Kusoma vitabu vingi kwa muda mfupi

Kusoma vitabu vingi kwa muda mfupi

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
483
KUSOMA VITABU VINGI KWA MUDA MFUPI.
********************************************
Baada ya kuweka listi yangu ya vitabu nilivyosoma mwaka jana marafiki wengi walikuwa ‘impressed’ na kuanza kutamani kusoma vitabu vingi zaidi, au kuanza kusoma vitabu. Wengi wametamani kujua ni njia gani wanaweza kutumia kusoma vitabu huku wakiendelea na shughuli zao kama kawaida. Wengine wanahisi orodha ile ni ya kughushi na kwamba si rahisi kusoma vitabu 40+ kwa mwaka. Hawajui kuna rafiki yangu amesoma vitabu 107. Ukifuatilia idadi ya vitabu wanavyosoma ‘wenzetu’ kwenye nchi zilizoendelea utastaajabu. Katika mtandao wa ‘Quora’, rafiki Sedrick Giddings amesoma vitabu 60, Dewan Sacha anasoma kurasa 200 -300 kwa siku, Lim Ming Dao anasoma vitabu viwili kila siku kwa siku 100 za mwaka, sawa na vitabu 200.

Lakini inategemea zaidi na aina ya vitabu unavyosoma, ukubwa wake na shughuli zako za kila siku. Jambo la msingi la kufahamu hapa sio kusoma vitabu vingi, jambo la msingi ni kuwa na utamaduni wa kujisomea. Narudia, jambo la msingi sio kusoma vitabu vingi, bali kuwa na utamaduni wa kujisomea. Kwani unashindana na nani? Kusoma vitabu vingi kuna faida yake kubwa tu, lakini unaweza kusoma vitabu vichache kwa makusudi maalum ukafaidika pia. Kwa mfano, muandishi wa vitabu anahitaji kusoma mengi kuliko anachokiandika. Kwa hiyo, huyo ana sababu ya kusoma sana, hususani mambo yanayohusu kile anachoandika. Ndio maana Yeriko Nyerere muda wote yupo na vitabu na nyaraka za ki-intelligensia na za kisiasa, kwakuwa ndio shughuli yake. Viongozi wa kisiasa, kidini nk wana sababu ya kusoma sana kwakuwa wanakutana na nyumati za watu wa khaiba tofauti kila siku. Na kwa kuwa wanasikilizwa sana na watu wa taaluma zote wana sababu ya kujua mambo mengi ili kujua nini cha kuongea na nini sio cha kuongea kwa wakati husika. Kiongozi asiyejisomea kila siku ataongea vituko tu. Hata kujenga hoja hawezi. Na mtu anayependa kushinda, lakini hawezi kushinda kwa hoja, atatumia upanga.

Kwahiyo kujisomea kuna umuhimu mkubwa sana. Watu wengine wana vitabu vyao maalum, kama ni biashara, riwaya, hamasa, ‘lifestyle’ nk. Wengine wanasoma sana mambo yanayohsu taaluma zao; madaktari, mainjinia, wanasheria, wana-theolojia, wahasibu, walimu, nk. Wanaji-update ili kujiongezea ushindani (competence) kwenye kuajiriwa au kujiajiri.

Kusoma vitabu vingi.
Kwanza lazima uwe na utamaduni wa kujisomea, iwe sehemu ya maisha yako. Kama ilivyo kwa mazoezi ya mwili, kunywa maziwa, au kunywa maji ya kutosha kwa siku, ni utamaduni unaotakiwa kujijengea ili usifanye kwa kujilazimisha, au kwa kulazimishwa. Anza na vitabu vidogo vidogo, au vijarida vinavyokuvutia. Ukisoma kitu kinachokuvutia utatamani kuendelea kukisoma na utamaliza bila kuchoka. Kwa hiyo unaweza kujikusanyia vitabu vidogo unavyopenda kwa kuanzia. Ndani ya hivyo vitabu unaweza kukutana na mambo mengine ambayo utatamani kuyajua zaidi. Kwa hiyo utatafuta vitabu vingine zaidi. Hapo utakuwa unajijengea taratibu utamaduni wa kujisomea. Baada ya muda utaona unatamani tu kuendelea kusoma. Ukipita muda hujasoma unakumbuka oooh, I have something to read.

Pili, muda wa kusoma. Asubuhi kabla ya kufanya jambo lolote, unaweza kushika simu yako ukafungua kitabu na kuanza kusoma angalau kwa dakika 30 hadi 60. Hapo itakuhitaji kuamka mapema. Kuna watu ni wavivu kuamka kwa sababu ya kuchoka. Kuna siri ndogo tu hapa; Kuwa mtu wa mazoezi hata mepesi, kunywa maji mengi, lala mapema; Ukifanya hivyo halafu ukapata tabu kuamka, tafuta daktari. Muda mwingine mzuri wa kusoma ni jioni kabla ya kulala, wakati unavuta usingizi. Ila sasa, inategemea na mambo mengine. Unaweza pia kusoma ukiwa kwenye gari (kama huendeshi), wakati wa ‘breakfast’ au wakati wa lunch kama mazingira yanaruhusu. Weekend, unaweza kutenga muda zaidi wa kusoma, au ukiwa safarini. Watu wengine husoma sana wakati wakiwa likizo ili kufidia muda waliokosa wanapokuwa wamebanwa na kazi.

Tatu, ni material unayotumia. Kuna baadhi ya vitabu ni vyeupe sana kiasi vinaharibu macho, au vingine vina maandishi madogo sana kiasi cha kuharibu macho na kuchoka mapema. Ukishindwa kusoma hapo huna sababu ya kujilaumu. Ni kosa la mchapishaji. Kwa wanaotumia simu au pads, au laptop ni vema wakatumia ‘application’ ambazo ni rafiki kwa kusomea, kwa maana ya uwezo wa kubeba vitabu vingi na kwa mpangilio mzuri, kukuza maandishi ili msomaji aamue ukubwa wa maandishi, uwezo wa kusoma kwa kusikiliza sauti (audio book), rangi ya pages na maandishi ili msomaji aweze kuamua kubadili rangi inayomvutia. Binafsi natumia Universal Book Reader (UB reader) ambayo ina sifa hizo nilizotaja.

Mbinu zingine ni kusoma mahali penye utulivu, au wengine wanasoma huku wanasikiliza music kwa earphone, ili kuepuka usumbufu unaoweza kukuharibia ‘mood’.
Kusoma, kama alivyosema Prof. Ben Carson kuna fanya ubongo uwake. Prof. Ben anasema, ‘Our brain is not a vessel to be filled, but a fire to be ignited’. (Bongo zetu sio chombo kinachoweza kujaa, bali ni moto unaotakiwa kuwaka). Na kama ilivyo kwa moto unapohitaji mafuta/fuel kwa ajili ya kuwaka zaidi, na ubongo unahitaji vitabu. Prof. Ben Carson ndiye daktari wa kwanza kufanikisha (yeye na timu yake) kutengenisha watoto wa kijerumani walioungana vichwa. Vitabu vyake ‘Think Big’ na ‘The Gifted hands’ ni vizuri kwa mtu anayeanza kusoma vitabu.

The mind needs book as the sword needs a whetstone, akili inahitaji vitabu kama upanga unavyohitaji jiwe la kunolea.

Mtu anayejua kusoma lakini hajisomei, hana tofauti na asiyejua kusoma. Wote wanakosa kitu kilekile; Mark Twain.

ANGALIZO
Kusoma sana kuna madhara yake pia. Unaweza kuangukia kwenye tabia ya ugoigoi ya kufikiria sana bila kutenda. Kama alivyosema Albert Einstein, ‘Be careful of too much reading, you can fall into a lazy habit of thinking”. Kwamba unaposoma mambo mengi, uwezo wa kufikiri unaongezeka sana, unakuwa na taarifa nyingi sana, na maneno mengi ya kuzungumza (sio lazima uzungumze). Kwa hiyo inaweza kukupelekea kuwa mtu wa kufikiri sana kiasi cha kupoteza muda wa kutenda. Kadiri unavyosoma sana, unajua mambo mengi sana, na ukijua mambo mengi sana unagudundua kuwa hujui mambo mengi sana, na kwa hiyo unaweza kuwa mtu wa kutafuta kujua muda wote, bila kutendea kazi yale ambayo tayari unayajua.

Hata hivyo, kujisomea kuna faida kubwa sana kuliko kinyume chake.

Nawatakia usomaji mwema! Vitabu 100+ mwaka huu au sio?
 

Attachments

  • images (3).jpg
    images (3).jpg
    18.3 KB · Views: 113
asante sana ndugu uzi umenigusa sana kwani mimi mwaka ulopita nimesoma vitabu 97 tu(ispiration books).bila kusahau vile vya bwana paul coelho aisee ni burudani sana.
vilevile umenigusa hasa katika the gifted hand na think big hapa ndipo utamu wa vitabu ulipo aisee from zero to hero!!!
mkuu nikushukuru sana kwa kunipatia website mpya ya vitabu(unversal book reader) nitaitumia ipasavyo.bila kusahau pongezi kwangu kwa kushinda tuzo ya best fiction books reader award katika mtandao wa goodreads.com.
nikuache tu na qoute ya dr.carson
"honest people they thinking big while dishonest people they are small in minded"
asante sana.
 
QUOTE

Mtu anayejua kusoma lakini hajisomei, hana tofauti na asiyejua kusoma. Wote wanakosa kitu kilekile; Mark Twain.

Mkuu hapo utakua unamsema mkuu wa mkoa wa jiji fulani...naskia mara ya mwisho yeye kusoma kitabu ni alipomaliza chuo.
 
QUOTE

Mtu anayejua kusoma lakini hajisomei, hana tofauti na asiyejua kusoma. Wote wanakosa kitu kilekile; Mark Twain.

Mkuu hapo utakua unamsema mkuu wa mkoa wa jiji fulani...naskia mara ya mwisho yeye kusoma kitabu ni alipomaliza chuo.
Kabla hujamuwazia mwingine kwa nini usijichunguze na kujisemea wewe! Hata kama ni kweli hasomi au hana utamaduni wa kujisomea haitakuongezea chochote mkuu! Na kwa comment yako, utakuwa hujamsaidia chochote zaidi ya kudhihirisha kiwango cha chuki na majungu ndani yako!
Nimejisikia tu kusema, si kwa nia mbaya!
By the way uzi mzuri sana huu!!
Asante sana mwandishi!
 
Mimi mvivu sana wa kusoma. Msaada mnafanyaje wenzangu kusoma vitabu 10 kwa mwaka?

Mimi hata kimoja kwa mwaka sijawahi.

Ila nataka kubadilika...
 
Mimi mvivu sana wa kusoma. Msaada mnafanyaje wenzangu kusoma vitabu 10 kwa mwaka?

Mimi hata kimoja kwa mwaka sijawahi.

Ila nataka kubadilika...
Rudia kusoma alichokiandika aliyepost kuna vitu vya msingi kavizungumza hapo!
 
Hata mada yenyewe sijaisoma yote.

Nina uvivu mwingi yaani nahitaji msaada ndugu chopeko

Hahahaha ndo maana nimeshtuka! As long as unajua kusoma hata maneno machache basi huna haja ya kukata tamaa, unaweza kusoma hayo mengi yaliyokusanywa na kuwa kitabu. Jiwekee malengo ya kusoma hata maneno 50 kwa kuanzia kila siku na kila baada ya muda labda week hivi unayadouble! Namaanisha kama umeanza na maneno 50 kila siku then week ijayo fanya 100 kila siku na week itakayofuata soma 200 kila siku! Endelea hivyo hivyo utakuja kujishangaa mwenyewe.
Naogopa kuandika mengi yasije kukushinda kuyasoma mkuu (Natania tuu)!!!
Karibu sana!
 
Tatizo la watu wengi husoma sana vitabu ila wanaishia kupata faida ya kujua mengi ila upeo wao unabaki pale pale.
 
Shukrani sana mkuu kwa huu uzi. Mi binafsi nimeanza na vitabu vya Dr. Myles Munroe.
 
Back
Top Bottom