Kusanya ya ombaomba jijini Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusanya ya ombaomba jijini Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhache, Sep 26, 2008.

 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ombaomba limekuwa ni tatizo kubwa katika miji mikubwa kama Dar es salaam. Upitapo maeneo ya Posta mpya, Fire na Magomeni utakutana na kundi kubwa la ombaomba vijana, watoto na wazee na hata watu wa makamo. Idadi yao inaongezeka kila kukicha.

  Leo nimepita maeneo ya Magomeni na kukutana na gari ya manispaa ikiwa inawakamata ombaomba. Sikujua wanawapeleka wapi baada ya kuwakamata? Inawezekana wanawakamata na kuwarejesha makwao. Je hii kamata kamata itakuwa endelevu? Au ni nguvu ya soda. Mimi ningeshauri wapelekwe mahali wafundishwe jinsi ya kujitegemea na kazi ngumu ikiwemo kuwafunga. Kwani warudishwapo makwao hawakawii kurudi mijini.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Wamkusanye na Kikwete ambaye kila kukicha hupita na kopo lake US kwenda kuomba.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,764
  Trophy Points: 280
  Leo nimepita maeneo ya Magomeni na kukutana na gari ya manispaa ikiwa inawakamata ombaomba. Sikujua wanawapeleka wapi baada ya kuwakamata? Inawezekana wanawakamata na kuwarejesha makwao. Je hii kamata kamata itakuwa endelevu? Au ni nguvu ya soda. Mimi ningeshauri wapelekwe mahali wafundishwe jinsi ya kujitegemea na kazi ngumu ikiwemo kuwafunga. Kwani warudishwapo makwao hawakawii kurudi mijini.

  WALE MACHINGA WAPO KRKOO?????????
   
 4. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mi sidhani kama kuwarudisha itasaidia,
  Ukimrudisha mtu kijijini kwao ukampa na kazi ya kufanya, kama kipato kitakua ni kidogo kuliko alichokua anapata Dar es Salaam, basi ujue lazima atajitahidi kurudi kwenye kazi yake ya zamani.

  Mi naomba labda sisi Watanzania tujirekebishe, HAMNA KUMPA HELA OMBAOMBA
  sio vibaya kuwasaidia wale wenye vilema. Mtu mzima kwa nini aombe??

  Hawa watu wana dharau sana, kuna siku nilimwambia ombaomba akae aagize chakula nitamlipia akakataa, akasema anataka hela. Kilichoniudhi alikua kipofu yuko na mtu anamsindikiza mzima kabisa. Nikamwambia kama unataka hela mwambie huyo anayekutembeza afanye kazi akupe. Nikamwambia aende kulala na huyo mwenzie aende
  kufanya kazi. Mwanaume mzima unatembea siku nzima juani unaomba??

  kama ni kuwasaidia, ni bora umnunulie muhogo wa kuchoma kuliko umpe hela
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani kukaa mjini kuna raha yake,suala hapa ni jinsi unavyoishi mjini yaani what are you doing for a living.Of course hata mie wananikera sana hasa hawa walofikia hatua ya kuvua sura ya aibu na kuingia kuomba tena kwa kudanganya katika nyumba za ibada.

  Hapa suluhisho ni maisha bora kwa kila mtanzania,kwani hata kama ningekuwa mie ningerudi tuuuu.
   
 6. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya maelezokuhusiana na omba omba yamenifanya niwaze ka upeo wambali zaidi na kujiuliza hivi kwani kupita pita na kuomba ni jambo baya ?hawa binadamu au wananchi wa kawaida maisha magumu yamewafanya wawe waombaji sasa usiwe mkuki kwanguruwe tu Serekali ya Tanzania inasifika kwa kuomba omba kila kona ya ulimwengu sasa huyu binadamu wa mitaani akiomba eti aondolewe badala ya kusaidia tumeona wapi jamani au ndio wafrika tumehafilika ??
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Je hawa waliozaliwa Dsm na ambao Dar ni kwao serikali/manispaa watawarudisha wapi?
   
 8. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ombaombao limekuwa ni kero kwa sababu linaharibu mandhari ya jiji. Mgeni kutoka nje ya nchi anapokewa na ombaomba wachafu kama maji ni tatizo sana. Akiondoka atakuwa na picha gani kuhusu Tanzania kisiwa cha amani. God Bless Tanzania.
   
 9. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  MHACHE,mgeni toka nje,hakuna cha kumficha,yote anayajua,hili ndio tatizo la sisi watanzania,tunatazama the smaller picture,kikwete akiwa nje ana ombaomba ni worse kuliko hao unaowasema.its time tujifunze kutazama the bigger picture otherwise we will always develop backwards
   
 10. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Kama serikali imechoshwa na kukerwa na ombaomba wa ndani kiasi cha kuwakamata na kuwarudisha makwao kwenye ufukara wa kuchosha walioukimbia ambao unasababishwa ama kuchagiwa na UFISADI, sipati picha JK nawe unapoenda kwa wajomba wa nje kuomba wanakufikiriaje!
   
 11. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Atapata picha halisi mkuu. Ukweli ndio huo maana hata serikali yetu inaendeshwa kwa kutumia asilimia fulani inayoombwa toka nje. Usineelewe vibaya labda kuombaomba ni katabia (kabaya) kilichojikita kwetu.
   
 12. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  With all respect to industriousness and a personal work ethic that detest the entire idea of living on handouts, I have to say that the government is not only unjustifiably punishing victims of it's own poor economic plans, but also that this is an unconstitutional violation of human rights with regards to Tanzanian's freedom of movement within the country.

  You can tell a lot about a society by how it treats the poorest of the poor. I am sure even in an environment with 1% unemployment you will still find people begging, but if adequate standards of human rights cannot be maintained during the entire exercise then it is better not to conduct the exercise at all.

  For example, how do you tell ombaomba from non-omba omba? How do you ensure the exercise is meaningful and they won't be back in a matter of weeks? What if they say they are Tanzanian citizens, exercizing their freedom of movement in the republic and soliciting help peacefully from sympathetic people without breaking any constitutionaly sound law? Under what law exactly are they "internally displaced"? Isn't "Uzembe and Uzururaji" too vague and potentially unconstitutional?

  I say if the government wants to solve this problem it has to look at the root of the problem.Poverty in rural Tanzania, low GDP per capita, low productivity, poor social services etc.

  Once you solve these problems, the influx of ombaomba would not be as pandemic and then the government can genuinely make a case, although indeed the spectre of the thorn of unconstitutionality will linger.
   
Loading...