Kushuka kwa hadhi ya wasomi wa sasa

Kushuka kwa hadhi ya wasomi wa sasa

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba kufahamu ikiwa hadhi wasomi nchini imeshuka au vipi

Kiwango cha elimu yangu ni darasa la Saba tu lakini nilikuwa nikisikia na kuona wasomi walivyokuwa wakiheshimika na Maisha yao yalikuwa bora kwa wengi wao katika kipindi cha uongozi wa awamu ya Pili, awamu ya Tatu na hata awamu ya nne kidogo lakini sio kwa awamu hii ya Tano

Wasomi Wa Sasa ambao wengine nilisoma nao shule ya msingi kipindi hiicho, waliopata bahati kusoma mpaka madiploma na madegree n.k wengi wao wanatia huruma, wamebaki kuitwa wasomi lakn mm cjaona heshima ya kuwa msomi

Wengi wapo mitaani hawana ajira maskini, wanajishughulisha na vijikazi ambavyo havikuwahitaji wasome sana mfano kulima bustani, dereva bodaboda, kuuza chips, kukata mkaa na n.k na hii ni kutokana na kukosa ajira.

Wana Maisha magumu afadhali sie ma mbumbu maana tulishazoea kuparangana na Maisha tunajua tuingie na tutokee wapi tupate fedha lakini wasomi wetu maskini hawajui nini cha kufanya maana walichojifunza wao vyuoni ni kuajiriwa lakini Sasa wanaambiwa wajiajiri.

Au mafanikio kwa elimu ya sasa imekuwa kama kucheza Tatu mzuka au Biko kwa mtoto wa mlala hoi.

Kama wasomi wamekuwa wengi sana basi kwasasa Elimu kuubwa sio Dili tena. Au itakuwa ni Dili Kama itawafundisha wasomi namna ya kujiajiri.

Binasfi sipendi kuona msomi alopoteza muda wake mwingi kusoma tukigombania kazi za wale tusiokuwa na elimu. Mfano Mimi ni Mkata mkaa cha ajabu namuona daktari, mwalim, injinia nao wanakata mkaa sasa ilikuwa na maana Gani kapoteza muda mwingi kwnye elimu?

Kama serikali yetu imeshindwa kuwaajiri wasomi iwaulize serikali zilizopita zilitumia mbinu gani kuwaajiri Kama wasomi wamezidi kiasi kukosa ajira basi tusiwakazanie saana kuwahamasisha watoto wetu wasome kwa bidii ni bora akishamaliza kidato cha nne tu aanze kupambana na harakati za Maisha kuliko kapoteza muuda wa kusoma sijui degree. Ni ushauri wangu mjinga Mimi.

Nawasilisha
Mkuu usisemem yote utaumiza wasomi hizo biashara unazotaja usiendelee,ulichokiandika kina ukweli inategemea na mtazamo,zamani waliosoma kazi ilikuwa ni uhakika lakini ,jiulize lengo la elimu lilikuwa ni watu waajiriwe au wapunguze ujinga?Zama za kusoma upate kazi zimeshapita,tunasoma tuelimike,elimu hiyo itusiaide tukipata kazi hewala tukikosa tuweze kufikiria jia mbadala kama kujiasjiri,au kufanya jambo lililojema.
Dunia imebadilika sasa hivi anaweza akaja mkenya ,mzimbabwe au mtu wa nchi yeyote akafanya kazi hapa.Lakini kusoma ni muhimu ili kujiongezea elimu na ujuzi wa mambo mbalimbali.
 
Nyerer ana MA ya Edinburgh, ambayo ni degree ya kwanza.

Alivyohitimu Edinburgh hiyo ndiyo ilikuwa shahada yake ya kwanza, kabla ya hapo hakuwa na shahada na baada ya hapo hakusomea shahada nyingine.

M.A ya Edinburgh ni tofauti na M.A ya Oxford. M.A ya Oxford ndiyo sawa na hizi M.A za kwetu, ambazo kawaida ni degree ya pili.

Master of Arts (Scotland) - Wikipedia

"The degree of Master of Arts in Scotland typically refers to an undergraduate degree (either a three-year general degree or four-year Honours degree) "

Uskochi vyuo hivi ancient kama St. Andrews, Edinburgh etc, vilikuwa na mfumo wao tofauti

Uskochi walikuwa na mtindo wao tofauti wa kuiita hiyo degree ya kwanza MA.

Kasome Kitabu cha rafiki yangu anayefundisha hapo Edinburgh, Dr. Thomas Mollony kuhusu miaka ya mwanzo ya Nyerere.

Kitabu kinaitwa "Nyerere: The Early Years"

Watu wengi hawaujui ukweli huu kuhusu Nyerere,wanafikiri MA ya Nyerere ni degree ya pili, kwa sababu inaitwa "Masters". Kumbe ni degree ya kwanza katika vyuo "ancient" vya Uskochi, ambayo inaitwa "Masters"

51rLpTQHlRL.jpg

Wow!

Thanks for that factoid.

I too was under the impression that his M.A. was a graduate degree.

Kuna siku niliweka mada hapa kuhusu 'Presidential libraries and museums [US style].

Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]

Taarifa muhimu kama hizo ndo zinapaswa kuhifadhiwa na kufafanuliwa na sehemu kama maktaba za hao viongozi.

Naamini watu walio wengi wanadhani/ wanaamini Nyerere alikuwa na Master's degree/ shahada ya uzamili.

It's shame we don't know a lot about our leaders.
 
Nazungumzia wasomi wa elimu ya juu yaani Form 6, certificate, diploma, degree,masters n.k mwenzangu wewe unajua msomi ni yupi?

Jukumu la elimu ni kumkomboa binadam kutoka ktk maisha ya hali ya chini (shida nyingi) na kumfanya binadam aishi maisha bora zaidi kwa kuitumia elimu yake vizuri. Swali kwako je unafikiri elimu ya Tanzania inamjenga mtu katika kutumia maarifa ili ajikwamue kutoka ktk maisha duni kwenda maisha bora??

Kuna msemo nilisikia wanasema "Ya Mzungu Darasani, Ya Nyerere mtaani". Mtu akiwa na hizi elimu mbili basi huyo ataweza kujikomboa kutoka katika maisha duni na kuwa na maisha bora. Elimu ya darasani pekee kwa tanzania bado haijafikia kuweza kumfanya mtu apambane na changamoto kwa sababu mara nyingi tunasoma kwa theory sana kuliko vitendo.
 
Usomi mana yake nini?

Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara, ana Ph.D, alikuwa anasema mtu kama hana degree hawezi hata kuongea naye

Huyo atakuwa alikuwa ni bonge la limbukeni na si msomi aliyepikika na akawiva.

Msomi aliyewiva sidhani kama anaweza kufanya ubaguzi wa namna hiyo kwa sababu atatambua kwamba hata kama mtu hana shahada ya chuo kikuu, akijichanganya naye kimaongezi hatokosa walau mawili matatu yaliyo mazuri na ya kujifunza.

Hata mtu mwenye ulemavu wa akili unaweza kujifunza mengi tu toka kwake licha ya huo ulemavu wake!!

Usomi unapaswa umfungue mtu kifikra. Kumbe wengine ndo wanazidi kujifunga tu.

Shameful.
 
Usomi mana yake nini?

Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara, ana Ph.D, alikuwa anasema mtu kama hana degree hawezi hata kuongea naye , wakati baba yake na mama yake waliomsomesha mpaka akapata Ph.D aliongea nao, na hawana hata cheti cha form six, tutamsifu huyu msomi kwa akili hizi?

Mganga wa madawa ya asili (herbalist) ambaye ameishia darasa la nne baada ya kujua kusoma na kuandika, lakini alirithishwa mikoba na babu yake kujua mitishamba mingi sana, na matibabu yake kwa matatizo mbalimbali ya afya, ambaye hata makampuni makubwa ya dawa yakitaka kutengeneza dawa mpya yanaweza kumsikiliza, kama hana cheti cha darasa la saba, ni msomi au si msomi?

Nyerere ana degree ya kwanza tu, ukiondoa za heshima, kaweka misingi ya taifa na kaeleza falsafa ya Ujamaa mpaka kakubalika dunia nzima.

Mwenzake mwingine ana Ph.D hata kuunganisha sentensi mbili kazi.

Msomi ni nani?
Kwa nionavyo Mimi usomi ni cheo au wadhifa aupatao mtu baada ya kufikia kiwango fulani cha elimu kinachotambulika kwa watu wote kuwa ni elimu ya juu.

Msomi ana elimu aliyosoma darasani, lakini kuwa na elimu ni jambo Moja na matumizi ya elimu hiyo ni jambo lingine. Wapo wanaoitumia vizuri( wamefanikiwa) wapo wanaoitumia vibaya( hawajafanikiwa) Kama huyo Dr. Mwenye pHD, wapo wasioweza kutumia elimu yao vizuri wala vibaya (wasiojilewa, walikuwa na uwezo mkubwa wa kukariri darasani na kufaulu tu)
Wapo wenye vipaji vya kuzaliwa ingawa hawa hawatambuliki Kama wasomi lakini wanaweza kuwa bora kuliko wasomi mfano ni huyo mganga tiba za asili za mitishamba.

Utambue kuwa kuna wasomi na mabingwa walobobea katika Nyanja mbali mbali, maana ya msomi itabaki kuwa Yule aliyekaa darasani na kusoma hadi kufikia elimu ya juu
Wengine hao ni sio wasomi Bali wanavipaji na wamebobea tu ila hatuwezi kuwaita wasomi
 
Kiranga mimi nakukubali umesoma sana na unaufahamu wa mambo mengi.Big up,lakini umepungukiwa na kitu kimoja tu.Najua unakijua,nilikusalimia kwa sentensi ya mistari kama miwili ukanijibu kwa "kitabu kizima".
Hata wasomi na wenye maarifa makubwa hawakosi kasoro
 
Unasoma ili upate kazi, ama upate ujuzi? Ukisoma ili upate kazi ndiyo matokeo kama hayo unayosema. Ika ukisoma ili upate ujuzi, hautahitaji kulalamika bali utakachofanya ni kuutumia ujuzi uliopata shuleni kukidhi mahitaji yako na kuisaidia jamii. Usiwashangae wasomi wengi wanaozalishwa leo hii hapa nchini, bali shangaa mfumo wa elimu uliofikisha wasomi mahala hapo walipo.

Malcom Lumumba karibu katika mjadala wa huyu ndugu maana naona ameleta hoja inayoendana na mjadala kuhusu elimu yetu Tanzania uliyoianzisha.
 
Nyerer ana MA ya Edinburgh, ambayo ni degree ya kwanza.

Alivyohitimu Edinburgh hiyo ndiyo ilikuwa shahada yake ya kwanza, kabla ya hapo hakuwa na shahada na baada ya hapo hakusomea shahada nyingine.

M.A ya Edinburgh ni tofauti na M.A ya Oxford. M.A ya Oxford ndiyo sawa na hizi M.A za kwetu, ambazo kawaida ni degree ya pili.

Master of Arts (Scotland) - Wikipedia

"The degree of Master of Arts in Scotland typically refers to an undergraduate degree (either a three-year general degree or four-year Honours degree) "

Uskochi vyuo hivi ancient kama St. Andrews, Edinburgh etc, vilikuwa na mfumo wao tofauti

Uskochi walikuwa na mtindo wao tofauti wa kuiita hiyo degree ya kwanza MA.

Kasome Kitabu cha rafiki yangu anayefundisha hapo Edinburgh, Dr. Thomas Mollony kuhusu miaka ya mwanzo ya Nyerere.

Kitabu kinaitwa "Nyerere: The Early Years"

Watu wengi hawaujui ukweli huu kuhusu Nyerere,wanafikiri MA ya Nyerere ni degree ya pili, kwa sababu inaitwa "Masters". Kumbe ni degree ya kwanza katika vyuo "ancient" vya Uskochi, ambayo inaitwa "Masters"

51rLpTQHlRL.jpg
Wasomi wanajaribu kuwekana sawa

Wenzangu na Mimi tunasubiri hitimisho
 
Mkuu usisemem yote utaumiza wasomi hizo biashara unazotaja usiendelee,ulichokiandika kina ukweli inategemea na mtazamo,zamani waliosoma kazi ilikuwa ni uhakika lakini ,jiulize lengo la elimu lilikuwa ni watu waajiriwe au wapunguze ujinga?Zama za kusoma upate kazi zimeshapita,tunasoma tuelimike,elimu hiyo itusiaide tukipata kazi hewala tukikosa tuweze kufikiria jia mbadala kama kujiasjiri,au kufanya jambo lililojema.
Dunia imebadilika sasa hivi anaweza akaja mkenya ,mzimbabwe au mtu wa nchi yeyote akafanya kazi hapa.Lakini kusoma ni muhimu ili kujiongezea elimu na ujuzi wa mambo mbalimbali.
Umesema ukweli kabisa
Lakini ulisemalo halimo vichwani mwa wanafunzi wetu wa kitanzania ndomana hata wewe umenishauri kuwa nisiwaumize roho kwa kutaja kazi zinazo wadhalilisha wasomi maana wakiwa wanasoma wanategemea kuajiriwa na ukiwambia wanafunzi wasome lakn ajira hakuna wengi watakata tamaa ya kusoma
 
Hapo sawa Mkuu. Akili yako sasa upgrade isiwe kijiko iwe mwiko
Ahahah asante kwa ushauri nitalifanyia kazi wazo lako japo nitaaribu maana sababu Akili Kijiko maana yake akili kidogo ujazo wa Kijiko sasa nikitaka ku upgrade labda iwe akili Sufuriaa
 
Wow!

Thanks for that factoid.

I too was under the impression that his M.A. was a graduate degree.

Kuna siku niliweka mada hapa kuhusu 'Presidential libraries and museums [US style].

Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]

Taarifa muhimu kama hizo ndo zinapaswa kuhifadhiwa na kufafanuliwa na sehemu kama maktaba za hao viongozi.

Naamini watu walio wengi wanadhani/ wanaamini Nyerere alikuwa na Master's degree/ shahada ya uzamili.

It's shame we don't know a lot about our leaders.
Mimi mwenyewe nilisikia hili zamani nikawa sijalielewa, nilivyosoma kitabu cha Dr. Mollony wa Edinburgh na kufuatilia hiyo M.A ya Edinburgh ikoje, ndiyo nikajua kumbe ni "undergraduate M.A".

Kitabu kina story nyingi sana mpaka Nyerere ilikuwa bado kidogo akatishe masomo kwa sababu familia yake ilikosa fedha za kujikimu. Halafu kuna mwanamke Nyerere alitaka kuozeshwa kabla ya Mama Maria, haikuwa riziki yake Waswahili wanasema.

It is such an eye opener.
 
Kuna msemo nilisikia wanasema "Ya Mzungu Darasani, Ya Nyerere mtaani". Mtu akiwa na hizi elimu mbili basi huyo ataweza kujikomboa kutoka katika maisha duni na kuwa na maisha bora. Elimu ya darasani pekee kwa tanzania bado haijafikia kuweza kumfanya mtu apambane na changamoto kwa sababu mara nyingi tunasoma kwa theory sana kuliko vitendo.
Umenena vyema mkuu
 
Huyo atakuwa alikuwa ni bonge la limbukeni na si msomi aliyepikika na akawiva.

Msomi aliyewiva sidhani kama anaweza kufanya ubaguzi wa namna hiyo kwa sababu atatambua kwamba hata kama mtu hana shahada ya chuo kikuu, akijichanganya naye kimaongezi hatokosa walau mawili matatu yaliyo mazuri na ya kujifunza.

Hata mtu mwenye ulemavu wa akili unaweza kujifunza mengi tu toka kwake licha ya huo ulemavu wake!!

Usomi unapaswa umfungue mtu kifikra. Kumbe wengine ndo wanazidi kujifunga tu.

Shameful.
Mengine ni mapungufu tu aliyonayo mtu kulinga na alivolelewa na utu alionao hata wasomi waliopikwa wakaiva wanaweza kuwa na roho mbaya ya ubaguzi, uchoyo, udicteta. Kama ilivyo kwa wasiosoma wapo wenye utu na haiba nzuri japo hawajui hata kusoma
 
Umesema ukweli kabisa
Lakini ulisemalo halimo vichwani mwa wanafunzi wetu wa kitanzania ndomana hata wewe umenishauri kuwa nisiwaumize roho kwa kutaja kazi zinazo wadhalilisha wasomi maana wakiwa wanasoma wanategemea kuajiriwa na ukiwambia wanafunzi wasome lakn ajira hakuna wengi watakata tamaa ya kusoma
Kuzalilika pia ndugu yangu ni jinsi mtu mwenyewe anavyo define,nitakupa mfaano kuna watu walileta hoja ooh inakuwaje bakresa anauza mpaka chapati?Sasa mwingine anaweza akaona kakosea,lakini anayejua mambo ya biashara anajua idadi kubwa ya watu ni amsikini kwa hiyo ukiwa na bidhaa inayonunuliwa na watu wa chini na wanaitumia kila siku uapata pesa nyingi kuliko kampuni inayouza gari za gharama zinazotumiwa na wachache.
Mimi binafsi nafanya kazi yoyote kama nitaona inanifaa bila kujari nia elimu kiasi gani,swali la kizushi,kuna mtu ukikutana naye njiani unaona usoni pake ameandikwa amesoma mpaka elimu gani?Mungu alijua.
Sasa hivi ndugu yangu ni kupambana kotekote,shida ya wasomi wanajiuliza maswali mengi kabla ya kufanya kitu na hii inatokana na shule,what if?What is tthe profit margin?What is the return of investment?What is the return on investment?Wakati wanatafuta majibu ,asiyesoma ila ni risk taker by nature anatengeneza pesa,by the time wanashituka "the market is saturated",ukienda kariakoo naamini utakuta wasomi wachache wanafanya biashara.
Kuna kitabu cha mtu mmoja namkubali sana kwenye haya mambo ya biashara ametunga kitabu hiki hapa chini

upload_2018-4-13_23-13-0.jpeg


This is a fact and not an opinion.Elimu inalemaza wakati mwingine ,tena elimu inaweza ikamharibu mtu kama ambavyo imemfanya Kiranga aseme hakuna Mungu.Hili jina lakitabu linaumiza wasomi wengi sana nikiwe
 
Bora umetusaidia Jamaa alishatupa tango pori
Fuatilia mjadala. Soma "Nyerere: The Early Years" kama unajua Kiingereza.

Usipende kushutumu tu.

Master of Arts (Scotland) - Wikipedia

The degree of Master of Arts in Scotland typically refers to an undergraduate degree (either a three-year general degree or four-year Honours degree) in humanities or social sciences awarded by one of the ancient universities of Scotland (the University of St Andrews, the University of Glasgow, the University of Aberdeen and the University of Edinburgh) p
 
Unasoma ili upate kazi, ama upate ujuzi? Ukisoma ili upate kazi ndiyo matokeo kama hayo unayosema. Ika ukisoma ili upate ujuzi, hautahitaji kulalamika bali utakachofanya ni kuutumia ujuzi uliopata shuleni kukidhi mahitaji yako na kuisaidia jamii. Usiwashangae wasomi wengi wanaozalishwa leo hii hapa nchini, bali shangaa mfumo wa elimu uliofikisha wasomi mahala hapo walipo.

Malcom Lumumba karibu katika mjadala wa huyu ndugu maana naona ameleta hoja inayoendana na mjadala kuhusu elimu yetu Tanzania uliyoianzisha.
Sio mfumo wa elimu tu bali mfumo wa Maisha ya watanzania ktk Nyanja zote Kama kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na nk.

Kwa uliloliongelea wewe la ujuzi hebu nikuulize kaswali kdogo

Watoto wa walala hoi( walio wengi kulinganisha na matajiri) huchagua kozi ambazo zina vipaumbele katika kupewa mikopo na zenye ajira zisizokuwa na utata. Mfano mtu alipenda kusoma uchumi mifumo inamlazimisha akasome udaktari au ualimu, na baada ya kupata ujuzi huo ambao hakuupenda bali mazingira yalimlazimisha hapati ajira aliyoifikiria mwanzo je unategemea huyo mwalimu maskini atumie ujuzi wake kujenga shule afundishe? Au daktari afungue hospital yake wakati mpaka hapo hawana hata mapenzi na taaluma zao?
 
Kuzalilika pia ndugu yangu ni jinsi mtu mwenyewe anavyo define,nitakupa mfaano kuna watu walileta hoja ooh inakuwaje bakresa anauza mpaka chapati?Sasa mwingine anaweza akaona kakosea,lakini anayejua mambo ya biashara anajua idadi kubwa ya watu ni amsikini kwa hiyo ukiwa na bidhaa inayonunuliwa na watu wa chini na wanaitumia kila siku uapata pesa nyingi kuliko kampuni inayouza gari za gharama zinazotumiwa na wachache.
Mimi binafsi nafanya kazi yoyote kama nitaona inanifaa bila kujari nia elimu kiasi gani,swali la kizushi,kuna mtu ukikutana naye njiani unaona usoni pake ameandikwa amesoma mpaka elimu gani?Mungu alijua.
Sasa hivi ndugu yangu ni kupambana kotekote,shida ya wasomi wanajiuliza maswali mengi kabla ya kufanya kitu na hii inatokana na shule,what if?What is tthe profit margin?What is the return of investment?What is the return on investment?Wakati wanatafuta majibu ,asiyesoma ila ni risk taker by nature anatengeneza pesa,by the time wanashituka "the market is saturated",ukienda kariakoo naamini utakuta wasomi wachache wanafanya biashara.
Kuna kitabu cha mtu mmoja namkubali sana kwenye haya mambo ya biashara ametunga kitabu hiki hapa chini

View attachment 743816

This is a fact and not an opinion.Elimu inalemaza wakati mwingine ,tena elimu inaweza ikamharibu mtu kama ambavyo imemfanya Kiranga aseme hakuna Mungu.Hili jina lakitabu linaumiza wasomi wengi sana nikiwe
Ukweli mtupu japo katika suala la Kiranga kutomuamini Mungu ni kutokana na kukosa elimu ya kiroho (meta-physics) yeye ameegemea sana kwenye elimu ulimwengu wa vitu vinavyodhihirika bayana na hataelewa mpaka siku atakapo amua kujifunza kwa dhati neno la Mungu
 
Back
Top Bottom