Mgogoro watikisa kanisa la Biblia Moshi

Mgogoro watikisa kanisa la Biblia Moshi

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
236
Reaction score
249
MGOGORO mkubwa wa kugombea umiliki na uendeshaji wa kanisa la Biblia Tanzania Kaskazini umeibuka huku baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wakifukuzwa na kusimamishwa kutoa huduma za Kiroho.

Mchungaji Benard Elly ambaye amekuwa akihudumu kwenye kanisa hilo kwa muda mrefu,amevurushwa na mtu anayejitambulisha kwa jina la Egjus Nchimbi ambaye amejitwalia madaraka ya uongozi bila baraka za kanisa hilo.

Nchimbi ambaye amekataa kuzungumzia mgogoro huo kwa madai si msemaji wa kanisa ,pia anadaiwa kumwandikia barua ya onyo Kali Askofu wa kanisa hilo,Ombeni Mille.

Askofu Mille amedhibitisha kuandikiwa barua hiyo huku akihoji mamlaka ya Nchimbi ya kumwandikia barua hiyo .

Jumapili iliyopita ,mchungaji Benard alijikuta akinyang'anywa kipasa sauti wakati wa Ibaada kanisani hatua ambayo ulizua mtafaruku kanisani hapo.

Benard amekuwa akiishi kanisani hapo kwa zaidi ya miaka 25 akitokea kituo cha Watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi .

Mgogoro huo umepelekea Mamlaka za serikali kusitisha utoaji wa huduma kanisani hapo baada ya Nchimbi kwenda Baraza la Ardhi la Kata ya Pasua akidai kujimilikisha kanisa.

Wakati hayo yakiendelea taarifa zinadai kuwa hati ya kiwanja namba 252 kitalu JJJ cha Kanisa hilo inadaiwa kupotea Katika mazingira ya kutatanisha ikiwa mikononi mwa mkandarasi Joseph Tillya aliyekuwa akijenga chuo cha Biblia cha Kanisa hilo.

Tillya tayari ameshatoa taarifa polisi za kupotea kwa hati hiyo na kupewa jalada namba PHQ/KIL/MOS/13274/2024 ya June ,2024 .

Kanisa hilo lenye hati ya usajili namba 15537 SA,lipo chini ya Taasisi ya BEREA na kuibuka kwa mgogoro huo kumeibua makundi mawili hasimu moja likimuunga mkono Nchimbi ambaye tayari amejiundia Bodi yake ambaye awali allkuwa mwenyekiti wa bodi ya Kituo cha Moshi Christian Center (MCC) kilichopo chini ya kanisa hilo.

Hata hivyo Askofu Ombeni amesema hatambui Bodi hiyo kwani awali Nchimbi alipewa barua ya kusimamishwa kazi 12/6/2024 na Bodi Halali ikimtaka kukabidhi ofisi 25/6/2024 lakini alipuuza na kuwqgeuka waliomlima barua.

Mbali na Hilo,Nchimbi na kundi lake wameanza kung'oa vibao vya kabisa hilo na mpango mkakati wao ni kubadilisha umiliki wa kanisa hilo .

Tayari Nchimbi amezuiwa kutoa pesa kwenye akaunti ya kanisa hilo baada ya Benki husika kujulishwa zuio Hilo.
Hiyo inatokana na kuwepo kwa madai ya kiasi kikubwa cha fedha kutolewa kwenye akaunti ya kanisa hilo na matumizi yake kutokujulikana jinsi fedha hizo zilivyotumika.
Askofu Ombeni amesema kila walipomtaka Nchimbi kutoa taarifa ya fedha hakufanya hivyo na badala yake akaamua kuunda Bodi yake ambaye Askofu Ombeni amesema hawaitambui.
 
Back
Top Bottom