Kushuka kwa hadhi ya wasomi wa sasa

Kushuka kwa hadhi ya wasomi wa sasa

AKILI KIJIKO

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
405
Reaction score
592
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba kufahamu ikiwa hadhi wasomi nchini imeshuka au vipi

Kiwango cha elimu yangu ni darasa la Saba tu lakini nilikuwa nikisikia na kuona wasomi walivyokuwa wakiheshimika na Maisha yao yalikuwa bora kwa wengi wao katika kipindi cha uongozi wa awamu ya Pili, awamu ya Tatu na hata awamu ya nne kidogo lakini sio kwa awamu hii ya Tano

Wasomi Wa Sasa ambao wengine nilisoma nao shule ya msingi kipindi hiicho, waliopata bahati kusoma mpaka madiploma na madegree n.k wengi wao wanatia huruma, wamebaki kuitwa wasomi lakn mm cjaona heshima ya kuwa msomi

Wengi wapo mitaani hawana ajira maskini, wanajishughulisha na vijikazi ambavyo havikuwahitaji wasome sana mfano kulima bustani, dereva bodaboda, kuuza chips, kukata mkaa na n.k na hii ni kutokana na kukosa ajira.

Wana Maisha magumu afadhali sie ma mbumbu maana tulishazoea kuparangana na Maisha tunajua tuingie na tutokee wapi tupate fedha lakini wasomi wetu maskini hawajui nini cha kufanya maana walichojifunza wao vyuoni ni kuajiriwa lakini Sasa wanaambiwa wajiajiri.

Au mafanikio kwa elimu ya sasa imekuwa kama kucheza Tatu mzuka au Biko kwa mtoto wa mlala hoi.

Kama wasomi wamekuwa wengi sana basi kwasasa Elimu kuubwa sio Dili tena. Au itakuwa ni Dili Kama itawafundisha wasomi namna ya kujiajiri.

Binasfi sipendi kuona msomi alopoteza muda wake mwingi kusoma tukigombania kazi za wale tusiokuwa na elimu. Mfano Mimi ni Mkata mkaa cha ajabu namuona daktari, mwalim, injinia nao wanakata mkaa sasa ilikuwa na maana Gani kapoteza muda mwingi kwnye elimu?

Kama serikali yetu imeshindwa kuwaajiri wasomi iwaulize serikali zilizopita zilitumia mbinu gani kuwaajiri Kama wasomi wamezidi kiasi kukosa ajira basi tusiwakazanie saana kuwahamasisha watoto wetu wasome kwa bidii ni bora akishamaliza kidato cha nne tu aanze kupambana na harakati za Maisha kuliko kapoteza muuda wa kusoma sijui degree. Ni ushauri wangu mjinga Mimi.

Nawasilisha
 
Wasomi hanaojitambua hufanya kazi za kawaida ambazo hazihitaji elimu kubwa lakini huo huwa ni mwanzo tu. Watu hawa huwa na malengo makubwa. Ni nadra kukuta msomi anafanya kazi ya kuchoma mkaa miak 5. Huwa wanafanya kazi hizo kwa mpito tu.
 
Wasomi mnatakiwa kujua kuwa usomi wa kutegemea ajira ndani ya nchi yetu ni ngumu sana labda mjitahidi kupata ajira nchi za jirani. Tanzania yetu bado inatatizo la kubebana hata kama hakuna elimu yoyote ilimradi mtoto wa dada,kaka, na vitu kama ivo.. Hili swala linanyima haki sana wasomi ambao wanahitimu masomo yao matokeo yake sasa.. Msomi huyo ambae muda wake mwingi alikuwa anautumia kusoma na kukosa muda hata wa kujichanganya na watu au biashara kwa ajili ajiwekee maandalizi ya kuzoea mazingira ya kujipatia kipato...Matokeo yake ni pale anapomaliza masomo alafu hana kitu anachoweza kufanya ili ajiingizie kipato anabaki kusubiri ajira kwenye nchi isiojuwa umuhimu wa wasomi.. Mifano ipo wazi katika serikali na makampuni binafsi kwamba kuna ka ujamaa kapo na hakatakuja kuisha sijui labda mimi niwe Raisi---

Maono yangu Wasomi msijidanganye sana na kujaza vyeti ndani juweni na kujipa uzoefu wa utaftaji pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji pindi mnaposubiri kumtumikia bwana au kuajiriwa.....
 
Usomi mana yake nini?

Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara, ana Ph.D, alikuwa anasema mtu kama hana degree hawezi hata kuongea naye , wakati baba yake na mama yake waliomsomesha mpaka akapata Ph.D aliongea nao, na hawana hata cheti cha form six, tutamsifu huyu msomi kwa akili hizi?

Mganga wa madawa ya asili (herbalist) ambaye ameishia darasa la nne baada ya kujua kusoma na kuandika, lakini alirithishwa mikoba na babu yake kujua mitishamba mingi sana, na matibabu yake kwa matatizo mbalimbali ya afya, ambaye hata makampuni makubwa ya dawa yakitaka kutengeneza dawa mpya yanaweza kumsikiliza, kama hana cheti cha darasa la saba, ni msomi au si msomi?

Nyerere ana degree ya kwanza tu, ukiondoa za heshima, kaweka misingi ya taifa na kaeleza falsafa ya Ujamaa mpaka kakubalika dunia nzima.

Mwenzake mwingine ana Ph.D hata kuunganisha sentensi mbili kazi.

Msomi ni nani?
 
Hiyo ni kwanaojitambua kwa wasiojitambua wanaangukia kwenye dimbwi la madawa ya kulevya, ulevi, na uchangudoa kwa kukata tamaa ya Maisha sababu kuu ikiwa ni mifumo mibovu ya nnchi ktk kutoa elimu na ajira
 
Mkuu msomi ni relative term so hakuna SI Unit ya msomi. Unaposema msomi unamaanisha mwenye level ipi coz hata anejua kusoma na kuandika pia ni msomi
Nazungumzia wasomi wa elimu ya juu
 
Usomi mana yake nini?

Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara, ana Ph.D, alikuwa anasema mtu kama hana degree hawezi hata kuongea naye , wakati baba yake na mama yake waliomsomesha mpaka akapata Ph.D aliongea nao, na hawana hata cheti cha form six, tutamsifu huyu msomi kwa akili hizi?

Mganga wa madawa ya asiliambaye ameishia darasa la nne baada ya kujua kusoma na kuandika, lakini alirithishwa mikoba na babu yake kujua mitishamba mingisana, na matibabu yake kwa matatizo mbalimbali ya afya, ambaye hata makampuni makubwa ya dawa yakitakakutengeneza dawa mpya yanaweza kumsikiliza, kama hana cheti cha darasa la saba, ni msomi au si msomi?

Nyerere ana degree ya kwanza tu, kaweka misingi ya taifa na kaeleza falsafa ya Ujamaa mpaka kakubalika dunia nzima.

Mwenzake mwingine ana Ph.D hata kuunganisha sentensi mbili kazi.
Kiranga mimi nakukubali umesoma sana na unaufahamu wa mambo mengi.Big up,lakini umepungukiwa na kitu kimoja tu.Najua unakijua,nilikusalimia kwa sentensi ya mistari kama miwili ukanijibu kwa "kitabu kizima".
 
Usomi mana yake nini?

Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara, ana Ph.D, alikuwa anasema mtu kama hana degree hawezi hata kuongea naye , wakati baba yake na mama yake waliomsomesha mpaka akapata Ph.D aliongea nao, na hawana hata cheti cha form six, tutamsifu huyu msomi kwa akili hizi?

Mganga wa madawa ya asili (herbalist) ambaye ameishia darasa la nne baada ya kujua kusoma na kuandika, lakini alirithishwa mikoba na babu yake kujua mitishamba mingi sana, na matibabu yake kwa matatizo mbalimbali ya afya, ambaye hata makampuni makubwa ya dawa yakitaka kutengeneza dawa mpya yanaweza kumsikiliza, kama hana cheti cha darasa la saba, ni msomi au si msomi?

Nyerere ana degree ya kwanza tu, ukiondoa za heshima, kaweka misingi ya taifa na kaeleza falsafa ya Ujamaa mpaka kakubalika dunia nzima.

Mwenzake mwingine ana Ph.D hata kuunganisha sentensi mbili kazi.

Msomi ni nani?
Nyerere ana MA tena ya Edinburgh, hata mapambano ya uhuru aliyaanza akiwa asharud kutoka Scotland
 
Kwako wewe msomi ni nani?

Unafikiri elimu ina jukumu gani kwa binadamu?
Nazungumzia wasomi wa elimu ya juu yaani Form 6, certificate, diploma, degree,masters n.k mwenzangu wewe unajua msomi ni yupi?

Jukumu la elimu ni kumkomboa binadam kutoka ktk maisha ya hali ya chini (shida nyingi) na kumfanya binadam aishi maisha bora zaidi kwa kuitumia elimu yake vizuri. Swali kwako je unafikiri elimu ya Tanzania inamjenga mtu katika kutumia maarifa ili ajikwamue kutoka ktk maisha duni kwenda maisha bora??
 
Kiranga mimi nakukubali umesoma sana na unaufahamu wa mambo mengi.Big up,lakini umepungukiwa na kitu kimoja tu.Najua unakijua,nilikusalimia kwa sentensi ya mistari kama miwili ukanijibu kwa "kitabu kizima".
Tatizo nimesoma sana dini.

Kwenye Quran nakumbuka nilifundishwa mtu akikusalimia kidogo, wewe mrudishie salamu kwa bashasha kemkem.

Kwa hiyo ukinisalimia maneno kidogo nikakurudishia salamu kemkem na hadithi na maneno na bashahsha na maswali, ujue nafuata mafundisho mazuri ya Quran na kukuthamini kwa bashasha kama ndugu yangu.

Kuna Mzee mmoja mwanajeshi (here we go again na stories) alikuwa kila siku anapita kijiweni, mzee hapendi stories sana.

Halafu inaonekana alikuwa hapendi shikamoo.

Basi watoto wa jirani wakimuamkia "Shikamoo" Mzee anaitikia kwa kutingisha kichwa tu. Pengine yeye aliona kuitikia "Marahaba" ni kukubali salamu ya kitumwa, lakini wale watoto wa jirani hawakuichukulia poa habari ile, ikaonekana kama vile yule Mzee aliwadharau kwa kutowaitikia kwa bashasha.

Kwa hiyo na mimi natumia bashasha vizuri tu.

Halafu usipende sana kuona mwenzako kapungukiwa bila hata kujadiliana naye, inawezekana wewe ukawa ndiye uliyepungukiwa na mwenzako ana la kukufunza.

Au hata kama yeye kapungukiwa, unaweza kumnyima wasaa wa kujifunza alichopungukiwa ni kipi.

Tuambizane tu, bila rabsha, kwa bashasha, kwa kutaka heri na fanaka,
 
Nyerere ana MA tena ya Edinburgh, hata mapambano ya uhuru aliyaanza akiwa asharud kutoka Scotland
Nyerere ana MA ya Edinburgh, ambayo ni degree ya kwanza.

Alivyohitimu Edinburgh hiyo ndiyo ilikuwa shahada yake ya kwanza, kabla ya hapo hakuwa na shahada na baada ya hapo hakusomea shahada nyingine.

M.A ya Edinburgh ni tofauti na M.A ya Oxford. M.A ya Oxford ndiyo sawa na hizi M.A za kwetu, ambazo kawaida ni degree ya pili.

Master of Arts (Scotland) - Wikipedia

"The degree of Master of Arts in Scotland typically refers to an undergraduate degree (either a three-year general degree or four-year Honours degree) "

Uskochi vyuo hivi ancient kama St. Andrews, Edinburgh etc, vilikuwa na mfumo wao tofauti

Uskochi walikuwa na mtindo wao tofauti wa kuiita hiyo degree ya kwanza MA.

Kasome Kitabu cha rafiki yangu anayefundisha hapo Edinburgh, Dr. Thomas Mollony kuhusu miaka ya mwanzo ya Nyerere.

Kitabu kinaitwa "Nyerere: The Early Years"

Watu wengi hawaujui ukweli huu kuhusu Nyerere,wanafikiri MA ya Nyerere ni degree ya pili, kwa sababu inaitwa "Masters". Kumbe ni degree ya kwanza katika vyuo "ancient" vya Uskochi, ambayo inaitwa "Masters"

51rLpTQHlRL.jpg
 
Tatizo nimesoma sana dini.

Kwenye Quran nakumbuka nilifundishwa mtu akikusalimiakidogo, wewemrudishie salamu kwa bashasha kemkem.

Kwahiyo ukinisalimiamaneno kidogo nikakurudishia salamukemkem na hadithi na manenona bashahsha na maswali, ujue nafuata mafundishomazuri ya Quran na kukuthamini kwa bashasha kama ndugu yangu.

Kuna Mzee mmoja mwanajeshi (here we go again na stories) alikuwa kila siku anapita kijiweni, mzee hapendi stories sana.

Halafu inaonekana alikuwa hapendi shikamoo.

Basi watoto wa jirani wakimuamkia "Shikamoo" Mzee anaitikia kwa kutingisha kichwa tu. Pengine yeye aliona kuitikia "Marahaba" ni kukubali salamu ya kitumwa, lakini wale watoto wa jirani hawakuichukulia poa habariile, ikaonekana kamavile yule Mzee aliwadharau kw akutowaitikia kwa bashasha.

Kwa hiyo na miminatumia bashasha vizuri tu.

Halafu usipende sana kuona mwenzako kapungukiwa bila hata kujadiliana naye, inawezekana wewe ukawa ndiye uliyepungukiwa na mwenzako ana la kujifunza.

Au hata kama yeye kapungukiwa, unaweza kumnyima wasaa wa kujifunza alichopungukiwa ni kipi.

Tuambizane tu, bila rabsha, kwa bashasha, kwa kutaka heri na fanaka,
Haya mkuu,naanza kukuelewa
 
Nyerer ana MA ya Edinburgh, ambayo ni degree ya kwanza.

Alivyohitimu Edinburgh hiyo ndiyoilikuwa shahada yake ya kwanza, kabla ya hapohakuwa na shahada na baada ya hapo hakusomea shahadanyingine.

Uskochi walikuwa na mtindo wao tofauti wa kuiita hiyo degree ya kwanza MA.

Kasome Kitabu cha rafiki yangu anayefundisha hapo Edinburgh, Dr. Thomas Mollony kuhusu miaka ya mwanzo ya Nyerere.

Kitabu kinaitwa "Nyerere: The Early Years"

Watu wengi hawaujui ukweli huu kuhusu Nyerere,wanafikiri MA ya Nyerere ni degree ya pili, kwa sababu inaitwa "Masters". Kumbe ni degree ya kwanza katika vyuo "ancient" vya Uskochi, ambayo inaitwa "Masters"

51rLpTQHlRL.jpg
Ahsante kwa elim

Hivi mi nikawa najua ni MA kama hizi za kawaida
 
Wasomi mnatakiwa kujua kuwa usomi wa kutegemea ajira ndani ya nchi yetu ni ngumu sana labda mjitahidi kupata ajira nchi za jirani. Tanzania yetu bado inatatizo la kubebana hata kama hakuna elimu yoyote ilimradi mtoto wa dada,kaka, na vitu kama ivo.. Hili swala linanyima haki sana wasomi ambao wanahitimu masomo yao matokeo yake sasa.. Msomi huyo ambae muda wake mwingi alikuwa anautumia kusoma na kukosa muda hata wa kujichanganya na watu au biashara kwa ajili ajiwekee maandalizi ya kuzoea mazingira ya kujipatia kipato...Matokeo yake ni pale anapomaliza masomo alafu hana kitu anachoweza kufanya ili ajiingizie kipato anabaki kusubiri ajira kwenye nchi isiojuwa umuhimu wa wasomi.. Mifano ipo wazi katika serikali na makampuni binafsi kwamba kuna ka ujamaa kapo na hakatakuja kuisha sijui labda mimi niwe Raisi---

Maono yangu Wasomi msijidanganye sana na kujaza vyeti ndani juweni na kujipa uzoefu wa utaftaji pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji pindi mnaposubiri kumtumikia bwana au kuajiriwa.....
Wewe ulipaswa uwe mwalim. Lakini hata ungekuwa Mwalim katika nnchi Kama hii isingesaidia maana badala ya kuwafundisha wanafunzi elimu inayoenda na mazingira yao silabasi zingekulazimisha uwafundishe watoto ma physics yaliyopitwa na wakati huko ulaya. Labda kweli uwe rais ubadili mfumo mzm
 
Back
Top Bottom