Kusoma UDSM ni dhamana

Kusoma UDSM ni dhamana

Hongera Mkuu, Hivi unadhani Udsm ingekuwa Jobeg ingekuwa sawa na chuo gani?
Kuna ndugu yangu kasoma China mambo ya IT, siku moja nikawakutanisha na jamaa yangu flani kapiga UDSM mambo hayo. Nilicho gundua kila mtu ana mnyonge wake man maana chalii alionekana mtupu mbaya akaambiwa " dogo uwe unakuja niku_ brush haujui kitu". Mimi naingia tena mzumbe kujazia madude.
 
Dogo mmoja alipomaliza form six akamweleza mzazi wake amechaguliwa chuo flan tofauti na udsm. Hahahaha mzazi akamwambia mwanae hongera mwanangu na ukazane kusoma hadi utakuja fika udsm


Mkuu nimecheka sana. Sasa aliona mwanae anaenda wapi?
 
Kuna ndugu yangu kasoma China mambo ya IT, siku moja nikawakutanisha na jamaa yangu flani kapiga UDSM mambo hayo. Nilicho gundua kila mtu ana mnyonge wake man maana chalii alionekana mtupu mbaya akaambiwa " dogo uwe unakuja niku_ brush haujui kitu". Mimi naingia tena mzumbe kujazia madude.


Kweli Mkuu, Kila boss ana boss wake
 
Nafikiri ni kulingana na kada husika...
Mfano Masuala ya Sheria, Biashara,Economics,Siasa...UDSM iko vizuri.....upande wa Engineering na kada kama hizo.wana wapinzani wazuri tu.....
Masuala Ya Utabibu ...MUHAS
Masuala ya Ardhi na Biashara zote za ardhi...etc ARU
Kilimo....SUA
Etc....
Nafikiri si sawa kugeneralize..lkn pia umashuhuri wa UDSM unatokana na historia husika kama state university lkn pia baadhi ya kada zake zinalenda zaidi na zinatoa watawala , wanasiasa etc..watu wa-public..kelele nyingi sana ..
Wakati vyuo vingine vinatoa watu watendaji mfani Madaktari....Watu kutoka Ardhi,SUA..etc watu kutoka hivi vyuo kwa asili ya taaluma zao huwezi wakuta kwenye majukwaa..na hata kutambua kuwa wamesoma kitu fulani ni ngumu mpaka siku uhitaji msaada wake..
Lkn pia kwa miaka ya sasa na jinsi inavyoenda hali iko tofauti sana kuna vyuo vingi sana ambavyo sasa vinatoa wataalumu wa taaluma za watu wa majukwaa na kypiga kelele na kutambulika mfano UDOM,SAUT etc..
Yajayo yanafurahisha


Upo sahihi kabisa Kiongozi. Ila usisahau kuwa aliyesomea MUHAS na Ardhi hujiona ni miongoni mwa Wana-udsm kimtazamo.Tafuta wasomi waliosomea vyuo hivyo uone nikisemacho
 
Waliosoma UDSM ndo wametufikisha hapa tulipo, kuanzia viongozi na wafanyakazi wengi wamesoma hapo na hawajaonesha kulipeleka taifa mbele. So sioni mchango wowote wa chuo hicho kikongwe


Wamebaki majivuno unaweza kusema kuwa huko chuoni walisomea shahada ya majivuno
 
Kwa style hii ya maisha watanzania tutatawalia na wajinga hadi akili itukae sawa. Yaan mtu anasoma sociology kisa udsm anajilinganisha na mtu anaesoma DIT elictrical? Yaan mtu kasoma HKL uko advance anajilinganisha na PCM ambae alipata matokeo mazur na kuamua kusoma kozi nyingne anayoipenda yeye amabayo haipo udsm? Kweli ujinga mzigo


Mkuu nenda pole. Mtu wa hivyo alisoma chuo kingine kutokana na kuwa hakuna kozi husika lakini si kukosa kigezo. Bado hujajua tofauti. Huwezi ona mtu anaumia kwenye mada hii endapo anaufaulu mzuri darasani au alisomea nje ya nchi. Wengi watakaokuja na povu humu ni wale wenye vimaksi vya foleni
 
nonsense tunachofanya nikinyume na tunachotakiwa kufanya serikali inavyuo vikuu kibao tuu badala ya kuboresha hali za hivyo vyuo vyake ktk kila nyanja imekaaa ikikikweza UDSM whats about UDOM SUA MZUMBE eti hadi mkuu wa nchi nae hiki ndo chuo bora wahitimu mchague hiki sasa tufunge vyuo vingine maana mnatuambia havitoi elimu sasa vya nini


Mkuu shida inatokea ni kuwa Vyuo vingine huchagua wanafunzi wenye ufaulu wa chini sana. Mfano DD wakati Udsm huchagua wenye ufaulu wakushangaza. Cha msingi serikali iboreshe elimu kwenye shule huku chini ili wanaopata maksi za juu wawe wengi angalau vyuo vingne vipate hata one za 3
 
Ukweli ndio huo.....

Nimesoma chuo cha uhasibu Arusha vyuo vyote vya ifm, mzumbe, tia na vingine(ukiachana na vya mtaani kama teku, sauti, tumaini, st joseph, st john, Jordan, n.k) naona tupo kundi moja tu , ,udsm ni level nyingine....Aisee tusijifanye hatumuoni tembo ambae yupo chumbani....Udsm ni baba lao

Lazima niende pale kusafisha nyota nichukue masters inayohusiana na uhasibu panapo majaliwa.
 
brot
Mkuu shida inatokea ni kuwa Vyuo vingine huchagua wanafunzi wenye ufaulu wa chini sana. Mfano DD wakati Udsm huchagua wenye ufaulu wakushangaza. Cha msingi serikali iboreshe elimu kwenye shule huku chini ili wanaopata maksi za juu wawe wengi angalau vyuo vingne vipate hata one za 3
duuh mkuu mimi pia nian degree sina ufahulu huo unaoutaja pia sijasoma UD so what does that mean
 
Nilitegemea ungeleta uzi unaoelezea ujuzi ulioupata chuoni hapo na jinsi unavyoutumia sasa kuleta matokeo chanya.Porojo hizo unazoleta ni sawa na bure tu.
Safari unayo wewe Mkuu Usiingize wengine kwenye safari yako
 
Ugonile bandugu!

Kusomea udsm ni zaidi ya watu wafikiriavyo katika taifa hili. Kusomea Udsm ni moja tiketi ya heshima katika taifa letu hasa kwenye ishu za elimu. Maisha ya mtu aliyesomea Udsm huwa tofauti kwa kiasi fulani na waliosomea Vyuo vingine. Sio kwenye siasa, uchumi, mahusiano, na mambo mingine kusomea Udsm hukupa ahueni ya maisha kiasi fulani.

Kwenye Mahusiano ya mapenzi ambayo huzalisha ndoa. Mwanaume aliyesomea Udsm angalau hupewa heshima kulingana na chuo alichotokea. Mwanamke hujivunia mwanaume aliyesomea Udsm kwa huonekana anaakili za shule kumbe wakati mwingine ni popoma. Mwanamke aliyesomea Udsm linapokuja suala la elimu humuona mume wake anamapungufu endapo hakusoma katika chuo tajwa. Watoto hujivunia kuwa na Baba aliyesoma Udsm kuliko vyuo vingine.

Ishu ya kazi, wahitimu wa Udsm hufurahia sana kipindi cha usaili kwani hujiona bora kuliko wengine. Hakuna maelezo matamu yanayomfanya mhitimu wa Udsm ajione atachaguliwa kwenye kazi husika kama wakati akijitambulisha wasifu wake wa elimu. Hapa utakuta moyo huwa mwepesi na faraja kiasi. Hilo linafurahisha sana hata kwa waajiri hasa waliotoka kwenye chuo hicho. Ni kama kuna kaubaguzi fulani hvi. Mwana Udsm awapo kazini huhakikisha anafanya kazi kwa ufanisi ili asionekane bongolala. Na hakuna aibu kama mwana udsm akiboronga looh! hiyo itakuwa habari yenye kushangaza sana na ya aibu. Kutokana na sifa ya chuo.

Undugu, Wana Udsm hupendana na kutafutana popote walipo. Usishangae mtu akifika kituo kipya cha kazi kuulizia/kuulizwa wewe umetoka chuo gani. Hapo ndipo mtu hujitutumua; nimesomea Udsm. Na kama hajasomea chuo hicho uso wake hunyong'onyea na usipokuwa makini anaweza kukutukana. Wa-Udsm wakikutana basi huunda urafiki na kuanza mishe za kazi na maisha.

Mitandao ya kijamii, Ukitaka kujua jambo fulani linapewa heshima basi angalia mtazamo wa tabaka la chini kuhusu jambo hilo. Ingia Facebook, 90% ya watumiaji kutoka Tanzania wamesomea Udsm. Hii ni moja ya mambo yanayoonyesha chuo hiki kinaheshimika na ni ndoto ya vijana wengi. Usishangae hata baadhi ya watu humu JF ambao wameandika huko FB kuwa wamesomea Udsm kumbe hawakusomea.

Majukwaa ya Siasa, Wahitimu wa Udsm ndio pekee wenye uthubutu na sasa wanakaribia kupata mamlaka ya kujitambulisha kila mara. Bungeni napo wenye kusikika wakipiga tambo ni hao hao. Utasikia mtu akisema: Nilipokuwa Udsm ndugu mheshimiwa Spika nilikuwa mwenyekiti sijui wa nini. Yaani basi tuu.

Nimalizie kusema kuwa Kusoma Udsm ni dhamana hivyo wahitimu mujidhatiti.
Sikutaka sifa niliamua kusoma chuo cha "TUYAJENGE SACCOS COLLEGE"

Povu linaruhusiwa
Ukweli mtupu
 
Nachojua kwenye interview nilifumua udsm wote, SUA nilikuwepo peke angu.
 
Back
Top Bottom