Kusema ‘Mamlaka zote zimewekwa na Mungu tunapaswa kuzitii’ inatumiwa vibaya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusema ‘Mamlaka zote zimewekwa na Mungu tunapaswa kuzitii’ inatumiwa vibaya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jul 29, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Siku hizi baadhi ya wanasiasa wanapotaka kujenga hoja fulani ili kuhalalisha vitendo vinavyofanywa na baadhi ya vyombo vya dola pale ambapo kuna malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu, tunawasikia baadhi yao wakidai “Mamlaka zote zimewekwa na Mungu tunapaswa kuzitii”. Hii ‘phrase’ inatumiwa vibaya! Ni kweli mamlaka zote za nchi zimewekwa na Mungu na kweli pia inatupasa kuzitii. Lakini tunasahau kwamba hatupaswi kutii mamlaka dhalimu kwa vile ni mamlaka. Ni kama kusema inabidi tuwatii wazazi kwa vile imeandikwa kwenye Biblia - Amri ya Nne ya Mungu. Lakini hatupaswi kuwatii wazazi kama wanatushawishi kutenda dhambi au kuvunja sheria halali za nchi kwa vile ni wazazi. Tunapaswa tu kuwatii wazazi katika mambo yote mema/mazuri. Na tuna uhuru na tunapaswa kutowatii katika mambo mabay yote. Hali kadhalika kwa mamlaka za nchi. Tunapaswa kuzitii mamalaka za nchi kwa vile zimewekwa na Mungu lakini hatupaswi (kama ilivyo kwa wazazi) kutii mamlaka zinazokosa haki au zinazovunja sheria za nchi. Kama mamlaka hizo zikishindwa kuwalinda wananchi wake na mali zao na badala yake kuwa chanzo cha vurugu na machafuko (uvunjaji wa haki za binadamu na kuwafanya wananchi kukosa haki au kunyanyasika kwa sababu hiyo) basi hatupaswi kuzitii mamlaka za aina hiyo. Hivyo, tusipende kupotosha umma, kuwa kutii mamlaka tunatii ‘blindly’, hapana! Ni katika mambo mema tu na si mabaya!
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Waache mambo ya kutumia vifungu kuficha madhaifu yao. Wangetenda haki na kuacha ulafi kwanza.
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ni sehemu gani ya Bible inasema hivyo?
   
 4. K

  Kingofkinzudi Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani jambo hili ni rahisi tu. Mamlaka ya kifisadi haiwezi kuwekwa na Mungu. Mamlaka ya uzinzi, uongo pia haiwezi kuwekwa na Mungu.
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Waraka wa mtume Paulo kwa wakorintho!!
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hii iliwahi kutokea nchini Uganda wakati wa Iddi Amin ambapo ilikuwa imeelekezwa hivi:
  "we should be obedient to the govenment" lakini baadhi wakaenda mbele zaidi na kusema kuwa ilibidi isomeke:
  "we should bu obedient to the JUST government"
  kwa maana hiyo ni challenge kubwa kwa watawaliwa kukubaliana na watawala kwa msingi huo lakini mimi naona inaweza kuwa sawa kwa sababu wakati mwingine Mungu anaamua kuwapa aina watawala ili liwe fundisho la kuwaongezea umakini ili kujifunza kwa kuona badala ya kusikia.
  Unadhani isingekuwa hivi hapa kwetu wewe ungejuaje umuhimu wa viongozi wazuri!????
   
 7. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waache waendelee kutumia phrase hiyo kuhalalisha udhalimu unaofanywa na CCM waone pigo watakalopigwa na Muumba. Jina la Muumba kamwe halitumiwi vibaya ukaachwa hivihivi, bila kukumbwa na ghadhabu ya Mungu.
  Sote tunajua kilichojiri wakati wa uchaguzi.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  hata zilizoingia madarakani kwa rushwa? hata zinazofisadi mali za umma? - mtume paul hakuwa na maana hiyo:
   
Loading...