Kusimikwa kwa Mkuu wa Kanisa, KKKT, Usharika wa Moshi mjini

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
18,394
16,391
Ibada imependeza wageni kutoka nje na ndani ya nchi!
Nitatoa Updates Zote baada ya ibada.

=================================================

Ibada ilikuwa nzuri sana!!
Mkuu mpya wa kanisa la kiinjili la
kilutheri, alitoa hotuba nzuri na ya
kupendeza.
Askofu Dr. Shoo, alipongeza kasi ya
Magufuli kwenye kutumbua majibu, na
alitahadharisha umakini na busara
zitumike ili wasio husika
wasiadhiriwe.
Askofu aliomba serikali itazame upya
swala la bei elekezi kwenye kutoa
elimu na lazma wadau wahusishwe.
Mkuu huyu mpya wa Kanisa ameiomba
serikali kuheshimu mihimili yote kwa
haki.
Amelaani sana kitendo cha majeshi
kuingia bungeni na wakati Bunge ni
sehemu ya kidemokrasia.
Askofu Shoo ameiomba serikali
itazame upya swala la katiba mpya
kwani wananchi wanahitaji katiba
mpya.
Pia amesisitiza uongozi wa umma
kuwa vizuri na uadilifu.

Kassimu Majaliwa, amejaribu kujibu baadhi ya hoja za Askofu Shoo,
Kuhusu Ada elekezi amesema watajitahidi sana na ni lazima wawashirikishe wadau wa elimu(wamiliki wa shule binafsi) ili waweze kukidhi mahitaji yao!

Kuhusu Katiba Mpya Majaliwa kasema amelichukua na litafanyiwa kazi...

Majaliwa amelishukuru sana kanisa kwa mchango wake mkubwa wa kuwahudumia wananchi kwa njia mbalimbali, haswa kwenye maswala ya Afya na Elimu.

================================================================================
Askofu Wa kanisa Katoliki Dayosisi ya
Moshi Padre Isack Aman Massawe.
Kasema serikali inatoa.huduma
kulingana na kodi inayokusanya!
amesisitiza watu kufanya kazi ili
serikali ipate pesa za kuwa hudumia.
Askofu Isack kasema hakuna kitu cha
bure, hiyo elimu bure kwa wanafunzi
haipo as long as watu wanalipa kodi
 
Sawa mkuu tunasubiri updates kwa hamu sana, ila siku nyingine usiwe na haraka ya kupost kabla hujamaliza sala

Mimi ni mtaalamu wa live updates, sema leo niko na wageni hapa, sitaweza kuifanya kazi kwa uhuru.
 
Anatambua uwepo wa Mawaziri wakuu wastaafu...pamoja na wake zao.
 
Bunge: Demokrasia itaimarishwa
anasema bunge ni kioo, na ataendelea kusimamia maadili.
Bunge liwe sehemu nzuri yakujenga kizazi kinachokuja.
 
Hapa tu ndio huwa nawadharaugi sana viongozi wa dini, hususani Wagalatia. Kwa sababu.

1/Wanatoa madhabahu zao kuwa majukwaa ya kisiasa na kiserikali. Kwa mfano hapo Kasimu Majaliwa(Ambaye hata kiimani sio Mkristo wala Mlutheri) anapewa madhabahabu na kuanza kutoa hotuba za kisiasa na kiserikali.

2/Wanaacha taratibu zao rasmi za kufanya ibada ili tu kiruhusu itifaki za viongozi wa Kisiasa na kiserikali zifanye kazi kanisani. Yaani ibada itawahi au kuchelewa kuanza au itachelewa kwisha kisa tu kuna kiongozi wa serikali yuko hapo. Kuna mahubiri hayatahubiriwa kisa tu yanaweza kumkwaza mwanasiasa fulani hapo kanisani.
Usishangae leo hapo kanisani waumini wakibuhudhiwa na maafisa usalama kisa tu, waziri mkuu Kassimu Majaliwa yupo hapo.
 
Back
Top Bottom