...inategemeana hali hiyo itakukumba kwenye mazingira gani. Imagine ushamtafuta mkeo siku nzima, njaa inakuuma, jasho linakutoka, majirani wanakuchungulia madirishani, na washkaji kijiweni wanakunyoshea vidole, wakati huo huo kina mama ntilie wa jirani wanajichekesha na vile vicheko vya ngebe... halafu shabaash... jamaa mmoja wapo anakufuata kukutonya "kawachungulie pale...!"
...eeh Mw'Mungu ndiyo mjuaji, mnh apishilie mbali!!!
...hakuna lenye unafuu mjomba, kufumaniwa ni kufumaniwa tu, ushajiharibia Cv! maana kuna wanaoweza kukuachia 'kilema' cha akili, wakiamua kukuvisha utungo kisha wakuingilie kinyume na maumbile, na picha wakazitoe kwenye 'UWAZI'!!!
...sidhani kama kuna mtu atayeweza kusema ukweli tendo atalolifanya akifikwa na 'kaadhia' hiyo, kwani huwezi jua 'wehu' wa mtu mpaka akumbane na mtihani kama huo.
Mchongoma na wengine,
Faida mojawapo ya kuwa Mwana JF ni pia kupata kujifunza mambo kadha wa kadha. Hili alilolileta Steve D unaweza kuona kama ni jambo la mzaha kwetu kuchangia, lakini ndiyo mambo ambayo yanaigusa jamii ya kawaida ya watanzania. Wengi hupendelea kuongelea uchumi ama siasa, lakini masuala ya mengine ya kijamii kama haya yana nafasi kubwa sana katika kuelimisha umma.
Kabla sijakwenda kutoa maoni au jibu langu juu ya swali au maswali yaliyoulizwa, kwanza ni vema sote tumuangalie binadamu ni nani.
Kwa tafsiri yangu, binadamu ni mnyama kama walivyo wanyama wengine isipokuwa yeye siyo hayawani (irrational). Binadamu ni rational animal.
Kwahiyo basi matendo yoye yafanywayo na wanyama kama vile kupigana, kuwa na wivu (kama jogoo) nk, hivyo vyote binadamu anavimiliki. Tofauti iliypo kati ya binadamu na wanyama wengine, ni namna gani anaweza kumiliki matendo ya yafanywayo na wanyama.
Binadamu amaepewa uwezo wa kujifunza, kuiga na kutawala mazingira yake. Kwa maana mbali ya vitu alivyotunukiwa kama usingizi, hasira, kulia, kucheka nk vilevile huweza kuwa daktari, mfamasia, mkulima, dereva nk.
Kwa kifupi, usisubiri hadi hapo upate matatizo ndiyo utake kujijua kwamba wewe ni nani, ni vema ujijue kuanzia sasa kwamba wewe ni binadamu (mnyama) na sifa zako kama binadamu unazifahamu. Hii itakurahisishia sana kuwa na mahusiano mazuri/kuridhisha na watu au viumbe vingine.
Nikirudi kwenye swali ni kwamba kama nimeoa au nimeolewa ni lazima nijue kwamba ninajihusisha au ninaihusisha nafsi yangu na binadamu mwingine ambaye ana sifa kama zangu.
Kwa upande wangu, linapotokea jambo lolote lile kwanza ni kujipa
muda wa kutafakari kabla ya kuchukua hatua zaidi. Hii elimu kama unayo inakusaidia kumiliki hasira na zaidi hukuongezea uwezo wa kufikiri unapokuwa na tatizo. Kama huna elimu ya kujitambua basi wewe ni hayawani.
Suala la kuachana au kusuluhisha litategemea mazungumzo baina yenu. hata siku moja usijaribu kuchukua maamuzi juu ya mkeo au mume bila ya kuwa na mazungumzo ya kina juu ya mustakabali wenu. Wengi hasa wanaume, huwa na maamuzi ya papo kwa hapo juu ya mustakabali wa ndoa zao pasi na kuangalia au kuzungumza kwa kina juu ya matatizo yao. Wakati mwingine makosa ya mke huwa ni matokeo ya makosa ya mume.