Kusoma UDSM ni dhamana

Hongera Mkuu, Hivi unadhani Udsm ingekuwa Jobeg ingekuwa sawa na chuo gani?
Kuna ndugu yangu kasoma China mambo ya IT, siku moja nikawakutanisha na jamaa yangu flani kapiga UDSM mambo hayo. Nilicho gundua kila mtu ana mnyonge wake man maana chalii alionekana mtupu mbaya akaambiwa " dogo uwe unakuja niku_ brush haujui kitu". Mimi naingia tena mzumbe kujazia madude.
 
Dogo mmoja alipomaliza form six akamweleza mzazi wake amechaguliwa chuo flan tofauti na udsm. Hahahaha mzazi akamwambia mwanae hongera mwanangu na ukazane kusoma hadi utakuja fika udsm


Mkuu nimecheka sana. Sasa aliona mwanae anaenda wapi?
 


Kweli Mkuu, Kila boss ana boss wake
 


Upo sahihi kabisa Kiongozi. Ila usisahau kuwa aliyesomea MUHAS na Ardhi hujiona ni miongoni mwa Wana-udsm kimtazamo.Tafuta wasomi waliosomea vyuo hivyo uone nikisemacho
 
Waliosoma UDSM ndo wametufikisha hapa tulipo, kuanzia viongozi na wafanyakazi wengi wamesoma hapo na hawajaonesha kulipeleka taifa mbele. So sioni mchango wowote wa chuo hicho kikongwe


Wamebaki majivuno unaweza kusema kuwa huko chuoni walisomea shahada ya majivuno
 


Mkuu nenda pole. Mtu wa hivyo alisoma chuo kingine kutokana na kuwa hakuna kozi husika lakini si kukosa kigezo. Bado hujajua tofauti. Huwezi ona mtu anaumia kwenye mada hii endapo anaufaulu mzuri darasani au alisomea nje ya nchi. Wengi watakaokuja na povu humu ni wale wenye vimaksi vya foleni
 


Mkuu shida inatokea ni kuwa Vyuo vingine huchagua wanafunzi wenye ufaulu wa chini sana. Mfano DD wakati Udsm huchagua wenye ufaulu wakushangaza. Cha msingi serikali iboreshe elimu kwenye shule huku chini ili wanaopata maksi za juu wawe wengi angalau vyuo vingne vipate hata one za 3
 
Ukweli ndio huo.....

Nimesoma chuo cha uhasibu Arusha vyuo vyote vya ifm, mzumbe, tia na vingine(ukiachana na vya mtaani kama teku, sauti, tumaini, st joseph, st john, Jordan, n.k) naona tupo kundi moja tu , ,udsm ni level nyingine....Aisee tusijifanye hatumuoni tembo ambae yupo chumbani....Udsm ni baba lao

Lazima niende pale kusafisha nyota nichukue masters inayohusiana na uhasibu panapo majaliwa.
 
brot
duuh mkuu mimi pia nian degree sina ufahulu huo unaoutaja pia sijasoma UD so what does that mean
 
Nilitegemea ungeleta uzi unaoelezea ujuzi ulioupata chuoni hapo na jinsi unavyoutumia sasa kuleta matokeo chanya.Porojo hizo unazoleta ni sawa na bure tu.
Safari unayo wewe Mkuu Usiingize wengine kwenye safari yako
 
Ukweli mtupu
 
Nachojua kwenye interview nilifumua udsm wote, SUA nilikuwepo peke angu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…