Kushindwa kwa olympik kosa ni la nani !? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushindwa kwa olympik kosa ni la nani !?

Discussion in 'Sports' started by sony wega, Aug 13, 2012.

 1. s

  sony wega JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana ktk kufunga michezo ya olympik nimeshudia wakenya na waganda wakiinjoy huku bendera zao zikipeperushwa kwa mafanikio yao ya usimamizi dhabiti ila kwa sisi sijui tunakwenda wapi
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama mnaamua kumueka dr mkangara kama waziri wa mchezo mnategemea kutakua na mafanikio kwenye hii sekta kweli?
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Kuna Rais Mstaafu mmoja alishasema kuwa" watanzania ni kichwa chwa mwendawazimu". Siku hizo hatukufahamu/ hatukuelewa amekusudia nini.

  Sasa tunaanza kufahamu pole pole kama hatutaki kuelewa fasta fasta.

  Wakameroon wamezamia, hawa wa kwetu wakirudi na mabegi yaliyajaa nguo za mitumba.Tushukuru.

  Kama kuna kesho, basi wakiwezeshwa watatuwakilisha vizuri. Vyenginevyo tutaambulia hii
  Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/306729-gazeti-la-the-east-african-katuni-ya-kejeli-kwa-tanzania-olympic.html
   
 4. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,228
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni selikari! hivi wanatumia vigezo gani kupata washiriki?hivi kwa nini tusiache kushiriki?.......dahhhh!!! ugolo tu.Hivi watanzania tunajivunia nini nje ya nch? umasikini ni sisi! taifa stars hamna kitu!olimpiki mikono nyuma! chama kilicho shika dora,akili za mbayuwayu! jamani sisi nini?????
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Halafu kilicho nisikitisha zaidi hivi hata ile ya kurusha mshale tunashindwa hata kupeleka wale morani wakati wanasifika kwa kuua simba. Yaani kuna michexo mingi ambayo tungekuwa makini tungeweza kushiriki lakini tumeng'ang'ania tu riadha wakati msosi wenyewe chipsi na mayai ya kizungu. Tukiambiwa tule dona na ngano hatutaki angalau tungekuwa na stamina. pole yetu tutabaki kuleta makocha wazungu bila kuona mabadiliko.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani it is the right time Tanzania igeukie kwene Fani ya Umbea na Majungu ndio tunavyoviweza tu, haiingii akilini kila tunachofanya tunashindwa
   
 7. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  alaumiwe KIKWETE kama tulivyoea
   
 8. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nafikiri yeye na SERIKALI yake haikwepi lawama hapa, kama aliweka wizara ya michezo na kuwachagua mawaziri Pamoja na katibu Mkuu, kazi yao moja wapo ni kutunga na kusimamia sera endelevu za michezo, na sio kwenda kuwaeka watu ambao wanavimba matumbo yao tu. Wizara ya michezo haiwajibiki chochote kwa michezo tanzania, na mbaya zaidi wanaziacha hadi timu za Taifa kuendeshwa na wababaishaji ili hali hizo ni kitambulisho cha mtanzania na ni suala la kitaifa zaidi. Mm nimechoka kuaibika kwa kweli, WaTz hatuna pa kujivunia
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwanza filibeth bahi ilitakiwa ajiuzuru mwenyewe kabla hajashukiwa, na haitajiki kwa kweli maana hamna lolote. Mimi nawashangaa sana viongozi wa tz ukishakiri umeshindwa kutimiza malengo si unajiuzulu tu. Ikiwezekana serikali imfukuze na tukae bila kushiriki kwa miaka kama 20 ili tujiandae. Hawa viongozi wengi wanang'ang'ania tu kwa vile kuna fungu la pesa linatoka olimpiki kuja lkn hawana hasa nia na dhamira kukuza michezo. Kwa maneno haya mi nasema kiongozi wa olimpiki ambaye kaipeleka timu london na bila kurudi hata na medali ajiuzulu ama afukuzwe kazi. Huku kubebana ni hatari angekuwa L-w-sa angeshamtimua maana mzee huwa aangalii makunyanzi kabisaa.
   
Loading...