Kushambuliwa Kwa Mtandao wa Jamii Forums.

Kushambuliwa Kwa Mtandao wa Jamii Forums.

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Kuna vijana wa kimasai jirani zangu hapa Naibili wamezoea sana kunitembelea. Kwenye kipindi cha uchaguzi kila siku walitaka kujua nini kinaendelea kwa sababu ni wapenzi wa chadema/ukawa. Kila wakija najitahidi kuwaeleza kinachoendelea kulingana na habari ninazopata JamiiForums.

Kuna siku walikuja nikawaambia sipati habari yoyote kwa sababu sehemu ninayopata habari imeshambuliwa.

"ooooooi!" mmoja alishangaa kusikia hivyo. "kwani hamnaga askari ya kulinda? Hapo mahali pa habari panatakiwa pawe na askari wengi ati wenye mabunduki na mabomu"

Niliona itakuwa ngumu na kupoteza muda kuwaeleza maana ya hayo mashambulizi, nikawaacha wakenda zao.
 
bora ulivyowaacha maana ungeanza kuwaelewesha mngekesha hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom