Kusitishwa ghafla kwa ujenzi wa Bomba la Mafuta Hoima - Tanga: Wafanyakazi wahaha, Museveni na Magufuli kuteta

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Wafanyakazi Mradi Bomba la Mafuta wapigania haki zao

Baada ya Kampuni kubwa ya mafuta ya TOTAL kuamua kusitisha shughuli za kutandaza bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania, wafanyakazi Watanzania wameanza kuhaha kupigania haki zao.

Uamuzi wa kusitisha ghafla mradi huo ulitolewa Ijumaa iliyopita na Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Martine Tiffan.

Akizungumza na wafanyakazi hao jijini Dar es Salaam, Martine aliwaeleza uamuzi huo wa ghafla kuwa umetokana na sababu nje iliyo nje ya uwezo wao.

Kiongozi huyo aliyewasili Alhamisi iliyopita kutoka Paris, Ufaransa na kesho yake kuitisha kikao cha dharura, alisema, "Tunasitisha shughuli zetu kuanzia sasa na wafanyakazi wote wanatakiwa kuondoka mara moja."

Baada ya maneno hayo, kiongozi huyo alifunga kikao na kuacha wafanyakazi hao wakiwa wametaharuki, wamepigwa 'bumbuwazi.'

Mradi huo hadi Jana ulikuwa na wafanyakazi Watanzania takribani 85.

Taarifa za uhakika ambazo ninazo ni kwamba wafanyakazi hao walikutana Jumatatu ya wiki hii kujadili mustakabali wao, hasa malipo yao na namna ya kuondoka kazini.

Katika kikao chao, waligundua kuwepo kwa malipo kiduchu katika mikataba yao ya ajira, hivyo kupanga mikakati ya namna ya kuhakikisha wanapata stahiki yao.

"Yaani tunaondolewa ghafla na bado waajiri wetu wanapanga kutulipa mafao madogo mno," alidokeza mmoja wafanyakazi hao.

Mikataba ya wafanyakazi hao, ambayo ni ya mwaka mmoja mmoja, haina vifungu vya kuwaneemesha zaidi kama ilivyo ya wafanyakazi wengine wa sekta ya mafuta na gesi.

Mikataba hiyo inaonyesha kuwa wanatakiwa kulipwa mshahara wa mwezi mmoja tu na malimbikizo ya siku za likizo basi, hali ambayo wao wanadhani ni kidogo, hasa ikizingatiwa kupewa taarifa ghafla.

Habari kutoka ndani ya mradi huo zinaeleza kuwa Total wala mradi huo siyo waajiri wa moja kwa moja wa wafanyakazi hao, isipokuwa wameajiriwa na wakandarasi; wengi kutoka Uganda na Uingereza.

Magufuli, Museveni kuteta kuunusuru Mradi wa Bomba la Mafuta

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda anatua leo jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo ya dharura na Rais John Pombe Mafuguli.

Pamoja na mambo mengine, ikiwamo kuhudhuria mkutano wa uwekezaji kati ya nchi mbili (Tanzania na Uganda), viongozi hao watapata wasaa wa kujadili njia za kunusuru mradi huo mkubwa.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa viongozi hao watakutana Ikulu iliyopo Magogoni, Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo hayo.
 
Kipindi wanasaini mikataba ya kazi kabla ya kuajiriwa walikuwa hawajui kama ujira ni mdogo?
.
Walipwe mafao makubwa kwa kazi gani waliyofanya? Kupima pima miamba barabarani ambako bomba litapita kazi waliyoifanya kwa wiki moja tu?
 
Duh.....nilisoma.pahala kenya wanapakia meli yao ya kwanza ya mafuta waliyochimba wao. Inawezekana kuna conflict ya kisoko au ya wanufaika.lakini pia lazima kuna maagizo ya kisiasa kutukomesha. Total haiwez kufanya tofauti na matakwa ya raisi wa ufaransa.
 
Kipindi wanasaini mikataba ya kazi kabla ya kuajiriwa walikuwa hawajui kama ujira ni mdogo?
.
Walipwe mafao makubwa kwa kazi gani waliyofanya? Kupima pima miamba barabarani ambako bomba litapita kazi waliyoifanya kwa wiki moja tu?
Una roho ya kimaskini sana, tena yenye nyongo nyingi zaidi ya damu.

Kazi yeyote, ukiondoa mshahara huwa inajenga pia matarajio. Kumsitisha mtu kazi ghafla maana yake unaua matarajio yake pia. Huko kwa wenzetu West Africa, ukifanya maamuzi kama haya si ajabu ukalazimika kuwalipa wafanyakazi up to 25 months salary. Sasa kwa kuwa akili zenu zimekaa kiLUMUMBA LUMUMBA na mmepewa tafsiri mpya ya uzalendo basi mnadhani maisha principal yake ya kwanza ni KUJIKOMBAKOMBA na kuabudu binadamu.

Utafutie ubongo wako ukombozi kabla haujafa kabisa.
 
Duh, inauma kama tutakosa dili hili 😩😩, kwani shida nini, mradi ulishafanyiwa evaluation, pro and cons, and utekelezaji kuanza, ghafla tu sababu za nje ya uwezo? Au wamegundua Uganda hamna tena mafuta?
 
Back
Top Bottom