Kuscratch kwa ITV kupitia Star Times

Tatizo c king'amuzi ni Itv wenyewe wanafanya makusudi ili wauze king'amuzi chao nimejaribu kufuatilia nikaambie siri hii pia sababu ya pili wameona Irv inapendwa wakaamua kufanya hivi

Inawezekana hiyo nadharia yako ni ya kweli maana sijawasikia itv wakilalamika kuhusu hilo, wawe makini lakini kwakuwa wanaweza kutoweka kwenye ramani maana star time imeuza ving'amuzi vingi sana kwa wananchi wa kawaida kabisa
 
Sijasikia kituo cha ITV kikilalamika kuhusu scratches kupitia ving'amuzi vya Star Times. ITV wawe makini sana kwakuwa wanaweza kutoweka kwenye ramani, maana star times imeuza ving'amuzi vingi sana kwa wananchi wa kawaida kabisa ambao sio rahisi kwao kuachana na ving'amuzi hivyo na kununua ving'amuzi vya Digitec vya ITV. Ile ngoma inayovuma sana ndiyo inayokaribia kupasuka, hivo ITV msilewe sifa kwa kujifanya kituo no.1 super brand nchini kidogokidogo wananchi watahamia Star tv, TV1, Channel ten na kwingineko ili kukwepa scratches. Asiyekuwepo machoni hatakuwepo moyoni pia si unajua? Kama hii ni hujuma ya serikali na TBC kwa ITV hamna budi kuwaomba radhi wapenzi wenu walioko startimes kwa usumbufu wanaoupata badala ya kukaa kimya na kudhani watavitupa ving'amuzi vyao vya startime na kununua DSTV au digitek kwa bei kubwa.
 
Nilijua ni mimi tu labda vijana wamechezea antena ila nikawa bado najiuliza mbona ni ITV na EAST Africa tu
 
Shida yake usikimbilie kuilaumu ITV,yenyewe inachofanya ni kuwapelekea feed hao startimes ili waingize kwenye multplexer zao,sasa ujuavyo hao startimes wana interest zao wanaweza wakacheza na hiyo signal watakavyo,umewahi kuona signal ya ITV iki scratch DSTV au TING au ZUKU au Continental au hata Digitek, au hata kwenye dish la kawaida la C band? signal ya ITV ndiyo yenye Quality ya juu kwenye local chanel kwenye sat,hivyo uongozi wa ITV hawapaswi lawama za scratching kwenye ving"amuzi vya startimes,isipokuwa ni startimes na washirika wake
 
Mkuu hata mimi ni hivyo hivyo. Scratch kwenda mbele. Channel nyingine fresh lkn ITV majanga.Malipo niliyolipa juzi ili niangaliae Afcon ndo ya mwisho. Afcon ikiisha nakipiga nyundo nahamia digitek kabisaaa. Pmbavu zao.

Malipo gani hayo umelipia uangalie afcon?
Mbona tbc2 ndo inaonyesha afcon na inaonyeshwa bure tuu hiki kipindi cha afcon au ni ishu nyingine unaongelea.
 
Afu hivi karibuni tangu itv ianze kukwaruza startimes kuna tangazo huwa nalisikia kwenye redio zao kuwa inashika kwenye decoder za digitek sijui dstv ting azam easy tv sijui na nini huko ila startimes haitajwi sijui ni kwanini wakati startimes ipo nahisi kuna issue flani kati ya mgt ya itv na startimes
 
Shida yake usikimbilie kuilaumu ITV,yenyewe inachofanya ni kuwapelekea feed hao startimes ili waingize kwenye multplexer zao,sasa ujuavyo hao startimes wana interest zao wanaweza wakacheza na hiyo signal watakavyo,umewahi kuona signal ya ITV iki scratch DSTV au TING au ZUKU au Continental au hata Digitek, au hata kwenye dish la kawaida la C band? signal ya ITV ndiyo yenye Quality ya juu kwenye local chanel kwenye sat,hivyo uongozi wa ITV hawapaswi lawama za scratching kwenye ving"amuzi vya startimes,isipokuwa ni startimes na washirika wake
Hongera mkuu,leo maneno yako haya yamethibitika pasipo shaka,kumbe ccm na startimes/tbc ndiyo wanaofanya hujuma kwa kituo hiki bora na kinachozingatia weledi,leo wameumbuka.
 
ITV wametoa tamko kuwa tatizo la itv kutoonekana vzr star times wanaohusika ni wao star times. Kinachoonekana ni kama hujuma ili watu wasiangalie habari itv
 
Mi inakaribia mwezi sasa ni shidaa, ITV kulikon?
Ni hujuma ndugu yangu,hawa startimes na tbc+ccm hawataki habari za ukweli na uwazi zinazoonyeshwa na ITV,leo mkurugenzi wa itv/redio one amethibitisha hilo kwa ushahidi usio na chembe ya shaka,heri mimi niliwashtukia hao vibaraka wa ccm mapema nikahamia zangu dstv na Azam tv,kwangu itv ni kama oxygen ipo muda wote,bila tone la scratch-stuck.
 
Mimi nina karibia wiki mbili nikajua ni kwangu tu kumbe ni hujuma!! Watanzania kazi tunayo.
 
Ukiona inafikia muda unaongoza kwa kutumia nguvu, wizi, hila, husuda, fitna na mambo yafafanayo na hayo ujue mwisho wako umekaribia.....
 
Back
Top Bottom