Kusingiziwa mtoto ambaye sio wako

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Katika pitapita zetu kwenye harakati za kumwagilia moyo, nikipita kwenye bar fulani nikawa nimemuelewa muhudumu mmoja, tukaelewana tukabadilishana namba, nikamuomba kulala naye usiku huo akakubali kwa mapatano ya kumlipa posho.

Muda ulipofika tukaenda kufanya yetu. Tulipofika chumbani alipovua, niliona dalili kama ana mimba maana alikua na tumbo kubwa na alikua anatema mate kila mala. Japokua nilikua na pombe kichwani lakini niliweza kutambua hilo.

Tumefanya yetu pakakucha, asubuhi nikampa chake kila mtu akaendelea na ratiba za maisha yake.
Baada ya miezi 6 iliingia namba mpya ikinipigia kwenye simu yangu, kupokea nikaskia sauti ya kike inaniuliza kuwa, “Lini utakuja kumuona mwanao?“

Nilipingwa na butwaa nikamuulize “Wewe ni nani?“ Akajitambulisha kiundani zaidi nikawa nimemkubuka, nikaamuliza, “Unataka nije kumuona mwanangu yupi?” Akasema hujui kama siku tupolala wote ulinipa mimba na tayari nimeshajifungua mtoto wa kike?

Nlistaajabu sana nikawa nimemkatalia kuwa mimi siwezi kuwa baba wa huyo mtoto maana hata siku hiyo tunalala wote ulikuwa una dalili zote za kuwa na mimba tayari, mawasliano yakawa yameishia hapo.

Baada ya week 1 tangu anipigie kuhusu taarifa ya kunibambikia mimba, ghafla nikapigiwa na namba Afisa Ustawi wa Jamii kuwa nahitajika ofisini. Nikaenda kusikiliza, nikahojiwa kama namfahamu huyo dada nikakubali kuwa namfahamu lakini nilipinga kuwa huyo mtoto sio wangu.

Afisa Ustawi akanishauri sana kuhusu matumizi madogo madogo ya mtoto nikakubari kuwa ntakuwa natuma pesa ya matumizi madogo madogo.

Kadri siku zinavyozidi kwenda naona kama inazidi kuwa kero, yule dada mhudumu wa bar anakuwa ananipigia mpaka saa 5 usiku, nikiwa nimelala anatuma mesej za ajabu, anakuja ofsini ninapofanyia kazi bila taarifa, yaani inakuwa ni vurugu.

Na nikiamuaria yule mtoto na muda tuliosex na mama yake na umri alionao yule mtoto ni tofauti kabisa, nahisi nimepigwa na kitu kizito kwasababu hata kusema kufanana hajafanana na mimi hata kidogo.

Naombeni ushauri wenu wana JF, nifanye nini ili kuondokana na hili tatizo la huyu dada mhuni?
 
Hao madem wa kuokoteza wasijue unakofanyia kazi aisee.. I mean hauko committed na mtu, why ajue vitu vingi kukuhusu?

Kwanza hata hawatakiwi kujua unapoishi.

Kama mlisex then after 6 month akwambie kajifungua, huyo mtoto ni njiti au?
 
Kuna uzi unatukanya juu ya wanawake washamba, wakuu nadhani tupate mfano hapa.

Ila Bro anza na kadi ya clinic, Kadi ya mtoto ndio uende kwenye DNA. Ukipewa kadi za huyo dada zichukue nenda kahakiki na kadi ya hospitali lazima kuna kamchanganyo utakapata tu. Ukikosa nenda kwa DNA sasa.

Ukimaliza hapo sasa nitakushauri namna ya kwenda mpeleka Mahakamani, hawezi taka kujinufaisha kirahisi rahisi hivyo akaachwa.
 
Asante sana kwa ushauri , nitaufanyia kazi huu ushauri
 
Nikiwahi kumwambia Afsa ustawi kuhusu kuomba appointment ya DNA TEST , baada ya siku ya DNA TEST kufika ili twende tukatoe samples , Afsa ustawi akawa amepata emergency ya kikazi 🥹.
Bila DNA huyo mwanamke atakutesa sana na inaonekana wanalengo moja na huyo jamaa wa ustawi wa jamii.
Kwenye kutoa hela ya matumizi ya mtoto haupo peke yako, mpo wengi na hapo ana vyeti vya mtoto zaidi ya kimoja.
Kama alikuuzia K, alishawauzia wangapi? Huyo mwanamke jambazi
 
Nikiwahi kumwambia Afsa ustawi kuhusu kuomba appointment ya DNA TEST , baada ya siku ya DNA TEST kufika ili twende tukatoe samples , Afsa ustawi akawa amepata emergency ya kikazi 🥹.
Ukitaka kujua kuwa umepigwa na kitu kizito kichwani mwambie hivi
Unataka ukamtambulishe huyo mtoto kwa mama yako mzazi, dada zako, shangazi zako na ndugu zako wamuone. Hawezi kukubali, chenga zinakua nyingi sana
 
Eti hata kufanana hajafanana na mimi ulitaka mfanane na unakana sio wako na amezaliwa akiwa na miezi 6

Yan me nmesex nae, Ndan ya miezi sita mtoto amezaliwa na ameshakua , tulipokutana alijua nmelewa na nlkua najielewa kabsa japo yeye ndo alinihudumia bia na nlizilipia zote, tulipofika chumban alipovua nguo nlioa tumbo kubwa la mimba na kuna baadhi ya style alikua hawezi kukaa nikimgeuza anakua mvivu, naamini nimepigwa na kitu kizito. Nasubiri mwisho wa mwezi huu akipiga siku kuhusu kumtumia hela sipokei na simtumii pesa yoyote, liwalo na lile,
 
Kuna kitu katuficha, huenda alikuwa demu wake au kipozeo...

Hakua dem wangu wala hakuwa kipozeo, it was the first time to meet each other. Na ndo ilkua mara ya mwisho tukapotezana mazima alikuja kunitafta baada ya miezi sita akisema amejifungua na wakati akiwa na mimba hakuwahi niambia kuwa ana mimba, it seemz jamaa aliempa mimba either alimluka ama jamaa hamudu mahitaji ya mtoto ipasavyo.
 
Alijuaje mahali pako pa kazi?

anakuja ofsini ninapofanyia kazi bila taarifa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom