Kusoma UDSM ni dhamana

Kusoma UDSM ni dhamana

Hahahah nilijua utasema hayo tu
mmekuwa mkijisifia kucreate ARU
Ila mtoto ashakuwa na anajitegemea sasa
It's 11 years now
Narudi kuwatrain watoto wa ud kuprove tu ARU is the best
Nikimaliza narud nyumban kubeba manyota hahahah


Uje kwa Baba yako upate urithi wako. Hizo nyingne ni mboyoyo tuu
 
Ningekuwa Mnyakyusa ningejiua muda sana. Sina uhusiano wowote na jamii hiyo. Sina hata aliyewahi kuwa rafiki kutoka jamii tajwa hapo
Ni much know sn, ukitaka kuwaenjoy we jifanye fala, me najitambulishaga kwao km mhehe au Msafwa basi atakudharau. Wasukuma nawapenda are so humble, imagine wanyakyusa, wachaga au wahaya wangekuwa wengi km wasukuma hapa nchini ingekuwaje!
 
Ugonile bandugu!

Kusomea udsm ni zaidi ya watu wafikiriavyo katika taifa hili. Kusomea Udsm ni moja tiketi ya heshima katika taifa letu hasa kwenye ishu za elimu. Maisha ya mtu aliyesomea Udsm huwa tofauti kwa kiasi fulani na waliosomea Vyuo vingine. Sio kwenye siasa, uchumi, mahusiano, na mambo mingine kusomea Udsm hukupa ahueni ya maisha kiasi fulani.

Kwenye Mahusiano ya mapenzi ambayo huzalisha ndoa. Mwanaume aliyesomea Udsm angalau hupewa heshima kulingana na chuo alichotokea. Mwanamke hujivunia mwanaume aliyesomea Udsm kwa huonekana anaakili za shule kumbe wakati mwingine ni popoma. Mwanamke aliyesomea Udsm linapokuja suala la elimu humuona mume wake anamapungufu endapo hakusoma katika chuo tajwa. Watoto hujivunia kuwa na Baba aliyesoma Udsm kuliko vyuo vingine.

Ishu ya kazi, wahitimu wa Udsm hufurahia sana kipindi cha usaili kwani hujiona bora kuliko wengine. Hakuna maelezo matamu yanayomfanya mhitimu wa Udsm ajione atachaguliwa kwenye kazi husika kama wakati akijitambulisha wasifu wake wa elimu. Hapa utakuta moyo huwa mwepesi na faraja kiasi. Hilo linafurahisha sana hata kwa waajiri hasa waliotoka kwenye chuo hicho. Ni kama kuna kaubaguzi fulani hvi. Mwana Udsm awapo kazini huhakikisha anafanya kazi kwa ufanisi ili asionekane bongolala. Na hakuna aibu kama mwana udsm akiboronga looh! hiyo itakuwa habari yenye kushangaza sana na ya aibu. Kutokana na sifa ya chuo.

Undugu, Wana Udsm hupendana na kutafutana popote walipo. Usishangae mtu akifika kituo kipya cha kazi kuulizia/kuulizwa wewe umetoka chuo gani. Hapo ndipo mtu hujitutumua; nimesomea Udsm. Na kama hajasomea chuo hicho uso wake hunyong'onyea na usipokuwa makini anaweza kukutukana. Wa-Udsm wakikutana basi huunda urafiki na kuanza mishe za kazi na maisha.

Mitandao ya kijamii, Ukitaka kujua jambo fulani linapewa heshima basi angalia mtazamo wa tabaka la chini kuhusu jambo hilo. Ingia Facebook, 90% ya watumiaji kutoka Tanzania wamesomea Udsm. Hii ni moja ya mambo yanayoonyesha chuo hiki kinaheshimika na ni ndoto ya vijana wengi. Usishangae hata baadhi ya watu humu JF ambao wameandika huko FB kuwa wamesomea Udsm kumbe hawakusomea.

Majukwaa ya Siasa, Wahitimu wa Udsm ndio pekee wenye uthubutu na sasa wanakaribia kupata mamlaka ya kujitambulisha kila mara. Bungeni napo wenye kusikika wakipiga tambo ni hao hao. Utasikia mtu akisema: Nilipokuwa Udsm ndugu mheshimiwa Spika nilikuwa mwenyekiti sijui wa nini. Yaani basi tuu.

Nimalizie kusema kuwa Kusoma Udsm ni dhamana hivyo wahitimu mujidhatiti.
Sikutaka sifa niliamua kusoma chuo cha "TUYAJENGE SACCOS COLLEGE"

Povu linaruhusiwa

Nadhani UDSM ni national university (ingawa siyo rasmi) kama ilivyo Muhimbili ambayo ni national hospital....Lakini pamoja na umaarufu wa UDSM mambo kwa sasa siyo mazuri sana...products zake za sasa siyo nzuri sana..vijana wa kizazi hiki hawapendi kusoma au kuchimbua issues...wanajielegeza mno kimasomo. ingawa ni kweli ikilinganishwa na vyuo vingine nchini UDSM bado kipo juu kwa mbali
 
Back
Top Bottom