikizidi natoka kaburini kuleta zogo...ha ha ha only at jf
 
Hao wajane lazima waolewe tena.
Kwahiyo kuwatamani sio vibaya.
 
Dunia inawayawaya roho chafu na laana vimetapakaa nafsini mwetu wanadamu!Mleta uzi ameamua kuwa wazi kwamba ingekuwa uwezo wake angependa kummliki mjane wa Deo!Nimelitambua hili kwa saikolojia ndogo tu,na si yeye peke yake na wengine pia.Eee Mwenyezi Mungu kawajaze roho wako mwema ili wafikiri na kutenda yakupendezayo ewe muumba wa ulimwengu,na uwasamehe kwa mawazo na matendo yao mabaya! Pia unisamehe hata mimi kwani sijakamilika na pia nisiwahukumu wenzangu kwani wewe ndiwe hakimu pekee,ni katika jina la Bwana wa sabato Yesu Kristo Amen!
 
Back
Top Bottom