Kusema uwongo mbele ya kadamnasi

Kusema uwongo mbele ya kadamnasi

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
548
Reaction score
62
Baada ya teknolojia ya simu kuingia Tanzania na mitandao ya simu kuenea kwa wingi, kumejitokeza kijitabia cha kusema Uwongo baina ya watanzania. Kwa mfano mko kwenye daladala kisha mtu anazungumza na simu tena kwa sauti kubwa na kusema, NIPO MUHIMBILI HOSPITALI HAPA NITAKUPIGIA BAADAYE. Anasema uwongo huo kwa sauti kubwa bila woga, aibu wala haya na watu wote wanamsikia. Je hii ni tabia nzuri. Hakuna anayekana kwamba, kusema uwongo ni kubaya iwe mbele ya kadamnasi au kinyume chake, lakini kusema uwongo wa namna hii kunaonesha nini? Tujitahidi kuacha tabia kama hizi kwani hazina mfano mzuri kwa watoto na inazoesha watu na hivyo kufikia hatua ya kuona kwamba, kusema uongo ni jambo la kawaida.
 
Tabia mbaya kabisa. Tabia ya joka wa zamani Ibilisi Dhambi ya uongo ndio dhambi ya kwanza kuitumia shetani alipomdanganya Hawa kuwa akienda kinyume na maagizo ya Mungu hatapata madhara yoyote
 
Kila mtu hudanganya kwa sababu zake hata kama anasema kwa sauti ya juu,mimi niliwahi danganya tena mbele ya mama mkwe lakini ilikuwa for the best na akaelewa maana bila kudanganya kila kitu kingeharibika
 
kusema uongo mbele ya watu na ukiwa peke yako,yote ni sawa tu hiyo yote dhambi,tofauti ukiwa pekeyako unamdanga uyo mtu na shahidi ni mungu peke yake,wakat ukidanganya ukiwa mbele ya watu mashaidi ni mungu na watu wanaokusikiliza
 
Kila mtu hudanganya kwa sababu zake hata kama anasema kwa sauti ya juu,mimi niliwahi danganya tena mbele ya mama mkwe lakini ilikuwa for the best na akaelewa maana bila kudanganya kila kitu kingeharibika
Ni kweli, lakini ninachokusudia ni kwamba, mtu wakati mwingine unalazimika kusema uongo lakini dhamira yako ya ndani inakusuta na unakuwa umelazimika kufanya hivyo. Lakini wako ambao wameufanya uongo kuwa ni sehemu ya maisha yao na hata wanaamini kwamba, ni lazima useme uongo.
 
Natambua kuna watu wanaishi kwa kusema uongo na ndio maisha yao kila siku,wakati mwingine kuongopa si jambo jema hata kidogo na madhara yake huwa makubwa sana.
 
Back
Top Bottom